Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 13 October 2019

MIAKA SABA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

 Ukurasa wa kuingia (log in page wa Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Raslimali za Taasisi 
 UVUMBUZI wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) umeleta fursa za maendeleo kwa mtu binafsi au kwa taasisi husika na faida nyingi zisizomithilika katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli mbalimbali na maisha kwa ujumla TEHAMA imekuwa ni njia mbadala ya kuhudumia wananchi na inapotumiwa na taasisi za umma katika utekelezaji wa shughuli zake na katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na kwa gharama nafuu ndiyo hujulika kama serikali mtandao.

Hivyo, Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inapata faida zitokanazo na matumizi ya TEHAMA kwa ufanisi, iliamua kuundaa taasisi mpya ambayo ilipewa majukumu ya kuratibu na kusimamia matumizi sahihi ya TEHAMA katika taasisi za umma ili ziweze kunufaika ipasavyo katika kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hivyo, kwa kuzingatia hili Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mh. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb), anasema Serikali ilianzisha Wakala ya Serikali Mtandao iliundwa kwa mujibu wa sheria Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997 chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikuwa na jukumu la kusimamia serikali mtandao na kuratibu maendeleo ya TEHAMA ndani ya Serikali na taasisi zake, baada ya kupitia matokeo ya tathmini ya hali halisi ya matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za serikali ambapo taasisi nyingi zilionyesha kujitengenezea mifumo na raslimali nyingine za TEHAMA bila kujali uwepo wa jitihata hizo katika taasisi nyingine. Hali hiyo ilichochea kuwa na urudufu wa jitihata za TEHAMA zinazofanana na zisizowasiliana wala kubadilishana taarifa.

Akizungumzia hali ilivyokuwa kabla ya Serikali kujikita katika matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma kwa umma, Mhe. Waziri anaelezea kuwa, Serikali mtandao ni nyenzo inayotumika katika kubadili na kuboresha utendaji kazi katika taasisi za umma na utoaji wa huduma kwa wananchi. “Kazi hii sio rahisi kuifanikisha, inahitaji rasilimali za kutosha, utashi wa kisiasa, watumishi waliobadilika kimtazamo na kimatendo ili kuhakikisha serikali mtandao inatumika ipasavyo ndani ya Serikali na taasisi zake (G2G), kati ya Serikali na sekta ya biashara (G2B) na kati ya Serikali na wananchi (G2C). Ili kuyafikia yote haya, tunahitaji kubadili mifumo ya utendaji katika Serikali kwa ujumla”.

Naye Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Bw. Priscus anasema kuwa mwananchi anapata manufaa mengi kutokana na matumizi ya TEHAMA kwa kuwa anarahisishiwa upataji wa huduma mbalimbali hapo alipo bila kutembea umbali mrefu na kwa gharama nafuu. Kwa upande wa taasisi za umma, TEHAMA inarahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika kuhudumia wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt Bakari Bakari akiongea  kuhusu jitihata za utekelezaji wa  Serikali Mtandao - UDOM Dodoma hivi karibuni
Akizungumzia mafanikio ya serikali mtandao yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Wakala ya Serikali Mtandao mwaka 2012 hadi sasa, Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dkt. Jabiri Bakari anaeleza kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa serikali mtandao, husan katika maeneo ya sera, sheria na miongozo, usimamizi, utengenezaji wa mifumo tumizi na ya kimkakati ya TEHAMA, na ujenzi wa miundombinu ya pamoja ya TEHAMA. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI