Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 30 March 2018

RC SHIGELLA MGENI RASMI TANGA CITY MARATHON JUMAMOSI WIKI HII MJINI TANGA

Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho kulia akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,
Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, Kawkab Hussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu
Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo
******************
MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika Jumamosi wiki hii mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya washiriki wakithibitisha kushiriki.

Alisema katika mashindano hayo msimu huu watazamia washiriki zaidi ya600 ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo medali ambazo zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.

Aidha alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo hilo.

“Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha umahiri wao.

Alisema njia zitakazopitia mashindano hayo zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa wakimbiaji ili kuweza kuepukana na adhari zinazoweza kujitokeza wakati yakiendelea.

Naye kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi.

Alizitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa kwanza km 21 atapata700,000 wa pili 500,000, huku mshindi wa tatu akipata 300,000 huku wengine kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha 50,000.

Hata hivyo alisema katika kilomita 10 mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa pili 150,000 na wa tatu 100,000 huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne mpaka 10 watapewa 30,000 pia kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa huduma ya maji kwa wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)


SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) watashirikiana kwa pamoja kuandaa Maonesho ya Kilimo NaneNane Kitaifa  yatakayofanyika Mkoa wa Simiyu Mwaka 2018.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utatoa dira ya kuyafanya Maonesho ya Kilimo NaneNane yawe ni Maonesho ya Kilimo Biashara ili Watanzania wapate fursa ya kuona teknolojia mbalimbali kwenye eneo la kilimo, mifugo na uvuvi.
 
“Matarajio yetu kama mkoa kwa kushirikiana na TanTrade ni kuona kwamba tunaingiza Maonesho ya Kilimo NaneNane kuwa tukio ambalo litawakaribisha watu wenye teknolojia mbalimbali Kitaifa na Kimataifa kwenye kuwezesha mageuzi ya kilimo,uvuvi na ufugaji wa nchi kwa kuonesha ni kwa namna gani wanaweza kumfikia mkulima, mvuvi na mfugaji mdogomdogo kwenye teknolojia ya kisasa ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili Maonesho ya Kilimo NaneNane yawekwe kwenye ramani ya dunia” alieleza Mtaka

Aliendelea kwa kuziomba Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali kuyatumia Maonesho haya kuyatangaza kwa kukaribisha makampuni yenye teknolojia kuja kuonesha mkoani Simiyu. 

Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwa makundi yote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo litakalofanyika Maonesho ya Kilimo Biashara ili uwekezaji huo uendane na viwango vya Kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka ameeleza kuwa TanTrade ni taasisi pekee iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya Maonesho ndani na nje ya nchi kisheria.

Hivyo,Rutageruka amesema kutokana na uzoefu wa uandaaji wa Maonesho mbalimbali,  kwa mwaka 2018 Maonesho ya Kilimo Biashara yatakuwa ni Maonesho bora kwasababu watawaandaa washiriki wote Kisekta,  kuweka miundo mbinu ya kisasa na kuyafanya Maonesho haya kuwa ya Kimataifa.

“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ina kiu ya kuona Maonesho ya Kilimo Biashara  yanakuwa ya kisasa  kama ilivyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambayo kwa Afrika Mashariki ndio Maonesho yanayoongoza kwa ubora na Maonesho haya ya Kilimo tutayafikisha huko” aliongeza Bw Rutageruka


WATALII WENGI WAZIDI KUTEMBELEA TANZANIA - WAZIRI KIGWANGALLA

 Waziri wa Mali  Asili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Dodoma jana.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudensi Milanzi  akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa mkutano huo.
**************

Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143 mwaka 2017 hali iliyopelekea kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika mjini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Wizara yake itaendelea kuvutia watalii wengi zaidi ili kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa.

“Mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 2.1 mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani Bilioni 2.2 mwaka 2017” alisema Dk. Kigwangalla.

Akifafanua Dkt. Kigwangala amesema lengo la Serikali ni kuona mafanikio haya yanazidi kuimarika, hivyo kila mtumishi katika Wizara hiyo lazima atimize wajibu wake ipasavyo katika kutimiza lengo la Wizara hiyo ambalo ni kuhifadhi na kusimamia maliasili, malikale na kuendeleza utalii.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha majukumu ya Wizara hiyo ipasavyo ni muhimu kuwa na bajeti ambayo itawezesha kushughulikia changamoto za migogoro ya mipaka katika maeneo ya hifadhi, kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali, upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea kazi, kutoa elimu ya maadili na kusimamia watumishi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Wednesday 28 March 2018

IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA


 Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro anawashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.

Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.

Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya  utulivu.

Wazazi wanatakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa  kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.

Vilevile Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.

Nawatakia Pasaka njema.

Imetolewa na:
Simon Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi


Tuesday 27 March 2018

KANUNI MBILI ZA SHERIA YA MAWASILIANO ZATANGAZWA


Sunday 25 March 2018

KINANA AZINDUA SEMINA ELEKEZI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA LEO JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James (MCC) Kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Kufungua Semina Elekezi kwa Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Wa Chama cha Mapinduzi leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kutoa maelezo na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo Maalum kwa Wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi ,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni Ndg.Steven Kazidi akiwasilisha Mada katika Semina Elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana CCM Taifa,leo katika Ukumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Meza kuu ikifuatilia Semina
(Picha zote na Fahadi Siraji wa UVCCM)


RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MATAWI KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipeana amani na Masista wa Kanisa Katoliki walipojumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti takatibu wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018


Saturday 24 March 2018

WANARWANGWA TUSHIRIKIANE ILI NAMUNGO FC ICHEZE LIGI KUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.akipata maelezo Jana March 24/2018kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Ruangwa Mkoa wa Lindi(DED) Bwana Andrea Chezue. Jinsi muonekano wa Uwanja wa Michezo wa kisasa Wilaya ya Rungwa utakavyo fanana
*************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa washirikiane kuhakikisha ndoto ya timu yao ya mpira wa miguu ya Namungo FC ya kucheza ligi kuu inatimia.

Amesema timu hiyo limeupa mkoawa Lindi na wilaya hiyo heshima kubwa imepanda imepanda daraja kutoka ligi daraja la pili kwenda daraja la kwanza katika msimu wa 2018/2019.

Waziri Mkuu ameyasema leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa wilaya hiyo kwenye eneo la Namungo na kuwaomba waendelee kuisaidia timu hiyo ili iweze kupanda na kucheza ligi kuu.

Amesema daraja la kwanza linaushindani mkubwa zaidi, hivyo ameutaka uongozi wa timu hiyo kutumia siku 120 zilisalia kabla ya kuanza kwa ligi kwa kufanya maandalizi ya kuisuka timu hiyo kabla ya kuanza mashindano.

“Lazima timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”

Pia Waziri Mkuu amekagua eneo la ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wilayani Ruangwa unaojengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea ambacho kinatarajiwa tumiwa na timu ya Namungo FC.
Awali, Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. Hassan Kungu amesema Namungo FC imefanikiwa kupanda daraja na sasa inashiriki ligi daraja la kwanza na malengo yao ni kuhakikisha inafanya vizuri ili iweze kucheza ligi kuu.

“Mbali na mafanikio hayo, timu yetu ya Namungo FC inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uwanja wenye viwango vya kuweza kucheza mashindano hao pamoja na chombo cha usafiri.”

Akizungumzia historia ya Namungo FC, Bw. Kungu amesema timu hiyo ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini.


WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.



Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.



Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.



Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa bidii.



Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama.



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.



Amesema Serikali imetoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.


 “Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”


Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

Pia, Waziri Mkuu amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya kituoni hapo.


MKUTANO WA BARAZA LA VYUO VIKUU KATIKA NCHI ZA EAC WAWEKA MIKAKATI KUINUA ELIMU YA JUU

Viongozi na wajumbe wa mkutano Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA) wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wakati wa mkutano wa siku mbili uliofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya ambao ulikweka mikakati ya kimarisha viwango vya wahitimu ili kuweza kushindana katika soko la ajira.
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje akizungumza kwenye mkutano huo .

Baadhi ya Wakuu wa taasisi za elimu kutoka Tanzania ambao walikua sehemu ya mkutano huo,kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolijia cha Nelson Mandela mkoa wa Arusha,Profesa Kalori Njau na Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoa wa Kilimanjaro,Profesa Faustin Bee.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya na Maendeleo ya Ukanda wa Kaskazini,Peter Munya akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika ubunifu ,kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje

Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolijia cha Nelson Mandela mkoa wa Arusha,Profesa Kalori Njau (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli za kitaaluma katika Chuo chake kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya na Maendeleo ya Ukanda wa Kaskazini,Peter Munya(katikati) ,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda,Dk Kirunda Kivejinja na viongozi wengine.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Elimu ya Juu nchini (TCU),Profesa Charles Kihampa(katikati) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu miakakti ya pamoja ya kuimarisha elimu ya juu katika nchi za Afrika Mashariki(EAC),kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje na kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St Jonnes mjini Dodoma,Profesa Emmanuel Mbennah.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano ulifanyika jijini Nairobi nchini Kenya.