Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 19 September 2017

TIC YASEMA HALI YA UWEKEZAJI NCHINI NI SHWARI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe amesema uwekezaji unazidi kushamiri nchini Tanzania na TIC inahakikisha wawekezaji wanaendesha shughuli zao vizuri na kwa faida.

Mwambe amesema hivi TIC imeondoa dosari zote zilizokuwa zinawakwaza wawekezaji na kwamba mwekezaji mpya anakamilisha mchakato wote wa kupata vibali na nyaraka nyingine za kumwezesha kuwekeza ndani siku tatu na kila huduma inapatikana ndani ya Ofisi ya TIC (One Stop Center).

Mwambe ameongeza kuwa kauli za kuwa hali ya uwekezaji Tanzania ni mbaya ni za uzushi na zenye nia ya kuchafua sifa ya Tanzania ambayo kwa ni moja ya nchi 10 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi duniani kwa wastani wa asilimia 7.2, na ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Afrika Mashariki.

Amesema ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepata uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 1.35 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 3 za Kitanzania, ikifuatiwa na Uganda iliyopata uwekezaji wa Dola za Marekani Milioni 537 ambao ni chini ya nusu ya Tanzania.

Mwambe ameongeza kuwa pamoja kuwepo kwa hali nzuri ya uwekezaji TIC inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwavutia wawekezaji na kuwaeleza fursa mbalimbali muhimu ikiwemo uwepo wa soko la uhakika la ndani ya nchi na nje ya nchi, vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa na TIC pamoja na ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza.


WAZIRI MKUU AUTAKA MKOA WA PWANI KUBORESHA MAENEO YA UWEKEZAJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea kiwanda cha Sabuni cha KEDS wilayani  Kibaha September 19, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo  na Kushoto  kwake ni Mkurugenzi Mtenaji wa kiwanda hicho, Jack Fen. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Pwani waboreshe miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 19, 2017) wakati akizungumza na kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Keds kilichopo Kibaha na kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford kilichopo Chalinze.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mkoani Pwani na amewaagiza viongozi wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanakuwa na miundombinu muhimu kama maji, umeme na barabara.

“Nimefarijika kuona miradi hii mikubwa ya ujenzi wa viwanda ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika, nawashukuru kwa kuunga mkono mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.”

Amesema mbali na viwanda hivyo kutoa ajira nyingi kwa Watanzania, pia vitakapoanza uzalishaji vitawawezesha wananchi kupata bidhaa mbalimbali kama vigae kwa bei nafuu kwa kuwa vitakuwa vinazalishwa nchini.

Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaofanyakazi kwenye viwanda hivyo wawe mabalozi wazuri wa Taifa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwathibitishia wawekezaji kwamba wao wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na hakuna haja ya kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda hivyo Bw. Jack Feng amesema ujenzi wa huo umekamilika kwa asilimia 90 na sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na ufungaji wa mitambo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji Oktoba mwaka huu.

Amesema vigae watavyovizalisha wanatarajia kuviuza kwa gharama nafuu kwa sababu asilimia 95 ya malighafi inapatikana ndani ya nchi. Pia ameahidi kutoa ajira nyingi kwa wananchi waishio kwenye maeneo yanayozunguka viwanda hivyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo amemuomba Waziri Mkuu awasaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.

Mhandisi Ndikilo amesema mahitaji waliyonayo ya nishati ya umeme ni megawati 92, ambapo kwa sasa wanasambaziwa megawati 40, hivyo ameomba suala hilo lipatiwe ufumbuzi wa haraka ili lisije kuathiri uzalishaji.


Friday, 15 September 2017

JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI


Na. Atley Kuni- TAMISEMI
Serikali imepanga kukarabati vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Canada ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88 sambamba na Bil.12 fedha za kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo (Mb) amesema lengo la serikali nikuhakikisha ifikapo Desemba 30, mwaka huu shughuli hiyo iwe imekamilika ipasavyo kwa kusimamiwa karibu na Wakuu wa mikoa wakisaidiana na Wakuu wa Wilaya.

Jafo amesema kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Serikali imepokea Dolla za kimarekani  Mil. 66 kutoka Benki ya Dunia ambapo vituo 103 vitakarabatiwa aidha pia Serikali  kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepata Msaada kutoka Ubalozi wa Canada wa dolla za kimarekani Mil 22, ambapo vituo 44 vya afya vitakarabatiwa kwa fedha hizo.

Naibu waziri huyo alisema,  fedha zingine zitakazo tumika katika zoezi hilo ni zile zilizo vuka katika mwaka wa fedha uliopita.

“Vituo 25 vitafanyiwa ukarabati kupitia fedha za Benki ya Dunia na mfuko wa afya wa pamoja zilizovuka mwaka wa 2016/2017, ambapo Bil.12 za kitanzania zitatumika,” alisema Jafo na kuongeza  kwamba kila  “kituo kitapatiwa shilingi Mil. 500 za kitanzania na baada ya ukarabati serikali itakuwa na jukumu lakupeka vifaa katika maeneo hayo”.

Waziri Jafo amesema, Maeneo ya kipaumbele wakati wa ukarabati huo ni pamoja na  Upasuaji (Theater), Wodi za mama na Mtoto (Martenity), Maabara(Laboratory), pamja na Nyumba za watumishi sambamba na maeneo mengine ya kipaumbele kutokana na fedha zilizopo.

Katika hatua nyingine Jafo amewagiza Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha Taarifa ya kila mwezi ofisini kwake juu ya maendeleo ya ukarabati, huku akiwataka Wakurugenzi na watendaji wengine kusimamia kwa ufasaha zoezi hilo.

Naibu Waziri hakusita kuonya juu wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo na maelekezo ya serikali yaliyotolewa 

“Nawaomba Wabunge na Madiwani kushirikiana bega kwa bega na watendaji katika kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi, alisema Jafo na kuongeza kwamba,  “ofisi yangu haita mvumilia Kiongozi au Mtendaji yeyote atakaye onekana kutumia fedha hizo vibaya au kushindwa kutimiza wajibu wake na kisha kukwamisha shughuli hii muhimu yenye nia njema kwa maisha ya watanzania.

Akihitimisha maagizo hayo  Naibu waziri Suleima Jafo, amezishukuru  Wizara zote za kisekta katika kusukuma gurudumu la maendeleo  na kwenda sambamba na kasi ya Rais  Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU,  ikiwapo, Wizara ya Afya, Fedha na Mipango pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambao walikuwa bega kwa bega katika mchakato wote wa kupatikana kwa fedha.


Thursday, 14 September 2017

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

 Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele (kulia) akiwa na Mgeni wake ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBA ,Peter Makau alipotembelea Bungin jini Dodoma September 13,2017.
 Mbunge wa Newala Mjini, Capt Mstaafu. George Mkuchika (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete Bungeni Mjini Dodoma.
 Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (kushoto) akizungumza na wabunge wenzake Bungeni Mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akizungumza na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Wabunge wanawake wakitoka Bungeni Mjini Dodoma walipohudhuria Kikao cha Bunge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama akifurahia jambo na Mbunge wa Kinondoni, Maulid  Mtulia
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) akizungumza na Mbunge wa jimbo la Mpendae,Salim Hassan Turky, Bungeni Mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiongozwa kutoka nje ya Bunge baada ya kuahirisha kikao cha Bunge mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Bungeni.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma.


Tuesday, 12 September 2017

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja akizungumza jambo na Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.

 Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya akifurahia jambo na Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Mbunge mteule wa Viti Maalum, CUF, Rehema Migilla akila kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, Bungeni Mjini Dodoma jana.Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Bungeni wakati akitoa maelekezo kwa kamati mbili za Bunge za Haki, Maadili na  madaraka ya Bunge inayoongozwa na George Mkuchika pamoja na ile ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Adadi Rajab kuwaita haraka na kuwahoji Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto na Mbunge wa Kinondoni, Saeed Kubenea kwa makosa tofauti. (Picha na Mroki Mroki).

 Wanafamilia na wanachama wa Chama cha CUF, waliomsindikiza Mbunga mpya wa Viti Maalum wa Chama hicho, Rehema Migilla wakimpongeza baada  ya Mbunge hiyo kula kiapo cha Umanifu Bungeni mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya. (Picha zote na  Mroki Mroki).

 Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya akifurahia jambo na Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju akiwasilisha Bungeni mabadiliko ya miswada mbalimbali ya sheria.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jamhuri wakiwa Bungeni kwa ziara ya kimasomo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Risala Kabongo, Bungeni Mjini Dodoma.
  Wabunge wakiwa Bungeni mjini Dodoma katika kikao cha Bunge.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni wakiwasili Bungeni mjoni Dodoma.
Wabunge wakiwa Bungeni mjini Dodoma.
 Wabunge wa Grace Kiwelu (kushoto) wa Viti Maalum na Ester Matiko wa Tarime Mjini wakiwa Bungeni.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa Bungeni mjini Dodoma.
 Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa akizungumza na Mbunge wa Mikumi, Jpseph Haule katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

 Wabunge wakiwa Bungeni mjini Dodoma katika kikao cha Bunge.


WABUNGE UPINZANI WAGOMEA TENA UAPISHO WA MBUNGE MPYA WA CUFWABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, leo kwa mara nyingine wamesusuia kushiriki uapisho wa mbunge mpya wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi CUF, Rehema Juma Migilla aliyeapishwa Bungeni mjini Dodoma leo. Anaandika Mroki Mroki, Dodoma.

Wabunge hao walikusanyika nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma asubuhi kabla ya Bunge kuanza na muda mfupi baada ya Mbunge huyo Mpya kula kiapo cha Uaminifu Mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai waliingia Bungeni kuendelea na Shughuli za Bunge.

Mgomo wqa Wabunge hao ni muendelezo wa  wabunge hao wa kuto kuwapa ushirikiano wabunge wote wapya wa CUF na wale wanaounga mkono upande wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibeahim Lipumba.