Rais Dkt John Pombe Magufuli
akimsindikiza Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo baada ya
kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017
*******************
RAIS John Magufuli ameendelea kupokea pongezi
kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo leo Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun
Obasanjo amempongeza kwa kuonesha mfano bora katika Bara la Afrika katika
kusimamia uchumi na kutetea maslai ya nchi katika uwekezaji.
Rais Mstaafu Obasanjo ametoa pongezi hizo muda
mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar
es Salaam leo.
Obasanjo amesifu juhudi za Rais Magufuli
kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali duniani na
kusimamia ipasavyo sera ya kuhakikisha nchi inanufaika, badala ya kuacha
wawekezaji wakijinufaisha wenyewe na nchi kuambulia kiasi kidogo cha mapato.
“Nimepita katika nchi kadhaa zikiwemo Msumbiji,
Malawi na sasa nipo hapa Tanzania, na huko kote nazungumzia masuala ya uchumi
na namna nchi zetu za Afrika zinapaswa kunufaika na uwekezaji katika maeneo
mbalimbali.
“Uchumi wa Tanzania unakwenda vizuri sana, na
juhudi za Rais Magufuli za kuhakikisha nchi yake inanufaika na uwekezaji ni
suala muhimu sana na la mfano, ameonesha mfano mzuri kwa viongozi wa Afrika na
hii ndio njia pekee itakayotuwezesha kukuza uchumi wetu, hatuwezi kuendelea
kuwaacha wawekezaji wananufaika wao na sisi kuambulia kiasi kidogo sana”
amesema Rais Mstaafu Obasanjo.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ameridhia ombi la
Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Mwendwa Judith Malecela kujiuzulu wadhifa wake.
Rais Magufuli ameridhia kujiuzulu kwa Mwendwa
Judith Malecela kuanzia leo Juni 20, 2017.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment