Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 15 March 2017

HABARI YA HIVI PUNDE: RAIS MAGUFULI AMTUMBUA KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU (BUNGE) ULEDI MUSSA



Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) , Uledi Abbas Mussa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kutenguliwa kwa uteuzi na kusimamishwa kazi kwa, Uledi Abbas Mussa kunaanzia leo Machi, 15 2017.

Hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi zaidi dhidi ya  Uledi Abbas Mussa kufuatia kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji.

Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Desemba 30,2015 ambapo katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)  Uledi aliteuliwa pamoja na Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira) yeye Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu – Sera).

Uledi amehudumu katika Ofisi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja, miezi miwili na siku 15. Kabla ya utezi wa Desemba 30,2015 Uledi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment