Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Utalii Mhe. Maitha Saif Majid aliefuatana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy walipokutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 18, 2017
Rais Dkt. John Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 18, 2017
Rais
Dkt. John Magufuli katika
picha ya kumbukumbu na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed
Hamad Al Rumhy na ujumbe wake baada ya kukutana na kufanya naye
mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 18, 2017
********************
MFALME
wa Oman Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said amemhakikishia Rais, Dkt. John Magufuli
kuwa nchi hiyo ipo tayari kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa
kuongeza uwekezaji katika viwanda, uzalishaji wa nishati, kuongeza thamani ya
madini, kuendeleza sekta ya gesi na mafuta na kuendeleza ukanda wa uwekezaji wa
Bagamoyo ili kukuza uchumi kwa kasi zaidi.
Ujumbe
huu wa Mfalme wa Oman umewasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Mafuta na
Gesi wa Oman, Dkt. Mohammed Hamad Al Rumhy aliyeongozana na Waziri wa Uwekezaji
wa Oman , Salem Ben Nasser Al Ismaily na Naibu Waziri wa Utalii, Maitha Saif
Majid, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Rumhy ambaye ameongoza watu zaidi 300 waliokuja nchini kwa meli ya Mfalme wa
Oman amesema ziara hii imelenga kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman
hususani katika masuala ya uchumi, ambapo Oman inabadilishana uzoefu na
Tanzania kuhusu biashara ya mafuta na gesi, itajenga kiwanda kikubwa cha
kuzalisha mbolea katika ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo, itajenga viwanda vya
mazao na kununua mazao ya wakulima na itawekeza katika uchakataji wa madini ili
kuongeza thamani.
“Rais
tunataka kushirikiana nanyi kuendeleza ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo,
tunataka Bagamoyo isiwe eneo la bandari tu, bali pia liwe ni eneo ambalo
tutajenga viwanda mbalimbali, tuzalishe mbolea na tununue mazao ya wakulima na
kuyasafirisha, sisi tupo tayari na kesho tunakwenda kuangalia eneo hilo ili
kazi zianze mara moja” amesema Dkt. Rumhy.
Kwa
upande wake Rais Magufuli amemshukuru Mfalme wa Oman MtukufuSayyid Qaboos bin
Said Al Said kwa kutuma ujumbe huo na amemhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari
kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na Oman.
Rais
Magufuli amemtaka Dkt. Rumhy kufikisha ujumbe wake kwa Mfalme na wawekezaji wa
Oman kuwa atafurahi kuona uwekezaji huo unaanza mara moja na kwamba Serikali
itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika kwa manufaa ya pande zote mbili.
“Dkt.
Mohamed naomba ukamwambie Mfalme kuwa namshukuru kwa ujumbe huu na namkaribisha
sana Tanzania, nimefurahi kuona mpo tayari kushirikiana nasi kujenga viwanda,
kuzalisha mazao na kuendeleza ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo, sisi tupo tayari
hata leo, njooni tushirikiane kwa sababu nyinyi ni ndugu zetu na tutafanya
uwekezaji kwa faida yetu sote” amesema Rais
Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli ametaka Oman iongeze ushirikiano na Tanzania katika masuala ya
utalii na usafiri wa anga, kuwekeza katika usindikaji wa nyama na uvuvi na
ushirikiano katika kubadilishana wataalamu wa nyanja mbalimbali wakiwemo walimu
wa lugha ya Kiswahili na Kiarabu.
Amemshukuru
Mfalme wa Oman kwa msaada kujenga visima vya maji 100 hapa nchini na amemuomba
kuungana na Serikali katika safari yake ya kuhamia Dodoma kwa kujenga
miundombinu itakayoweka kumbukumbu ya ushirikiano wa kidugu na kihistoria kati
ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Dkt. Suzan Alphonce Kolimba.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment