Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 28 February 2018

TRENI YA ABIRIA DODOMA-KIGOMA KUPITIA TABORA YAPATA AJALI UVINZA

Treni ya abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora imepata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza mkoani Kigoma hii leo baada ya kichwa kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka.


JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 77.3 KUJENGA NEW BAGAMOYO ROAD DAR ES SALAAM

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia), na Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida, baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya Mradi wa upanuzi wa  Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Doto James, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili yaMradi wa upanuzi wa Barabara ya njia nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam. Anayeangalia makaratasi nyuma ni Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
***********************
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini leo Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Doto James amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia  kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

"Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini" Alisema  Doto James.

Ameishukuru Japan kwa msaada mwingine uliotolewa mwezi Septemba, 2017 wa kiasi cha fedha za Japan (Yen) milioni 69 sawa na shilingi bilioni 1.4 ambazo zimetumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hiyo itakayoanza kujengwa

James ameeleza kuwa  awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge pamoja na kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Mlalakuwa, Lugalo na Tegeta.

“Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza  Doto James.

Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kutolewa kwa msada huo ili kuwezesha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara kuanza kutayafanya matokeo ya kujenga barabara hiyo kuanza kuonekana dhahiri ikiwemo kupunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa ili kuokoa fedha nyingi zinazotokana na changamoto za msongamano huo.

"Ili kukamilisha usanifu wa kina wa mradi huu, nilisaini mkataba wa usanifu wa kina wa mradi wa upanuzi wa barabara ya new Bagamoyo  (Awamu ya Pili) miezi mitano iliyopita, hatimaye sasa ninasaini mkataba wa sehemu kuu ambayo ni ujenzi wenyewe" Alisema Balozi Yoshida.

Balozi huyo wa Japan hapa nchini, amesema mradi huo utasaidia kuboresha ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini na kwamba msaada huo ni mwendelezo wa kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania.

Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari  yanayokadiriwa 52,000 yanayopita kila siku katika barabara hiyo.


LUNDENGA AJITOA KUANDAA MISS TANZANIA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Ageny, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo ambapo alitangaza rasmi kampuni hiyo kujitoa katika uandaaji wa shindano Miss Tanzania  tangu Februari 2018. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi ambao ndio watakuwa waandaji wapya wa Miss Tanzania. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mwingereza.
Mashindano ya Miss Tanzania kuanzia sasa yatakuwa yakiandaliwa na Kampuni ya The Look Company Limited, inayoongozwa na Mwanadada Basila Mwanakuzi aliyepata kuwa Miss Tanzania 1998. 

 Kampuni ya Lino Intentional Agency Limited imekuwa waandaaji wa shindano la Miss Tanzania tangu mwaka 1994 na katika kipindi hicho inajivunia kutwaa taji la Miss World Africa 2005 kupitia Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari


RC MWANRI APOKEA VIFAA VYA UTUNZAJI MAZINGIRA

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya thamani ya milioni 4.4 ambavyo vitasaidia katika kampeni ya uhifadhi mazingira na upandaji miti . Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(mwenye koti  la bluu)  akipokea  vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 4.4 ambavyo vitasaidia katika kampeni ya uhifadhi mazingira na upandaji miti . Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd.Baadhi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 4.4 vilivyotolewa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Mkoa wa Tabora za kampeni yake ya kuhakikisha eneo hilo linakuwa la kijani kwa kupanda miti kwa wingi. Picha na Tiganya Vincent


WAZIRI MKUU AZINDUA BARABARA YA TANDAHIMBA MJINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Wilaya ya Tandahimba, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.


CCM MANISPAA YA IRINGA YATEKELEZA AHADI YA MBUNGE MSIGWA KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA.

Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi TV na king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mbunge wa viti maalumu ritta Kabati akiwa na diwani wa kata ya Mshindo Ngwada pamoja na matha walipokuwa wakikabidhi TV na king'amuzi cha Azam kwa viongozi wa soko kuu la manispaa ya Iringa
Wananchama wa chama cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara walipohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa TV na king'amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa soko kuu manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa kimetekeleza ahadi ilikuwa imeahidiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni za mwaka 2015 ya kuwatafutia TV wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Iringa chini ya mgombea wake wa ubunge mchungaji Petter Msigwa ambaye kwa sasa ndio mbunge wa jimbo la Iringa mjini 
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alipokuwa anakabidhi TV nchi 58 na king’amuzi kwa kiongozi wa masoko hapa manispaa.

Rubeya alisema kuwa wametoa TV hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo wanapata habari kwa wakati.

“Mimi nimekuja jana hapa mkaniambia kero hii nikaichuklua na chama change kimeifanyia kazi haraka iwezekanavyo na saizi tumekuja kukabidhi” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaamini kwenye utendaji na sio kulalamika na kuandamana hivyo kuna tumia vizuri falsafa ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu ndio maana tupo hapa kufanya kazi kwa vitendo kwa wananchi.

“Chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinafanya kazi kwa vitendo pale tunaposikia kero za wananchi tunatafuta njia za kutatua changamoto hizo ndio maana leo tunaleta hii TV na king’amuzi ili wafanyabiasha mpate habari mkiwa hapa kazini” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiasha ya kutekelezwa kwa ahadi ambazo zilizotelewa na mbunge wakati kampeni na imepita miaka mingi haijatekelezwa hivyo wakaamua kuichua na kuitatua ili kuwapa haki wananchi na wafanyabishara wa soko hilo.

“CCM tukitoa ahadi tunatekeleza kwa wakati lakini wenzetu wamekuwa wanapiga propaganda tu za maneno hivyo wananchi mnatakiwa kuchagua viongozi ambao wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa maendeleo ya wananchi wanaowangoza” alisema Rubeya

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu ritta Kabati alisema kuwa kitendo cha leo walichokifanya chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinaonesha kuwa chama hicho ni chama cha wananchi wote ndio maana leo wametoa TV na king’amuzi kwa ajili ya kupata habari kwa wananchi wanaopata huduma katika soko hilo.

“Kupata habari ni haki ya kila mwananchi wa mtanzania anapata habari kwa wakati hivyo kutoa TV hii kutasaidia kuongeza wigo kwa wananchi kupata habari kwa wakati” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi wa soko hili kuandaa mkutano wa kusikiza kero ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa haraka zaidi na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dr Johh Pombe Magufuli.

“Mwenyekiti naomba mniandalie mkutano nije kuwasikiliza kero zenu kwa kuwa ni haki yenu na msipofanya hivyo mtakuwa mnajinyima haki yenu ya msingi ya kutatuliwa kero zenu” alisema Kabati

Naye mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew aliwashukuru chama cha mapinduzi kwa msaada walioutoa kwa kuwa wamerahisisha wafanyabiashara kupata habari wakiwa kazini.

Mathew alikiomba chama hicho kuongezea nguvu kwenye masoko mwengine ya manipsaa ya Iringa kupata hata TV ndogo hata kama sio kuwa kama ambayo imetolewa leo katika soko kuu la manispaa ya Iringa

“Naomba nimbe kama hapo mbe mtapa nguvu nyingine basi tunaomba mtukumbuke tena maana kuna soko hilo hapo chini nalo linahitaji kuwa na Tv nao wewe kupata habari kama haki yao ya msingi kujia nini kinaendelea duniani” alisema Mathew

Aidha Mathew akawamba viongozi wa CCM kuwasidia kuiomba SUMATRA kutengeneza njia ya daladala ipite katika soko hilo ili kuongeza mzunguko wa kibiashara kama ilivyo mikoa mingi hapa nchini.