Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 4 May 2017

KAJEMBE; MZARAMO ALIYEUTEKA MJI WA MOSHI KWA BIASHARA YA KUKAANGA MIHOGO

WAANDISHI wa Habari ni watu wa kuzunbuka sana nchini na Duniani kwa ujumla katika harakati za utafutaji habari za kuhabarisha jamii juu ya nini kimetokea wapi na kwanini kimetokea kama kina faida basi kitaweza kusaidia jamii nyingine inaposoma habari hiyo kwa kuelimisha, kuhabarisha au hata kuburudisha.

Februari 23,2012 Mpigapicha/Mwandishi wa Tovuti hii, Mroki Mroki alifika katika mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro na katika pitapita zake mtaani alibahatika kupita katika mtaa mmmoja maarufu na kukuta watu wengi wakisubiri kupaa huduma ya Mihogo ya kukaanga.

Hali ile na kwa jinsi alivyokuwa akiijua vyema Historia ya Mji wa Moshi na wachaga kwa ujumla juu ya ulaji wa mihogo ilimfanya nae aungane na watu wale kusubiri kupata kipande cha m,hogo wa kukaanga.

Wakati anasubiri alihamasika kuzungumza na mwendeshaji wa biashara hiyo na kukubaliana kuchukua taswira za biashara hiyo kuanzia maandalizi hadi ulaji wake huku wakiongea mawili matatu juu ya biashara hiyo.

Hakuna asiyejua kuwa wachaga walikuwa hawali mihogo kutokana na hapo zamani kula chakula hicho na watu kufa hivyo waliamini kuwa mihogo huwa na simu na si chakula kimfaacho binadamu kwa namna yeyote ile.

Lakini siku hizi hali ni tofauti katika Mji wa Moshi, kwani kila ifikapo jioni majira ya saa 10 hivi, baadhi ya wakazi wa Moshi wanakuwa katika haraka ya kwenda mahali kujipatia chakula wakipendacho. Chakula hiki kimetokea kuwavuta wengi sana ambao hata hapo awali walikuwa wakiamini yakwamba ulaji wa mihogo ni hatari sana.

Hofu hii ilitokana na baadhi ya wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro hususani wachagga kuamini kuwa mihogo ni sumu na si chakula, lakini siku hizi mihogo inalika kwa wingi katika mji huu bila kuchagua kabila la mchagga, mpare, muarusha, mzungu ama anatoa Esia. 
Aliyefanikiwa kuwateka wakazi wa Moshi na kuwafanya kila ifikapo jioni wahahe kuitafuta Mihogo si mwingine bali ni Mzaramo Mzaliwa wa Chanika pale Kisumu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na hapa moshi anajulikana kama Mzee Kajembe. 
Nilipofika katika ofisi yake swali la kwanza kumuuliza kuwa “Mzee wewe ni mwenyeji wa wapi?” akiwa na tabasamu na pasi na shaka alinijibu kuwa mimi mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam.
Kwajibu hilo, nikawa sina swali bali nilimpa hongera kwa kufanikiwa kuleta chakula cha Kizaramo mjini Moshi na kukiandaa vyema kiasi cha Mchagga kushindwa kulala bila kula kipande cha Mhogo kutoka kwa Kajembe.

Jinalake halini ni Rashid Nassor Kajembe, ananiambia kuwa aliingia mji wa Moshi akiyoka uzaramkoni mwaka 1982 na ilipofika mwaka 1984 akaamua kuanza kuuza mihogo ya kukaanga. 

Anasema mwanzo daima ni mgumu lakini sasa kidogo afadhali, maana anasema alipoanzia DSM Street miaka hiyo na bade katika mitaa ya Simu tofauti na sasa alipo New Street.

Kiukweli anawateja wa kila namna anasema Wahindi nao wanaila sana mihogo tena huifuata na kupanga foleni. Mhindi anasema “Walahi Ogo tamu kushinda Makate” Tupate matukio zaidi ya picha.
 Mihogo ikiwa jikoni katika eneo ambalo Mzee Kajembe anafanyia biashara Kajembe Shop.
 Kajembe akiwa na kijana wake Juma Kajembe wakimenya mihogo majira ya asubuhi.
  Mzee Kajembe akimenya mihogo hiyo
Wateja wa Mihogo ya Mzee Kajembe kama nilivyowaambia hapo awali kuwa ni wa kila aina na kila rika.
 Mmoja wa vijana wa Mzee Kajembe, Mohamed Ally akiweka mihogo jikoni


 Vijana hawapendi Chips mjini Moshi ni Mihogo tu kutoka kwa Mzee Kajembe. Mdau nakusihi ufikapo mjini Moshi usiache kufika New Street jirani na Hoteli maarufu za Zebra na Buffalo ujipatie Mihogo ya aina yake. Habari hii ilichapishwa mara ya kwanza na Fadher Kidevu Blog 2012.


5 comments:

 1. DAAAAH mzee anapika mihogo mitamu sana asee. nlipelekaga wazungu pale mwaka jana mpaka leo wakinitafuta kunisalimia wanaiulizia

  ReplyDelete
 2. Mzee Kajembe nimekaa naye sana. Aliwahi kufanya kazi TBL miaka ya tisini. Pia ni mtaalamu wa kukaanga karanga.

  ReplyDelete
 3. Nikae kimya tu. Huyu mzee sio kwa utaalamu na akili, nimefanya utundu mwingi sana na ukorofi utotoni ili kwenda kula kwake.

  ReplyDelete
 4. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 5. Huyu mzee ni shida wahindi wakiikosa mihogo kwake wanaandamana. Mimi si mlaji wa mihogo lakini baada ya kuionja miogo yake nilipokaribishwa na dada mmoja wa bufallo cafe nilianza kuwa mlevi wa mihogo. Napenda navyojitahidi kuwa msafi na umakini katika uandaaji wa mihogo yake. Ni kweli kauteka mji wa moshi kuanzia wahindi, wazungu, wachina na sisi waafrika. Si rahisi kumshawishi mangi kula mihogo wakati mangi ni mzee wa nyama choma na bia. Nampa Salute na kuwasihi wafanya biashara wengine wadogo kutokata tamaa katika kukuza biashara zao. Ubunifu na kujituma ni chachu ya mafanikio katika biashara

  ReplyDelete