KUMEKUWEPO na
upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internaship programme) bila malipo yaani
fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza
mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.
Taarifa kwa umma, iliyotolewa na Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kupitia kwa Mkuu Kitengo
cha Mawasiliano Serikali-Afya, Nsachris
Mwamwaja inasema kwa
sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke
waliopo kwenye mafunzo.
"Barua
iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa
ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na
Serikali ya Tanzania," ilisema taarifa hiyo ya Mwamwaja.
Aidha wapo ‘intern’
wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji
mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni
mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo kwa kujigharimia pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao
walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi mapema kumalizia program yao ya udaktari.
Hivyo ni
watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine
waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila
malipo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment