Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 29 May 2018

WIZARA YA ARDHI YAOMBA BILIONI 73 KWA MWAKA 2018/2019.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maedeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akiwasilisha Bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameliomba Bunge kujadili na kuopitisha kiasi cha shilingi 73,071,273,632 iloi wizara iweze kutumiza majukumu yake.
 Waziri, Lukuvi ameliambia Bunge kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018/19 wizara inataraji kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 120 kutokana na kodi, tozo, na ada mbalimbali za zinazotokana na shughuli za sekta ya ardhi kwa kutekeleza mikakati ambayo wamejiwekea. 
 Msemaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii, Halima Bulembo akisoma taarifa ya Kamati Bungeni leo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akijadili jambo na Naibu Waziri wake, Dk. Angelina Mabula Bungeni leo. 
 Wabunge wakiwa Bungeni jijini Dodoma leo 
 Wageni wakiwa Bungeni jijini Dodoma
 Wabunge Munira Mustapha akijadili jambo na Hussein Bashe Bungeni jijini Dodoma.
 Wageni wakiwa Bungeni wakifuatulia kikao cha Bunge leo. BOFA HAPA KUONA ZAIDI.


Monday, 28 May 2018

SIMANZI YA TAWALA BUNGENI, KIFO CHA MBUNGE KASUKU BILAGO

 VILIO, Majonzi na Simanzi vimetawala katika viunga vya Bunge jijini Dodoma hii leo kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mwalimu Kasuku Bilago. Anaandika Mroki Mroki – Daily News Digital, Dodoma

Mwalimu Bilago alifikwa na umauti wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumamosi Mei 26, mwaka huu  jijini Dar es Salaam.
 Muda mfupi baada ya Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kufungua kikao cha Bunge kwa kusoma dua, alitoa Bungeni hapo Taarifa ya Spika kuhusiana na msiba huo mzito uliolifika Bunge, naabade kutangaza kuahirisha Bunge hadi Mei 29 saa tatu asubuhi, ili kupisha Maombolezo huku mipango ya kuuleta mwili katika viwanja vya Bunge kwa heshima za mwisho ikifanyika.
 Daily News Digital ilishuhudia wabunge wakitoka Bungeni huku wakiwa na nyuso za huzuni na wengi wao wakibubujikwa na machozi na vilio vya kwikwi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amemtaja marehemu kuwa ni miongoni mwa wabunge Bora ambao walikuwa wakijenga hoja  na kutoa michango yenye maslahi mapana kwa Jimbo lake na nchi kwa ujumla.

Nae Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule alizungumzia msiba huo na kusema ni pengo kubwa Mwalimu Bilago ameliacha si kwa Kambi ya Upinzani bali kwa Bunge zima kutokana na mchango wake aliokuwa akiutoa.
 “Mwalimu Bilago alikuwa Mwalimu kweli kweli, hakuna siku ambayo alisimama kuchangia asipate sapoti ya Bunge zima nah ii ni kutokana na ucheshi wake lakini pia hoja zake za msingi alizokuwa akizitoa Bungeni,”alisema Haule.

Mwili wa Marehemu Bilago unataraji kuletwa Bungeni Mei 29 kwa heshima za mwisho na baade kusafirishwa hadi Kijiji cha Kasuga Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma ambako utahifadhiwa Mei 30 mwaka huu. 
 Wabunge mbalimbali wakifarijiana kufuatia Msiba huo mzito wa Mwezao.
 Mawaziri wakiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha Mbunge Kasuku Bilago wa Jimbo la Buyungu, Wilayani Kakonko mkoa wa Kigoma.
Wabunge wakisaini kitabu cha maombolezo


Friday, 25 May 2018

MAKONGORO APEWA KAZI CCM PIA YUPO PINDA


 Makongoro Nyerere
Mizengo Pinda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. John Pombe Magufuli leo Mei 25, 2018 amewateua Ndg. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Waziri Mkuu Mstaafu) na Ndg. Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Ndg. Magufuli amefanya uteuzi huo kwa kutumia mamlaka aliyonayo kwa  mujibu wa katiba ya CCM toleo la mwaka 2017.

Majina ya wateule hao yatawasilishwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika Mei 28, 2018 Jijini Dar es Salaam.


Wednesday, 23 May 2018

WANAWAKE WAJAWAZITO WANATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA.

WANAWAKE wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.

“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.

“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .

Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”


KUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA LEO, MAMBO YA NJE YASOMA BAJETI YAKE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk, Augustine Mahiga akiwasilisha Bungeni Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 leo ambapo ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Shilingi 177,006,232,000 ambapo kati ya hizo Bilioni 154.810 ni kwaajili ya matumizi mengineyo, Bilioni 11,795 kwaajili ya Mishahara na Bilioni 10.4 kwaajili ya Maendeleo. 
Balozi Mahiga ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Shilingi 177,006,232,000 ambapo kati ya hizo Bilioni 154.810 ni kwaajili ya matumizi mengineyo, Bilioni 11,795 kwaajili ya Mishahara na Bilioni 10.4 kwaajili ya Maendeleo. 
 Mmoja wa wanafunzo wa Chuo cha Diplomasia akifuatilia hotuba hiyo ya Bajeti.
 Mbunge wa Handeni Vijijini, Mboni Mhita akizungumza Bungeni jijini Dodoma jana.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, akizungumza Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akijibu maswali yaliyoelekezwa katika Wizara yake Bungeni jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk.Augustine Mahiga akijadiliana jambo na Naibu Waziri wake, Dk.Suzan Kolimba Bungeni leo kabla ya kuanza kusoma Bajeti yao.
 Baadhi ya wageni kutoka Chuo cha Diplomasia na maeneo mengine wakifuatilia shughuli za Bunge jijini Dodoma leo. 
 Wabunge wakiwasindikiza Bungeni Wabunge, Steven Masele na Mboni Mhita ambao wamechaguliwa kuwa Viongozi katika Mabunge ya Afrika na Afrika Mashariki.

 Baadhi ya wageni kutoka Chuo cha Diplomasia na maeneo mengine wakifuatilia shughuli za Bunge jijini Dodoma leo. 
Baadhi ya wageni kutoka Chuo cha Diplomasia na maeneo mengine wakifuatilia shughuli za Bunge jijini Dodoma leo. 


Tuesday, 22 May 2018

TANZANIA YAPIGIWA MFANO MATUMIZI BORA YA FEDHA ZA MAENDELEO ZA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban(kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa Magavana kutoka nchi za Afrika  kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini wakati wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Busan- Korea Kusini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (katikati) akiwa na baadhi ya Magavana wa nchi za Afrika, kushoto kwake ni  Gavana wa Kenya Mhe. Henry Kiplagat Rotich na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB,  Dkt. Nyamajeje Weggoro baada ya kumaliza majadiliano yanayaozihusu nchi wanazoziwakilisha, Mjini Busan- Korea Kusini. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango-Korea)
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika zenye matumizi bora ya fedha zinazofadhiliwa na Benki hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara na nishati.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayesimamia nchi 7 za Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro wakati  wa kikao  cha Magavana wa nchi za Afrika kwenye Mkutano wa  mwaka wa Benki ya AfDB unaoendelea Mjini Busan, Jamhuri ya Korea ya Kusini.
Dkt. Nyamajeje alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa nchi  za Afrika zinatokana na ukosefu wa  wataalamu wa fani mbalimbali, jambo linalosababisha miradi mingi  kutomalizika kwa wakati  hata hivyo Benki ya AfDB inaendelea kuangalia ni jinsi gani inaweza kusaidia kutatua matatizo hayo na kuleta maendeleo chanya kwa nchi za Afrika.
Akizungumza katika Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali ya Tanzania imesawasilisha barua kwa uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ili iweze kusaidia katika ujenzi wa  Uwanja wa ndege ya Msalato Jijini Dodoma na Uwanja wa ndege wa Zanzibar,  aidha miradi hiyo ikiridhiwa na kutekelezwa  itakua kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa Viwanda nchini Tanzania.
Tanzania ni wadau wakubwa  katika Benki ya AfDB hivyo inanufaika na mikopo nafuu inayotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara  za kiwango cha Lami hususani mkoa wa Tabora na pia miradi ya  Nishati  ya umeme na maji maeneo mbalimbali nchini.


WABUNGE WA CUF WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI

WABUNGE watatu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) mikoa ya Lindi na Mtwara wamepongeza kasi ya utendaji kazi ya Rais John Pombe Magufuli katika kutatua kero za wananchi wa mikoa hiyo.

Wabunge hao Bw. Selemani Said Bungara (Kilwa Kusini), Bw. Zuberi Mohammed Kuchauka (Liwale) na Bw. Maftaha Abdallah Nachuma (Mtwara Mjini) walitoa pongezi hizo jana, (Jumatatu, Mei 21, 2018) wakati walipopewa nafasi ya kusalimia wananchi kwenye mikutano ya hadhara ambayo Waziri Mkuu alihutubia.

Akiwa wilayani Lindi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kituo cha kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa katika kijiji cha Mahumbika, aliwapa fursa wabunge wote alioambatana nao katika ziara hiyo maalum kwa ajili ya uzinduzi wa miundombinu ya nishati kwa mikoa ya Kusini.

Mapema, akizungumza na wananchi na viongozi wa taasisi mbalimbali mkoani humo waliohudhuria uzinduzi huo, Mbunge wa Kilwa Kusini, Bw. Bungara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Lindi alisema analishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuisimamia vizuri Serikali ya CCM.

“Faida ya demokrasia ya vyama vingi ni kwamba CCM bila CUF, CCM hakuna na CUF bila CCM, CUF hakuna; kama ambavyo hakuna Simba bila Yanga wala hakuna Yanga bila Simba. Tuwe kitu kimoja tu, Kusini kwanza, vyama baadaye!” alisisitiza.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa juhudi zake za kuwaunganisha wabunge wa mikoa ya Kusini bila kuwabagua au kujali itikadi zao.

Naye Mbunge wa Liwale, Bw. Kuchauka alisema: “Niwapongeze wewe Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa yale ambayo mnayasimamia na mnayaamini kwamba yataleta ukombozi kwa wananchi wa Tanzania. Lazima nikiri kwamba wakati mnazindua sera ya uchumi wa viwanda, nilikuwa siamini katika hiyo sera yenu kwa sababu niliona ni moja ya mbinu zenu za kututenga sisi watu wa mikoa ya Kusini.”

“Niliona hivyo kwa sababu nilijiuliza unawezaje kuwa na uchumi wa viwanda wakati huna nishati ya uhakika ya umeme? Baada ya tukio la leo, sasa nimeona mwanga kwamba mikoa ya Kusini nayo inaweza kushiriki kwenye uchumi wa viwanda,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema hivi sasa hakuna asiyeona mambo yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwani dunia yote imekuwa kama kijiji na lolote linalofanywa na Mhe. Rais au Waziri Mkuu hakuna asiyelijua. “Lolote analolifanya Mheshimiwa Rais au wewe Waziri Mkuu Watanzania wote watalijua, hakuna asiyeliona. Hivi sasa hakuna haja ya kubishana nani kafanya nini, jambo kubwa ni kuungana na tuangalie Tanzania yetu. Vyama vyote baadaye, Kusini kwanza,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Bw. Maftaha alisema mwaka 2006 baada ya kuhitimu kidato cha sita, alipangiwa afanye mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya sekondari Mingoyo, eneo la Mnazi Mmoja lakini alitafuta nyumba ya kuishi yenye umeme hakupata.

“Wakati ule nyumba zenye umeme zilikuwa hazizidi hata 10, na kulikuwa na simba na wadudu wa kila aina. Leo nafarijika kuona kwa kasi ya ajabu, ninyi viongozi tuliowapa dhamana, mnatumia rasilmali za nchi hii, mnasambaza umeme kwa wananchi wa mikoa ya Kusini, na pale Mnazi Mmoja leo hii, umeme siyo tatizo tena.”

Wabunge wengine waliofuatana na Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bibi Hawa Ghasia; Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Bi. Hamida Mohammed Abdallah (Viti Maalum). Mbunge wa Nachingwea, Bw. Hassan Elias Masala, Mbunge wa Nanyamba, Bw. Abdallah Dadi Chikota.

Jana jioni, Waziri Mkuu alizuru pia mkoa wa Mtwara na kukagua ujenzi wa bandari, ukarabati wa mabomba ya kupokelea mafuta, matenki ya kuhifadhi mafuta, kuzindua upanuzi wa kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa bandari.


TAARIRA RASMI AJALI YA MAOFISA WA TICFUATILIA MAJUMUISHO YA BAJETI 2018/2019: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


Monday, 21 May 2018

LIVE BUNGENI: WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. DKT. HAMISI KIGWANGALLA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YAKE 2018/2019


Friday, 18 May 2018

WAZIRI MPINA ABAINI UPOTEVU WA BILIONI 263 UTOROSHAJI MIFUGO NJE YA NCHI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga joelson kulia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo wakiwa kwenye  bango la uzinduzi wa Operesheni Zagamba 2018. Operesheni hiyo  ni maalum kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nchini, ambapo kitaifa ilizinduliwa Namanga kwenye Wilaya ya Longido. Picha na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga joelson kulia akitoa maelezo ya maana ya Operesheni Nzagamba2018 kwenye  bango la uzinduzi wa Operesheni Zagamba 2018. Operesheni hiyo  ni maalum kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nchini, ambapo kitaifa ilizinduliwa Namanga kwenye Wilaya ya Longido. Picha na John Mapepele

Na John Mapepele, Arusha
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Serikali kila mwaka inapoteza jumla ya sh bilioni 263 kila mwaka kufuatia kushamiri kwa utoroshaji wa mifugo nje ya nchi na uingizaji wa mazao ya mifugo usiozingatia sheria na taratibu za nchi hali inayochangia ushindani usio wa haki kwa wazalishaji wa ndani ya nchi.

Akizungumza jana kwenye mnada wa mifugo wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa operesheni maalum ya kitaifa ya kudhibiti upotevu wa mapato na usimamizi wa biashara ya mifugo na mazao yake iliyopewa jina la ‘Operesheni Nzagamba 2018’ Waziri Mpina alisema operesheni hiyo itamfikia kila mtu anayejishughulisha na tasnia nzima ya mifugo.

Alisema operesheni hiyo itafika kwenye minada ya mifugo, bandarini, viwanja vya ndege, mipakani, kwenye masoko na maduka,supermarket, na machinjioni ili kujiridhisha na uhalali wa biashara hiyo.

Pia Waziri Mpina alisema operesheni hiyo imefanikiwa kubaini kuwepo kwa ubabaishaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kufanya udanganyifu katika biashara ya dawa za mifugo,upotevu mkubwa wa mapato na uingizaji holela wa mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi ikiwemo nyama na maziwa kupitia njia za panya.

Akitolea mfano eneo la Namanga zaidi ya mbuzi 22,000 zilikamatwa zikitoroshwa kwenda nchini Kenya huku makusanyo yakiongezeka na kufikia sh milioni 200 kwa muda wa mwezi mmoja tangu kuanza operesheni hiyo ambapo kwa upande wa Mwanza makusanyo yameongezeka kutoka sh milioni 17 kwa mwezi na kufikia Sh. Milioni 532.

Waziri Mpina alisema tathimini ya awali iliyofanywa na wizara yake imebaini kuwa wastani wa ng’ombe milioni 1.6 hutoroshwa kila mwaka kwenda kuuzwa nchi za jirani ambapo Serikali hupoteza sh bilioni 56.4 kwa mwaka huku upande wa ngozi Serikali ikipoteza sh. Bilioni 87.6 kwa mwaka ambapo kwa upande wa nyama na maziwa Serikali hupoteza zaidi ya sh bilioni 120 kila mwaka

Aidha alionya kuwa mifugo itakayokamatwa ikitoroshwa kwenda nchi jirani kinyume cha sheria Serikali itafanya maamuzi magumu ya kutoza faini kubwa ili kuhakikisha watu wote wanafuata sheria ili mifugo hiyo iweze kunufaisha watanzania wote kupitia mfumo wa ushuru na kodi.

Kuhusu tozo ya mifugo inayokwenda nchi za nje, Waziri Mpina alisema msimamo wa Serikali unabaki pale pale ambapo kila ng’ombe atatakiwa kulipiwa sh 20,000 na Mbuzi sh. 5,000 huku akiruhusu vibali vya biashara za mifugo vinavyotolewa na halmashauri viendelee kutumika hadi pale Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakapoamua vinginevyo.

Pia Waziri Mpina alipongeza uamuzi wa kujengwa kwa mnada wa kisasa wa mifugo katika eneo hilo la uliofadhiliwa na Mradi wa MIVARF na kugharimu sh. Milioni 782 na kusisitiza kuwa mnada huo utakuwa mkombozi mkubwa kwa wafugaji kupata soko la uhakika la mifugo yao.

Kaimu Katibu Mkuu Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Lovince Assimwe alisema operesheni hiyo imewezesha kubaini mianya ya upotevu ya mapato yatokanayo na sekta ya mifugo na kusisitiza kuwa itakuwa endelevu hadi pale wadau wa sekta hiyo watakapofuata sheria za nchi.

Dk Assimwe Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kusimamia sekta ya mifugo ili iweze kutoa mchango unaostahili kwa maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo alimshukuru Waziri Mpina kwa juhudi kubwa anazofanya za kudhibiti utoroshaji wa mifugo na kumhakikishia kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo itaendelea kushirikiana na wizara kuhakikisha mifugo haiendi nje ya nchi kwa njia za panya.

Alisema maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Mpina atatumia uwezo wake wote kuhakikisha yanasimamiwa kikamilifu ili kuweza kupata matokeo mazuri yanatoyarajiwa.