Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 30 September 2017

TSN,TBC ZA TWAA TUZO ZA DSE 2017 PIA ZIPO NMB, TBL NA STANDARD CHARTERED BANK

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Magazeti), Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa. (Picha na Mroki Mroki).
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Digital), Kaimu Mkurugenzi wa habari na Matukio wa TBC, Prudence Costantine (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania,(TBL), Bruno Zambrano (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB anaeshughulika na Mikakati na mahusiano ya wawekezaji, Anna Mwasha (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi wa pili katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.


MWENYEKITI WA CCM TAIFA, RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Rodrick Mpogolo kabla ya kufungua mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)   jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es Salaam.


Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam.


Thursday 28 September 2017

WAZIRI DKT. TZEBA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MBOLEA DAR ES SALAAM



Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba akiongea na wadau wa Mbolea wa Tanzania alipofungua mkutano wao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu (kulia) akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba zawadi ya kitabu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau mbolea walipkutana jijini Dar es Salaam leo Septemba 28 2017. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Mbolea Tanzania, Salum Mkumba na Mkurugenzi Mkazi wa Taasis ya Biashara za Mbolea Afrika (AFAP), Dkt. Mbette Mshindo. 
 
Mkurugenzi Mkazi wa Taasis ya Biashara za Mbolea Afrika (AFAP), Dkt. Mbette Mshindo akiongea na wadau wa mbolea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau mbolea walipokutana jijini Dar es Salaam leo Septemba 28 2017. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Mbolea Tanzania, Salum Mkumba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba na Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Eng. Mathew Mtigumwe akitambulishwa kwa wadau. 
 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam.
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam.

Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam.BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. KIGWANGALLA AKERWA NA UCHAFU HOSPITALI YA MKOA WA MARA


Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana.

Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akihoji uchafu uliokuwa ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana

Baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mkoa wa Mara, hali hiyo ni kinyume na utaratibu wa vyumba vya upasuaji

Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo chumba hicho cha upasuaji huku akipata maelezo.
Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara.
******************
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji vya hospitali ya rufaa ya Musoma na zahanati ya Murangi na vyumba hivyo kubadilishwa stoo na eneo la taka. 
 
Naibu Waziri ambaye Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne alifanya ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini uchafu uliopo katika chumba cha upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa mashuka na mipira yake kuwekwa chini na huku kukiwa na vifaa vya kuwekea mashuka hayo. 
 
"Hivi ndivyo mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani ya nyie kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu jamani, sisi sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa Mkoa au mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo hopspitali ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa?"Alihoji Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa. 
 
Aidha aliagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda kuajiri Mganga mfawidhi wa hospitali (Medical officer Incharge) mpya atakayesimamia hospitali hiyo. 
 
Sanjali ya hayo alishangazwa pia kuona chumba hicho mabomba na masinki yakiwa mabovu na ukosefu wa taa katika chumba cha kutokosea vifaa, (stearlization Room) vifaa vya kubebea madawa ambavyo vinanesa nesa na vifaa vya kuchemshia vifaa vya upasuaji vikiwa chakavu na sehemu ya kuwekea vifaa hivyo ikiwa pia chakavu. 
 
Akiwa katika chumba cha upasuaji cha Murangi alipokelewa na harufu za damu iliyooza na harufu ya popo,huku vifaa vya kutupia taka zikiwa ni ndoo za mafuta ya kupikia na kuagiza pia usafi ufanyike na kuondolewa kwa kinyesi cha popo na kuziba maeneo wanayopita kwani sehemu hiyo inatakiwa kuwa na usafi wa hali ya juu. 
 
Aidha aliagiza kuwepo kwa mtaalamu wa mashine mpya iliyopo katika chumba hicho,na mashine ya usingizi,(Anaesthesia Machine), kwani hakuna mtaalamu na kuwekwa mfumo wa computer ili kukusanya mapato halisi. Akiwa katika wodi ya wazazi aliwasalimu wazazi waliojifungua siku hiyo na kuwaombea afya njema. 
 
Nao Wazazi, Nyachiro Phares wa kata ya chumwi aliyejifungua siku hiyo mtoto wa kike na Sikujua Goda wa Kata ya Musanja aliyejifungua mtoto wa kiume waliipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Mwanamke anajifungua salama kuliko hapo awali ambapo walikuwa wanajifungua nyumbani hali ambayo ilikuwa inahatarisha afya na usalama wao. 
 
Akizungumza mara baada ya Naibu Waziri kutembelea wodi ya wazazi,chumba cha upasuaji na Maabara, Mjumbe Mkutano Mkuu UWT Taifa kutoka Wilaya ya Musoma, Eva-Sweet Musiba alimpongeza Naibu waziri huyo kwa ziara yake Mkoani Mara ambayo italeta chachu ya kufanya kazi kwa uadilifu na si kwa mazoea ambayo yalikuwa yamekidhiri. Aidha amewataka akina Mama kuipenda Serikali ya awamu ya Tano kwani inajali akina mama, wazee na watoto. 


Monday 25 September 2017

WAZIRI MKUU AHANI MSIBA WA MJUMBE WA MKUTANIO MKUU WA CCM RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Maudia Abdaallah ambaye ni Mjane wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  ya wilaya ya Ruangwa, Marehemu  Selemani Bakari  wakati alipokwenda kuhani msiba huo, Majohe, Ilala jijini Dar es salam Septemba 25, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji  katika msiba wa   Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa , Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda Majohe wilayani Ilala jijini Dar es salaam kuhani msiba huo, Septemba 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Saturday 23 September 2017

RAIS MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JESHI 422 JIJINI ARUSHA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Maafisa wapya 422 wakipita Jukwaa kuu baadea ya kutunukiwa kamishenin  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nan Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania an Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
Sehemu ya umati wa maelfu ya wananchi ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania an Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na madiwani na waliowahi kuwa madiwani wa CHADEMA walioamua kuhamia CCM wakati wa sherehe za kukamisheni maafisa wapya wa kijeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017