Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 31 January 2017

NOGESHA UPENDO YA VODACOM YAFIKIA TAMATI


Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya Promosheni ya”Nogesha Upendo”jana jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya washindi  400 wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1/-kila mmoja na zaidi ya wateja 1200 wamejishindia shilingi laki 1 kila mmoja  kupitia promosheni hiyo iliyofikia tamati jana ambayo iliwawesha wateja wa kampuni hiyo kuzawadiwa dakika za muda wa maongezi, MB za intanenti bure na  fedha taslimu pindi wakijiunga na kifurushi chochote cha mtandao huo,Kushoto ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo,Mosi Nassoro.
 ***************
Promosheni ya ‘Nogesha Upendo’ iliyozinduliwa mwezi uliopita imemalizika leo ambapo imewawezesha
 watumiaji  wengi wa mtandao huo kujishindia fedha taslimu na vifurushi vya muda wa maongezi na intanenti.Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,amesema kuwa promosheni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kufanikisha lengo lililokusudiwa na kuwapa watumiaji wa mtandao huo zawadi ya kipekee.“Hadi kufikia sasa  wateja wapatao 400  wameweza kujishindia fedha taslimu shilingi milioni 1/-kila mmoja na wateja zaidi ya 1,200 wamejishindia fedha taslimu shilingi laki 1/-kila mmoja na wapo maelfu ya wateja ambao wamezawadiwa dakika za muda wa maongezi na MB za intanenti bure”.Alisema Nkurlu.Alisema Vodacom inayo furaha kuona promosheni hii imewezesha maisha ya wateja wake kuwa murua na itaendelea kubuni promosheni nyingine zenye lengo la kubadiilisha maisha ya wateja nahuduma mbalimbali za kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.”Tunawashukuru sana wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii kwa kuendelea kuwa katika familia ya Vodacom na tunawaahidi kuendelea kuwapatia huduma bora wakati wowote na mahali popote.


USAJILI KILI MARATHON KUFANYIKA MLIMANI CITY


Na mwandishi wetu

Usajili wa mbio maarufu za Kilimanjaro Marathon sasa utaanznia jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mlimani City, imefahamika.


Muandaaji mkuu na muanzilishi wa mbio hizo, John Addison alisema usajili huo utaania Mlimani City na hii itakuwa mara ya kwanza kwa zoezi hilo kufanyika jIjini Dar es Salaamtangu kuanzishwa kwa mbio hizo miaka 15 iliyopita. 
  

Alisema usajili huo utafayika Februari 18 na 19 eneo la kuegesha magari mbele ya mgahawa wa Grano pembeni ya KFC kuanzia saa nane mchana hado saa mbili usiku. “Tunaamini watu wengi watajitokeza kwa sababu itakuwa mwishoni mwa wiki,” alisema na kuongeza kuwa hii itapunguza msongamano wa usajili Mjini Moshi.


Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastors Mrosso alisema wanajivunia kuwa wabia wa Kilimanjaro Marathon ambazo kwao ni mbio kubwa na wanaamini watu wengi watajitokeza kujisajili na pia kutembelea maduka mbalimbali na kupata huduma kutoka Mlimani City. 


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye ni mdhamini mkuu aliwapongeza waandaaji kwa kuanzisha usajili wa Dar es Salaam na kusema itarahisisha zoezi zima na kuhakikisha kila mtu anasajiliwa kwa wakati na kuepusha msongamano wa watu siku za mwisho.


Umie Naye Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini, George Lugata aliwataka washiriki wote watumie fursa hii vizuri ili waweze kushiriki katika mbio hizi.


Kwa mujibu wa Bw. Addison, Usajili Arusha utafanyika Kibo Palace Hotel Februari 21 na 22 kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usikuna Moshi usajili utafanyika Keys Hotel  Februari 23 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 24 (saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni) na Februari 25 (saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana).


“Tumeongeza siku za usajili kwa vituo vyote ili watu wengi zaidi watumie fursa hii na kuepusha msongamano wa watu Mjini Moshi tunawaomba washiriki wote watambue kuwa safari hii usajili utafungwa mapema kabisa kwani hakuna usajili utaendelea baada ya saa sita mchana Februari 25,” alisema Bw. Addison.Wadhamini wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-walemavu, Grand Malt-5km. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.


Mbio za mwaka huu zitafanyika Februari 26 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.


PATA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016 HAPA

Baraza la Mitihani la Taifa leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne 2016 kuona matokeo hayo bofya hapa.

MATOKEO YOTE HAYA HAPA CHINI  

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2016

MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2016
ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi.
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 

Na Richard Mwaikenda
MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


WABUNGE WAPYA WANNE WALAKIAPO CHA UAMINIFU BUNGENI LEO

Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Anne Kilango Malecela, akila kiapo cha uaminifu Bungeni mjini Dodoma leo. Jumla ya wabunge wanne walikula kiapo chao mbele ya Spika wa Bunge hii leo ambapo kati yao watatu ni wakuteuliwa na Rais na mmoja wa kuchaguliwa na wananchi kutoka jimbo la Dimani.
 Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Alhaji Abdalah Bulembo, akila kiapo cha uaminifu Bungeni mjini Dodoma leo
 Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, akila kiapo cha uaminifu Bungeni mjini Dodoma leo
Mbunge wa jimbo la Dimani  Zanzibar, Juma Ali Juma akila kiapo cha uaminifu Bungeni mjini Dodoma leo
 Wabunge mbalimbali wakiingia Bungeni mjini Dodoma leo.
 Wabunge mbalimbali wakiingia Bungeni mjini Dodoma leo.


Monday, 30 January 2017

LWENGE AZINDUA MPANGO WA MALIPO YA HUDUMA ZA MAJI KWA MATOKEO

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh Milioni 28.1 kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Deus Mchele na Mhandisi wa Maji Wilaya, Grace Mukulasi fedha za kusaidia maboresho ya huduma za maji. Halmashauri 57 nchini zilipatiwa fedha chini ya Mpango wa Malipo ya Maji kwa Matoeo uliozinduliwa jana kitaifa mkoani Dodoma.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh Milioni 28.1 kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Deus Mchele na Mhandisi wa Maji Wilaya, Grace Mukulasi fedha za kusaidia maboresho ya huduma za maji. Halmashauri 57 nchini zilipatiwa fedha chini ya Mpango wa Malipo ya Maji kwa Matoeo uliozinduliwa jana kitaifa mkoani Dodoma.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Malipo ya Maji kwa Matoeo uliozinduliwa jana kitaifa mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Malipo ya Maji kwa Matoeo uliozinduliwa jana kitaifa mkoani Dodoma.
 Waziri Lwenge akizungumza na Naibu Waziri Jafo wakati wa uzinduzi huo.
 Kundi la Burudani la Simba Dume kutoka Chihanga mkoani Dodoma likitoa burudani.

 Wa
 Kundi la Burudani la JKT Makutopora nalo liliburudisha halaiki. SOMA ZAIDI HAPA


MKUTANO WA 6 WA BUNGE KUANZA KESHO, WABUNGE 4 KULA KIAPO, MASWALI 125 KUULIZWA NA 16 YA PAPO KWA PAPO KWA WAZIRI MKUU

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Masiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akizungumza na wanahabi mjini Dodoma leo akitoa taarifa ya yale yatakayojiri katika Mkutano wa sita wa Bunge la 11 unaotaraji kuanza kesho Januari 31 hadi Februari 10 mwaka huu mjini Dodoma.
***************

Mkutano wa Sita wa Bunge unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 31 Januari 2017 na kumalizika tarehe 10 Februari 2017 Mjini Dodoma. Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-

1.0         KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-

(i)         Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
(ii)       Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
(iii)      Mhe. Anne Kilango Malecela
(iv)    Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)

2.0         MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.3.0       KAULI ZA MAWAZIRI
Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa  kama ifuatavyo:-

(i)     Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

(ii)   Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

4.0       MISWADA YA SHERIA
Katika Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika mwezi Novemba, 2016 Miswada mitatu (3) ya Sheria ilisomwa  kwa mara ya Kwanza Bungeni na kupelekwa kwenye Kamati husika ili ifanyiwe kazi.

Hivyo katika Mkutano huu wa Sita Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mara ya Pili, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 91. Miswada hiyo ni:-

  1. Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).

  2. Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

  1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)


Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
30 Januari, 2017.


TANZIA: MLINDA MLANGO DAVID BURHAN WA KAGERA SUGER AFARIKI DUNIA

 David Burhan enzi za uhaibwake akiwa mazoezini.
David Buruhan kipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki leo Januari 30,2017 katika Hospital ya Bugando Mwanza.

Burhan inadaiwa kua aliumwa ghafla wakiwa njiani kuelekea Singida kwenye mechi ya Azam Federation Cup. Na waliporudi Kagera hali yake ikazidi kuwa mbaya na hivyo kukimbizwa Bugando. 

Hii ni kwa mujibu wa Kocha wake Mecky aliyenipigia asubuhi hii.


MALIASILI NA UTALII NDANI YA HABARILEOSunday, 29 January 2017

TRENI YA TRL YAPATA AJALI LEO MABEHEWA MANNE YAANGUKA KADHAA WAJERUHIWA

 Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa imepata ajali leo na mabehewa yake tisa kati ya hayo manne kuanguka kabisa.

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)umetoa taarifa kuwa leo  Januari 29, 2017 mnamo  saa 9:40 alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali . 

Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia.

Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika.


Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame  Mbarawa  .Mkuu wa TRL Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi , Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S. Chillery wako  katika eneo la ajali! .

Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es Salaam na  inatarajiwa kuwasili saa 2 usku.

Aidha  uongozi wa TRL umehakikisha umma na wateja wake kuwa njia ya reli  kati ya Ruvu na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji  zirejee kama kama kawaida.


15 WALIOFUKIWA MGODINI GEITA WAOKOLEWA HAI

 Waokoaji wakiwanasua wachimbaji kutoka katika kifusi kilichowafunika ardhini.
 Wachimbaji wakiwa wameokolewa na wakipatiwa huduma ya kwanza.
 Jopo la Madaktari na wauguzi wakiendelea kuwapa huduma.
Watu wa 15 waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa Dhahabu wa RZ Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa hai.

Leo asubuhi timu ya waokozi ilitoboa shimo hadi eneo walilokwama watu hao na kutumbukiza tochi na redio ya mawasiliano kwa kutumia kamba na ikarudi juu ikiwa tupu. "Tumeshusha tochi na radio via drill hole ,kamba ikarudi tupu means vimepokelewa lakini kwenye radio awasikiki," ilisema taarifa kutoka eneo la tukio.

Aidha waokoaji walishusha  barua peni na karatasi kupitia shimo hilo na vitu hivyo vikapokelewa  na kurejesha majibu kuwa wote 15 wazima isipokuwa mmoja amechomwa na msumari na kuorodhesha majina yao nankuimba chakula.

Timu ya madaktari walishauri wasipewe chakuka bali dripu tu wanatakiwa wanywe mana awajala siku mbili.

Kwa sasa zinashushwa dripu maalum za maji kupitia shimo hilo.y


MWENYEKITI MPYA WA TUME YA UMOJA WA AFRIKA KUOATIKANANKESHO ADIS ABABA ETHIOPIA

Nani kukalia kiti cha Tume ya Umoja wa Afrika (AU)?

Swali hili litajibiwa Jumatatu, Januari 30, wakati wajumbe kutoka nchi wanachama 54 watakapoketi na kupiga kura.

 Morrocco nayo inataka uanachama wa AU na huenda kura yake ikawa na umuhimu katika kumchagua mwenyekiti mpya endapo itajumuishwa. 

Mwenyekiti anaemaliza muda wake ni Dr Nkosanzanz Dlamini Zuma, na tayari wagombea watano wameonesha nia ya kuitaka nafasi hiyo akiwepo Wazi wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed.

Wengine walioweka wazi kuwania nafasi hiyo ni Mwanadiplomasia na msomi wa Senegali, Abdoulaye Bathily, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, Mwanasiasa mkongwe wa Botswana, Pelonomi Venson-Moitoi lakini pia yupo aliyekua mshauri wa Rais wa Guinea, Mba Mokuy.


Saturday, 28 January 2017

RAIS MAGUFULI AENDA ETHIOPIA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa  Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam. *****************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 28 Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Paul Makonda.

Pamoja na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria Mkutano huo.

Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe. Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki tangu aingie madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05 Novemba, 2015


VITUO VYA TRA VYA KUHAKIKI TIN KUFUNGULIWA JUMAMOSI NA JUMAPILI

TAARIFA KWA UMMA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwajulisha wadau na umma kwa ujumla kwamba vituo vya kuhakiki Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) vitakuwa wazi siku ja jumamosi tarehe 28  Januari 2017 kuanzia saa 3:00 hadi 11:00 jioni na jumapili tarehe 29 Januari 2017 kuanzia saa 4:00 hadi saa 9:00 Alasiri.

Vituo hivyo kwa Ilala ni TRA Samora, 14 Rays - Gerezani na Shaurimoyo. Kinondoni ni Millennium Tower Kijitonyama, Kibo complex- Tegeta na Ofisi ya Kodi Kimara. Temeke ni Uwanja wa Taifa, Ofisi ya Kodi Kigamboni na Ofisi ya Kodi Mbagala.

Aidha Mamlaka inaukumbusha  umma kwamba tarehe ya mwisho wa kuhakiki TIN ni tarehe 31 Januari 2017. Hivyo ni vyema kwa wale wote ambao hawajahakiki TIN kufika katika vituo tajwa mapema ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza baada ya zoezi kufungwa rasmi 

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi 
TRA - Makao Makuu


SERIKALI KUTUMBUA WAHUJUMU WA TAZARA

Meneja wa Karakana ya Dar es Salaaam ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Eng. Timothy Kayani, akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa vipuri vya treni vilivyotengenezwa katika karakana hiyo jijini Dar es Salaam, alipotembelea karakana ya Mamlaka hiyo kuona utendaji wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), alipotembelea mamlaka hiyo kuona utendaji kazi.
 ************************
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa  Makame  Mbarawa  amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambaye ataendelea kuisababishia hasara Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuendelea kuihujumu na kusababisha mamlaka kujiendesha kwa hasara.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Tazara, kuangalia utendaji ambapo amebaini matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua stahiki.

“Ninafahamu kuna watu 10 hapa ambao wao ni chanzo kikubwa cha matumizi mabaya ya fedha na miongoni mwao wapo Watanzania na Wazambia, nawahakikishia kuwa kila atakayetumia vibaya fedha zinazotolewa na Serikali hatutamvumilia kwenye Serikali hii’, amesema Prof. Mbarawa.

Profesa Mbarawa amesema kumekuwa na idadi kubwa ya watumishi ambao hawana tija  na kuagiza menejimenti ifanye uhakiki na kubaini mahitaji halisi ya Watumishi na watakaobainika kuzidi wahamishiwe ofisi ya tazara Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Prof. Mbarawa ameuagiza uongozi wa Tazara Makao Makuu kuacha mara moja kutumia mtandao ya kampuni binafsi kutuma taarifa za Ofisi na kuagiza kuanza kutumia mtandao wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara moja.

‘Nikirudi tena hapa sitaki kuona mnatumia mitandao wa Kampuni binafsi kutuma taarifa za kiofisi ninawaomba muhakikishe mnatumia  mtandao wa TTCL’ amesisitiza Prof. Mbarawa.
 
Kwa upande Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Bw. Fuad Abdalla amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa na Mamlaka inajiendesha kibiashara.

‘Kama mkoa tumekuja na mikakati mizuri ya kutumia mifumo ya Tehama kama njia ya  udhibiti wa mapato, kama ulivyona hivi sasa tunakamilisha mfumo wa Tehama tunaoutumia kufatilia treni kila inapoondoka kwenye Stesheni ya Makao Makuu Dar es Salaam na mfumo huu ukikamilika tutawaashawishi na wenzetu wa Zambia kutumia mfumo huu ili tuweze kudhibiti upotevu wa mapato’ Amesisitiza Bw. Fuad Abdalla.

Bw. Fuad ameongeza kuwa pamoja na mifumo mipya ya Tehama Tazara inaendeleza kwa kasi ukarabati wa mabehewa ya abiria na mizigo ili kuongeza tija na kuiwezesha Mamlaka kupata faida.


Friday, 27 January 2017

UHAMIAJI WATAKIWA KUCHUNGUZA KAYA 180 ZILIZOINGIZWA KATIKA MPANGO WA TASAF WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WILAYANI KAKONKO

 MKUU  wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma, Kanal Hosea Ndagala akizungumza na mmoja wa wananchi katika vijiji vya Kata ya Nyabibuye alipotembelea.
MKUU  wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma, Kanal Hosea Ndagala ameitaka Idara ya Uhamiaji kuharakisha kufanyia  Uchunguzi kwa  kaya 180 ambazo zilizobainika kuwa na wakuuu wa kaya ambao walidhaniwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.
 
Kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu  uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

Kauli hiyo aliitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Wataanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

Ndagala alisema  kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitisha na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa  kuchukuliwa hatua .

"Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache moja wapo ikiwa  wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanarumia kunywea pombe na mambo mengine nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki  majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ilikuweza kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.

Sauda Lumala ni Mmoja kati ya Wanufaika alisema kwa upande wake alipo pokea fedha za TASAF alinunua Mbuzi na bata ambapo Mpaka sasa anajumla ya Mbuzi  watatu na bata kumi alizo zalisha kupitia miradi ya kusaidia Kaya masikini.

Alisema changamoto wanayo kumbana nayo katika suala zima la kuanzisha miradi baadhi ya Wanawake wengi wakipokea fedha hizo waume zao wanawanyang'anya na kuzifanyia mambo yao binafsi hali inayopelekea kushindwa kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizo kusudiwa.

Nae Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kakonko, Maria Tarimo  alisema mpaka sasa kuna jumla ya wanufaika 7775 katika wilaya ya Kakonko zinanufaika na mpango huo ambao umeleta manufaa makubwa na wengi wao wameanza kufikia malengo yaliyopangwa na wameanzisha miradi endelevu itakayo wasaidia kupambana na umasikini.
 
Alisema katika uhakiki wa Kuwaondoa watu wasio stahili katika Mpango huo waliobainika ni  watu 180 wanaozaniwa kuwa sio Raia ambao wataondolewa kwenye mpango huo na watatakiwa kurudisha fedha walizo kwisha kuzichukua kinyume na utaratibu.


TRA yatwaa Tuzo ya Ubunifu wa Miradi kwa Sekta za Afrika.

 Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya  Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wamfumo wa TANCIS kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga. Mfumo huu wa TANCIA umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha.
 *****************
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepata tuzo kutoka Umoja wa Afrika (AU) kutokana na mfumo wa Uondoaji Mizigo Bandarini (TANCIS) ambao unafanya kazi kwa ufanisi na uharaka zaidi pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa.

Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Nchi za Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia,   baada ya kufanyika shindano la Taasisi za Serikali za Umoja wa Nchi hizo kutokana na kuboresha mifumo ya utendaji kazi katika taasisi zao.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kisiga amesema kuwa TRA na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ndiyo taasisi pekee za Serikali zilizoweza kufanya vizuri katika ubunifu katika utendaji wa taasisi hizo.

“Tuzo hizi zinatolewa na nchi za Umoja wa Afrika kwa taasisi za Serikali ambapo hushindanishwa katika masuala ya ubunifu katika utendaji kazi wa taasisi husika,” alisema Bi. Mindi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata,  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo alisema TRA imeshinda tuzo hiyo kutokana na ubunifu wa mfumo wa TANCIS ambao umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha. 

Alisema mfumo huu umeunganishwa na mifumo mingine ya TRA na ya wadau muhimu ambao wanahusika katika uondoshaji wa bidhaa katika udhibiti wa forodha .

“Mfumo wa TANCIS humwezesha mwagizaji wa bidhaa kufuatilia hatua iliyofikiwa  katika kuondosha bidhaa zake kwa kutumia simu ya kiganjani au kifaa kingine chochote cha kielektroniki hivyo mfumo huu unarahisisha utoaji huduma na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Bw. Kayombo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde alisema kuwa taasisi yake imepokea tuzo hiyo  ya ubunifu kwa kupitia mfumo wa kanzidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Alisema TRA iliwawezesha kupata taarifa zilizohusu walipajikodi wa (PAYE) ambazo zilifanikisha uchambuzi wa waajiri wasiochangia Mifuko ya Jamii.

TRA na SSRA wameahidi kuendelea na ubunifu zaidi ili kuhakikisha wanaendelea kubaki katika nafasi ya ushindi na kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.