Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 24 November 2017

MBUNGE GAMA AFARIKI DUNIA

MBUNGE wa jimbo la Songea mjini, Leonidas Gama amefariki Dunia. 

Taarifa kutoka Songea zinasema kuwa Gama amefikwa na umauti usiku wa kuamkia leo mkoani Songea katika Hospitali ya Peramiho ambako alilazwa kwa muda mfupi kufuatia maradhi ya kiharusi ambayo yalimpata juzi usiku akiwa nyumbani kwake huko Likuyu nabaadae kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Gama amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.


Monday, 20 November 2017

IKULU YAKANUSHA KUTENGULIWA KATIBU MKUU UTUMISHI

Taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro sio za kweli na zipuuzwe.

Wananchi endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali, na pia watumiaji wa mitandao ya kijamii mnakumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.

Serikali itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.


Friday, 17 November 2017

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA WAKATI WA KUAHIRISHWA KWA BUNGE NOVEMBA 17, 2017

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge, mjini Dodoma.

Mbungewa Viti Maalum, Hawa Mchafu Chakoma akiulizwa swali Bungeni, mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo akiuliza swali kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, mjin Dodoma.

Wabunge wakjadiliana wakati wa vikao vya Bunge, mjini Dodoma ambalo limeahirishwa leo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Wednesday, 15 November 2017

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA NOVEMBA 15, 2017

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo wakati wa vikao vya Bunge, mjini Dodoma.
   Mbunge wa Viti maalum Tabora, Munde Tambwe akijadiliana na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Bungeni, mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge wakijadiliana.

Baadhi ya wageni wakifuatilia vkao vya Bunge, mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Monday, 13 November 2017

UKOSEFU WA AJIRA WAPUNGUA NCHINI

Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema,  ukosefu wa ajra kwa vijana nchini unazidi kupungua kutokana na juhudi mbalimbali za serkali. 

Amesema hatua hyo inatokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuboresha na kutengeza mazingira yatakayowawezesha vijana kujiajiri.

Mhagama ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/2018 ambapo alisema, tatizo la ajira ni changamoto ya kidunia lakini  serikali imekuwa ikijtahidi kuhakikisha inatengeza mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha program 8rasisimishaji wa ajira ambazo  Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi.


MUHIMBILI KUANZA KUPANDIKIZA FIGO DESEMBA

Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kabla ya Desemba 30, mwaka huu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) itaanza kutoa matibabu ya kupandikiza figo ikiwa ni hatua ya kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi.

Ummy ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018 ambapo amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakibeza juhudi mbalimbali za serkali katika kuboresha huduma za afya.

Amesema kwa sasa Hospitali ya Taifa Munimbili kupitia taasisi zake kwa kiasi kikubwa imepunguza wagonjwa waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi. 

Amesema kipndi cha nyuma Hospitali ya Muhimbili ilikuwa ina uwezo wa kuwafanyia upasuaji watoto 15 kwa wiki lakini sasa hivi ina uwezo wa kuwafanyia watoto 50.


SERIKALI KUPIGA MNADA NG’OMBE 10,000

Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametanga kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 10,000 wa kutoka nchi za Rwanda na Uganda ambao wamekamatwa katika operesheni ya siku saba inayoendelea nchini.

Mpina aliyasema hayo wakati akijivu hoja zilzoibuliwa na wabunge ambapo amesema ng’ombe hao watapgwa mnada kama ilivyokuwa kwa ng’ombe 1,325 wa kutoka nchin Kenya ambao walikamtwa baada ya kungia nchini.

Akichangia Mpango wa Maendeleo ya Tafa wa mwaka 2017/2018, Waziri Mpina amesema, wapo watu wanaosema kuwa  hatua hiyo inaweza kuvuruga mahusiano ya nchi za Afrika Masharki ambapo amesisitiza kuwa uhusiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uko imara na hauwezi kuvurugwa na uhalifu.

“Hakuna ushirika wa uhalifu, watu wanaoingza mifugo kutoka nje ya nchi ni wahalifu kwasababu wamevunja sheria…mhalifu akija hapa hawezi kutetewa kwasababu ya ushirika, ushirika wetu sio wa uhalifu, mashirikiano yetu ni mazuri kwasababu yapo ksheria,” amesema.


ELIZABETH MICHAEL AU LULU NINANI?

MUIGIZAJI na Muongozaji Filamu, Elizabeth Michael (Lulu) ,22, leo amehukumuiwa kifungo cha Miaka Miwili gerezani  baada ya Mahaka Kuu Tanzania, kumtia hatiani kwa kosa la kumuua Bila kukusudia. Anaandika Mroki Mroki wa Daily News Digital. 

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.

Alisema  Aprili 12, 2012 ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Lulu kufikishwa Mahakamani ambapo alifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma za mauaji ya marehemu Kanumba.

Lakini baadae baada ya kusota rumande kwa takribani miezi kumi, Lulu alibadilishiwa mashitaka na kushitakiwa kwa mauaji ya bila kukusudia, shtaka lililomuwezesha kuwa nje kwa dhamana hadi leo.

Tukio hilo lilitokea mnamo Aprili 6, 2012 huko Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam wakati ikielezwa kuwa wasanii hao wawili wakiwa ni marafiki wakaribu.

LAKINI ELIZABETH AU LULU NINANI?


SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA SHERIA ZA KAZI ILI KULINDA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha utekelezaji wa sheria za kazi ili kulinda haki za wafanyakazi wa majumbani pamoja na kujenga uelewa wa wadau kuhusu matakwa ya mkataba na haki za kisheria.

Kauli ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati aliyeuliza kikwazo kinachokwamisha kuridhia mkataba wa Shirika la Kazi Duniani(ILO)namba 189 na kazi za staha kwa wafanyakazi wa majumbani wakati LESCO imeshapendekeza kuridhia. 

Amesema Tanzania kama nchi mwanachama wa ILO ilishiriki kikamlifu katika majadiliano na upitishwaji wa mkataba wa kimataifa wa LO wa wafanyakazi wa majumbani namba 189 wa mwaka 2011 ambao unalenga kukuza kazi za staha kwa wafanyakazi wa majumbani .

“Serikali inathamini mchango wa wafanyakazi wa majumbani katika kujenga uchumi wan chi. Hii ndiyo maana Bunge lako tukufu lilitunga sheria ya Ajira na Mahusiano kazini namba sita ya mwaka 2004 ambayo inazitambua haki za wafanyakazi wa majumbani kama livyo kwa wafanyakazi wengine,” amesema.


Friday, 10 November 2017

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) SASA LAFIKILIA KUJA NA UTALII KWA BODA BODA NA BAJAJI

Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Thursday, 9 November 2017

HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe, wakati akiuliza swali la papo kwa papo, bungeni mjini Dodoma, Novemba 9, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu swali la papo kwa papo, leo bungeni mjini Dodoma, Novemba 9, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kabla ya kuanza kikao cha Bunge mjini Dodoma, Novemba 9, 2017. 
**************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba vyombo vya dola vya ndani ya nchi havijashindwa kuchunguza matukio ya kihalifu yaliyotokea nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na subira.

Amesema Serikali hairidhishwi na matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa, ambayo yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi yake yamesababisha vifo na wengine kujeruhiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2017) wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

Bw. Mbowe alitaka apew kauli ya Serikali juu ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tukio la kushambuliwa na mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, ambapo alishauri uchunguzi huo ufanywe na vyombo vya kimataifa, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya ndani vya dola.

“Vyombo vya ndani vya dola vina uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi na vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu. Nawaomba wananchi waendelee kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola na mara uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa mbalimbali juu ya vitendo vya kihalifu vinavyotokea kwenye maeneo yao kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma imeanza kutekelezwa kwa kuwapandisha madaraja watumishi wanaostahili sambamba na kulipa malimbikizo yao mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema baada ya kumaliza ulipaji wa malimbikizo ndipo Serikali itaendelea na hatua ya uboreshaji wa mishahara kwa watumishi wote wa umma, hivyo amewaomba waendelee kuwa na subira na imani na Serikali. Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Bw. Omary Kigua aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itapandisha mishahara ya watumishi wa umma.

Pia Waziri Mkuu amezungumzia changamoto ya masoko kwa mazao ya mbaazi na tumbaku ambayo yanashughulikiwa na Serikali na tayari baadhi ya nchi zimeanza kuonyesha nia ya kununua mazao hayo, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na uvumilivu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Bibi Munde Tambwe aliyeiomba Serikali kumpatia ufafanuzi juu ya kukosekana kwa soko la tumbaku ambayo imelundikana katika maghala na Bibi Pauline Gekul Mbunge wa Babati aliyelalamikia kukosekana kwa soko la zao la mbaazi.

Akizungumzia kuhusu zao la tumbaku, Waziri Mkuu amesema changamoto hiyo imetokana na wakulima wa zao hilo kuongeza uzalishaji tofauti na makubaliano yaliyofikiwa awali na wanunuzi. “Nawaomba wakulima waendelee kuwa wavumilivu Serikali inafanya mazungumzo na nchi za lran, Korea Kusini, Misri na Indonesia ili waweze kununua tumbaku hiyo na kuwaondolea usumbufu wakulima.”


Tuesday, 7 November 2017

FOUR-DAY TRAINING FOR SOUTH SUDAN MEDIA PROFESSIONALS BEGINS IN ARUSHA

 The Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Dr. Kamugisha Kazaura, officially opened the four-day Republic of South Sudan Media Training workshop at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.
 A section of South Sudanese delegates during the opening session of the Republic of South Sudan Media Training workshop in Arusha.
 Participants at the four-day media training workshop in a group outside the EAC Headquarters in Arusha.
GIZ’s Head of German-EAC Cooperation, Mr. Bernd Multhaup (standing, third right), with South Sudanese delegates to the RSS Media Training workshop at the EAC Headquarters in Arusha.
*******************
A four-day training workshop on the East African Community integration process for Public Communications Officers and journalists from media houses in the Republic of South Sudan (RSS) kicked off at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania today.

The workshop is part of a comprehensive capacity building programme on the integration process to enhance the young nation’s integration into the Community. CLICK HERE TO READ THE FULL STORY.


Monday, 6 November 2017

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA WAKURUGENZI WAWILI BUKOBAAMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI


Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo.
Mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo 

Wazazi hususa ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae

Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha

Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu kutokana na kufichwa huko

“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina

Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule

Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii wanaweza kuwa viongozi wakubwa wa serikalini hapo baadae

Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri

“napenda kuwasihi ndugu zangu wamasai kuachana na mila za kizamani kama vile ukeketaji na kuozesha watoto wa kike mapema kwani swala hilo sio jema na limepitwa na wakati na napenda kuwataka wananchi wote hususa ni ndugu zangu wamasai kuwafichua wale wote ambao bado wanaendeleza mila za zamani kama vile ukeketaji”Alisisitiza Amina


UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WAANZA KUTANGAZA UTALII WA NDANI KUSINI MWA TANZANIA KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto).
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania - CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto) akitolea ufafanuzi wa masuala mbali mbali jinsi umoja wao ulivyo na lengo kuu la kuweza kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.  Halfa hiyo iliyofanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam.
Burudani ya ngoma ikiendelea. Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akiingia ukumbini. Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (mwenye tai nyekundu) akiwa na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri wakiwa katika picha ya pamoja na wanaumoja wa CAAT. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Source: Kajunason


Friday, 3 November 2017

NAURI MPYA ZA MABASI YA MIKOANI HIZI HAPAWAWILI WAFA AJALINI WAKIWAHI KESI MAHAKAMANI ARUSHA

Gari dogo aina ya Toyota Mark X T 796 DFG walilokuwa wakisafiria David Chijana (33) aliyekuwa akiendesha gari hilo na James Alfed (40) wakazi wa Dar es Salaam.
 Gari baada ya kupata ajali.
WATU wawili wamekufa papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria Toyota Mark X T  namba za usajili  T 796 DFG kupata ajali USA River jijini Arusha leo mchana. Anaandika Mroki Mroki.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo inayosemekana ilikuwa ikitokea dar es Salaam kwenda jijini Arusha.

Mmoja wa waliopoteza maisha ni David Chijana Karani wa Idara ya Ufundi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Aidha taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Chijana aliondoka jijini Dar es Salaam jana jioni kwenda Arusha kuhudhuria kesi ya mirathi.

Chanzo kingione kinasema kuwa David alikuwa akiwahi Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo mama yake alikuwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakisomewa hukumu ya kesi ya Wizi Benki ya Exim ambapo hata hivyo alikuhukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,  Charles Mkumbo amethibisha kutokea kwa vifo hivyo na kuwataja marehemu kuwa ni David Chijana (33) aliyekuwa akiendesha gari hilo na James Alfed (40) wote wakazi wa Dar es Salaam.

 Kamanda Mkumbo alisema chanzo cha gari hilo ni mwendo kasi ambapo kabla ya ajali iligongana na gari aina ya Noah kasha kuruka juu  na kusababisha vifo katika eneo la River Tree Kata ya Pori kwenye barabara ya Moshi /Arusha na ilitokea  saa 4:35 asubuhi.


Thursday, 2 November 2017

RC MAKONDA AFANYA KIKAO NA TANESCO, AWAGIZA KUTATUA KERO ZA UMEME KWA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefanya kikao na Mameneja wa TANESCO Kanda zote za Dar es Salaam kujadili mkakati wa kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme na maboresho ya miundombinu ya Umeme.

Lengo la kikao hicho ni kujadili mahitaji ya Umeme kwa Mkoa, Kero ya kukatika umeme mara kwa mara (Mgao), Mpango Mkakati wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na Mvua zinazoendelea kunyesha na Mpango mkakati wa kuhakikisha Taasisi zote za Umma ikiwemo Shule, Vituo vya Polisi na Vituo vya Afya vinakuwa na Umeme wa Uhakika.

Makonda amesema kuwa kukatika kwa umeme imekuwa kero kubwa kwa wananchi na wakati mwingine kusababisha hasara hivyo anaamini TANESCO ya sasa chini ya Serikali ya awamu ya Tano itamaliza kero hizo.

Katika kikao hicho TANESCO wamemuahidi Mkuu wa mkoa kuwa umeme utaongezeka kuanzia leo Maeneo yote yaliyokuwa yakisumbuliwa na upatikanaji wa Umeme hali itakuwa Shwari kuanzia leo.

Kuhusu suala la Umeme mashuleni wamekubaliana kuandaa mchanganuo wa mahitaji yanayohitajika kisha kufikisha ofisini kwake ili kila shule iunganishwe na huduma ya umeme.

Makonda amewataka kuwa na lugha nzuri kwa wateja na kufika kwa wakati pindi wanapopewa taarifa za hitilafu ya umeme.

Kwa upande wake Meneja mwandamizi TANESCO Dar es Salaam na Pwani Eng.Mahende Kugaya amemuahidi Mkuu wa mkoa kuwa watatekeleza yale yote waliyoagizwa kuanzia siku ya leo ikiwemo kutatua kero za Wananchi za mgao wa Umeme na kufikisha huduma ya umeme kwenye Taasisi zote za umma ikiwemo Vituo vya Polis, Vituo vya Afya na Shule. 

Aidha amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa  kuwa eneo la Mbagala na Kigamboni kuanzia mwezi Disemba watapata umeme wa uhakika.