Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 31 July 2017

IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.

Hata hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aidha, katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.


Sunday 30 July 2017

WIZARA YA AFYA YATOLEA UFAFANUZI KUHUSU MAFUNZO YA UTARAJALI

KUMEKUWEPO na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internaship programme) bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.

Taarifa kwa umma, iliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kupitia kwa Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya, Nsachris Mwamwaja inasema kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.

"Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na Serikali ya Tanzania," ilisema taarifa hiyo ya Mwamwaja.

Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo  kwa kujigharimia  pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi  mapema kumalizia program yao ya udaktari.

Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka  kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.


CHUO CHA IFM CHATENGA WIKI NZIMA YA KUTOA MAELEZO NA KUFANYA UDAHILI KWA WANAOTAKA KUJIUNGA NA CHUO HICHO

 Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk. Kadida Mashaushiakizungumza na Blog ya Daily News-Habarileo juu ya Wiki moja kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, maelekezo na kufanya udahili wa kozi mbamlimbali zinazotolewa na chuo hicho.
 Watu mbalimbali waliofika chuoni hapo kwajili ya kupata amelezo juu ya namna ya kujiunga na chuo hicho wakisikilizwa na maofisa wa chuo.
CHUO Cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM) kimetenga mda wa wiki moja kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, maelekezo na kufanya udahili wa kozi mbamlimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii katika Chuo Hicho Dk. Kadida Mashaushi alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa zoezi hilo litaanza tarehe 29 mwezi huu na kumalizika tarehe 5 mwezi ujao (8) katika Chuo hicho kilichopo jijini hapa.

“Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam na wale wa mikoa ya jirani, fursa hii ambayo imetolewa na chuo cha usimamizi wa fedha nchini ni adimu kwa kutoa maelekezo kwa wazazi, wanafunzi watarajiwa, waombaji na wadau mbalimbali kuzielewa kwa usahihi kozi mbalimbali ambazo zinatolewa na chuo,” alisema.

Dk Mashaushi alisema kuwa zoezi hilo ni mwitikio wa chuo hicho baada ya serikali kutoa muongozo kwa namna ambavyo wanafunzi wapya wa elimu ya juu watadahiliwa mwaka huu wa masomo (2017/18) na maelekezo yaliotolewa kuhusu vigezo vya kuingia elimu ya juu.

Alisema kutokana na maelekezo hayo, kumekuwepo na mkanganyiko miongoni mwa wa wadau mbalimbali kwenye sekta ya elimu ya juu hususani kwa  upande wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini, hivyo kupelekea chuo hicho kuanzisha hilo zoezi kwa ajili ya kusaidia katika kutatua changamoto hizo.

“Zoezi hili litasaidia wale ambao wanatamani kuingia elimu ya juu, kuwawekea wepesi wa kutosha ili kufanikisha malengo yao,” alisema na kuongeza kuwa katika zoezi hilo, chuo hicho kinatoa maelekezo ya kina na kujibu maswali yale ambayo jamii kwa ujumla imekanganyikiwa baada ya mabadiliko ya udahili yalitolewa mwaka huu na serikali.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni uelewa usietosheleza kwa muomba na kupelekea baadhi ya wao kuomba kozi ambayo hana sifa nayo na ombi lake kwenda kwa katika kozi mabayo sio sahihi na baadaye kutochaguliwa.

Mashaushi alisema pia wakati huohuo vyuo navyo huenda viakapata wanafunzi wachache katika zile nafasi ambazo zipo. Zoezi la udahili kwa wanafunzi wa elimu ya juu linatrajiwa kusitishwa tarehe 30 mwezi ujao (8) mwaka huu.

“Changamoto kubwa kwa vyuo kutokua ufafanuzi ili kila mwenye alama zinazotosheleza akapata kuomba kwa usahihi kwa mujibu wa vigezo viliwekwa na serikali, vyuo na taratibu ambayo serikali imeweka mwak huu,” aliongeza.

Kwa hatua nyingine, Dk.Mashaushi alisema kuwa kwa wale wa mikoa ya mbali, watapata taarifa mbalimbali kuhusu udahili wa mwaka huu kupitia tovuti ya chuo ambapo pia watapata fomu ya maombi ya kujiunga na chuo.

“Kwa wale wa Mwanza watapata maelekezo, ufafanuzi katika kituo chetu cha mafunzo kilicho huko  ambapo watakutana na maaofisa wetu. Na wale wengine ambao pia hawataweza kufika wanaweza kutumia tovuti yetu na njia ya posta katika kuwasilisha fomu zao,” alisema.

IFM imejikita katika kutoa kozi za uhasibu ngazi ya shahada, stashahada na cheti. Pia chuo hicho kimejikita katika fani ya bima na hifadhi ya jamii ambapo halikadhalika inatolewa kozi ya shahada kozi ya bima na hifadhi ya jamii na kozi maeneo ya kodi kwenye ngazi ya shahada, stashahada na cheti.

“Chuo pia kiko vizuri na miongoni mwa vyuo vichache  ambavyo vinatoa mafunzo katika maswala ya bank na fedha katika ngazi ya shahada  (Bachelor of banking and finance) na stashahada (ordinary diploma in banking and finance) na cheti kwa wanafunzi watarajiwa elimu ya juu.


Friday 28 July 2017

KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU



 MBUNGE wa Singida Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amewafuta machozi akinamama wa jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na Tundu Lissu wilayani Ikungi, Singida baada ya kuwanunulia vitanda 52 ili kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto. Anaandika Mroki Mroki/TSN Digital DSM.

Kwa muda mrefu, akinamama hao walikuwa na kilio cha kukosekana kwa huduma hizo, hasa vitanda vya kujifungulia, hivyo kumlilia Kingu aliyeamua kubeba jukumu na mbunge mwenzake.


Akizungumza na TSN Digital kwa njia simu, Kingu alisema ameamua kutoa msaada huo kutokana na maombi aliyoyapata kutoka kwa akinamama wa eneo la Ikungi na pia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida juu ya kuwasaidia katika sekta ya afya kwa kuwapatia vitanda vya kujifungulia.


“Ni kweli ninatarajia siku yoyote nitakwenda kukabidhi vitanda 86 katika Wilaya ya Ikungi, ambako kuna majimbo ya Singida Magharibi nilipo mimi na jimbo jirani la Singida Mashariki kwa Tundu Lissu, kufuatia maombi ya wananchi hasa akina mama ambao huteseka sana kwa kwenda umbali mrefu kutafuta huduma za afya wakati wa kujifungua,” alisema Kingu.

Kingu alisema kati ya vitanda hivyo 86 vyenye thamani ya Sh. Milioni 48.9, vitanda 52 atavigawa katika jimbo la Singida Mashariki na vingine 34 atavigawa katika jimbo lake la Singida Magharibi.

Amesema kati ya vitanda hivyo 52 atakavyovigawa Singida Mashariki, vitanda 26 ni maalumu kwa ajili ya akinamama kujifungulia na vitanda vingine 26 kwa ajili ya wodi za kawaida.



Aidha, amesema katika jimbo lake atakabidhi vitanda 34 vya kujifungulia ambavyo kati ya hivyo, vitanda vinne ni vya kisasa vinavyotumia umeme.

Wilaya ya Ikungi ina jumla ya Kata 28 ambapo kati ya hizo, kata 13 zipo katika jimbo la Singida Mashariki ambapo katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ilikuwa na takribani wakazi 272,959.


RAIS MAGUFULI AAGIZA NAIBU KAMISHNA UHAMIAJI GRACE HOKORORO ASIMAMISHWE KAZI

RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Grace Hokororo (pichani)asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.
                  
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. 

“Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”

Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi  kuivumilia.”

Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo  Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.

"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo  Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."

Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. " Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchungilzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.


TBC KUZINDUA CHANNEL YA MASUALA YA UTALII MWEZI DESEMBA MWAKA HUU



MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC), Dk. Ayoub Rioba amesema chaneli ya utalii itakayokuwa ikirushwa na televisheni hiyo itazinduliwa Desemba 30, mwaka huu.

Amesema chaneli hiyo itasaidia kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuwa kila Mtanzania pamoja na wageni wengine wataweza kufahamu sekta ya utalii ya Tanzania kupitia chaneli hiyo.

"Tunatarajia kumaliza andiko Agosti 10 ambalo litaenda sambasamba na uombaji wa leseni ambao tunatarajia itakuwa Septemba 10," amesema Dk Rioba wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa wahariri na wanahabari waandamizi wa masuala ya utalii unaofanyika mkoabi Tanga.
 
Mratibu wa Mradi wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada kuhusu hifadhi za mazingira asilia na mikakati ya utalii kwa wanahabari.
 Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah akifuatilia mkutano huo unaoendelea na mkoani Tanga
 Waandishi mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini unaofanyika jijini Tanga.