Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 30 June 2017

FERRE GOLA ALIVYOKONGA MASHABIKI WA MUZIKI WA DANSI SHOW YAKE YA KWANZA DAR

 Mwanamuziki Ferre Gola wa Congo, Djany Pacha, akiwa hewani baada ya kubinjuka sarakasi wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama.
Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (katikati) akiimba na kucheza sambamba na wanenguaji wake wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Agostino Maige, akicheza sebene na muongoza shughuli 'Mc' Mussa , wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama. 
 Rapa Mwanamke Ruth Nzele, wa mwanamuziki wa Kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola, akirap wakati bendi yake ikitoa burudani katika onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama. 
 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Agostino Maige, akipiga makofi kumshangilia mnenguaji wa Ferre Gola,  Ilunga Mulumba, wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


JENGO LA ABIRIA LA TERMINAL III KUKAMILIKA MWAKANI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika pichaa ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na watendaji mbalimbali mara baaada ya kukagua ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo mchana.

Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International,  Rey Blumrick akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wa hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo mchana.

Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International, Rey Blumrick akifafanua Jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa  Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema, mradi wa ujenzi wa jengo la abiria namba tatu (terminal III) unatarajiwa kukamilika Septemba, mwakani.

Mbarawa ameyasema hayo leo, baada ya kutembelea na kukagua mradi huo ambapo pia ameoneshwa kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake na kwamba hadi sasa baadhi ya vifaa vimeshaanza kufungwa.

“Tumeona iko haja ya kuendelea na mkandarasi huyu ili kuhakikisha anamaliza kazi katika muda ambao tumekubaliana,” amesema.

“Jengo hili likishakamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua watu milioni sita kwa mwaka lakini ukijumlisha Terminal II na III zitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka,”.

Aidha, Profesa Mbarawa amemuhakikishia mkandarasi wa jengo hilo, Bam International kuwa serikali itakuwa ikilipa kwa haraka malipo yote baada ya mkandarasi huyo kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa kazi alizofanya na kuhakiki.


LYANGA ATEULIWA KUWA KAMANDA WA KANDA MAALUM YA PWANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amemteua,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Onesmo Lyanga kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Pwani ikiwa ni hatua ya kupambana na matukio ya uhalifu katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. Anaandika Katuma Masamba.

IGP Sirro amemtangaza Lyanga kuchukua nafasi hiyo leo (Ijumaa) katika makao makuu ya jeshi hilo wakati akizungumza na wanahabari.

“Wananchi wampe ushirikiano kwa sababu matatizo ya kule hayawezi kumalizwa na vyombo vya dola, bali kwa kushirikiano na wao, watoe taarifa ili hawa wahalifu wapatikane,” amesema Sirro.

Lyanga kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema, kwa ssaa serikali inafanya jitihada za kurekebisha miundombinu ili kanda hiyo mpya iweze kufanya kazi zake vizuri.

“Kanda hii imeshaanza kazi na Kamanda wake ameshateuliwa… suala la kumaliza uhalifu Kibiti na Mkuranga ni suala ambalo halina mjadala ni suala la lazima,” amesema.


MASAUNI ATANGAZA MAJINA YA WATUHUMIWA 16 WA MAUAJI YANAYOENDELEA KIBITI, MKURANGA NA IKWIRIRI

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani y Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI

Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akionesha moja ya silaha zilizopatikana katika mapambano hayo.
 **************
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji  katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani. Anaandika Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
 
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
 
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu  na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
 
“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.
 
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
 
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.


DAR YAPONGEZWA KWA KUFUNGUA KITUO CHA URITHI WA UBUNIFU MAJENGO NA UTALII Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , Nuru Millao (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini , Roeland Van De Geer (kulia) wakifunua kitambaa kuonyesha jiwe la msingi linaashiriwa kufunguliwa kwa  Kituo  cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo katika jengo la Old Boma leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Millao akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla ya kufungua kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo  na Utalii kilichopo katika jengo la Old Boma leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiongea na wageni (hawapo katika picha) wakati wa hafla ya kufungua  Kituo  cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii  kilichopo katika jengo la Old Boma leo  Jijini Dare s Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (mwenye mtandio) akiwa katika picha na wageni waliohudhuria hafla ya ya kufungua kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo kilichopo katika jengo la Old Boma na Utalii leo Jijini Dar es Salaam
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , Nuru Millao  ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kulifanya jengo la Old Boma kuwa Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na Utalii (DARCHI).Anaandika Lorietha Laurence- WHUSM.

Akizungumza katika hafla ya kufungua  kituo  hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, Millao alisema hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unadumishwa na kukuzwa.

“Ni dhahiri kuwa wananchi  wataweza kufahamu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi majengo ya kale kutokana na elimu watakayoipata kupitia kituo hiki katika kukuza utamaduni ” alisema Millao.

Aidha alitoa wito kwa kwa Jumuiya ya Wasanifu Majengo Tanzania kuendelea kushirikiana na Taasisi za ndani na nje ya nchi katika kutekeleza mipango ya kutunza majengo na sehemu za kale ili  kuhifadhi historia na utamaduni wa Mtanzania.

Pia amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Jiji la Dar es Salaam kusimamia sheria kwa  kushughulia kero mbalimbali zinazotokana na udhaifu wa sheria za kuendeleza majengo ya kale.

Naye  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameeleza kuwa kufunguliwa kwa  kituo hiko ni fursa ya kukuza pato la uchumi wa nchi kupitia mapato ya watalii watakaokitembelea.

 “Tayari tumeweka mipango mbalimbali ya kuhakikisha Jiji letu la Dar es Salaam linakuwa sehemu ya Utalii kwa kutoa mafunzo kwa madereva Taxii ambao wanahusika katika kuwasafirisha  watalii ili wawe na uelewa zaidi kuhusu kituo hiki ” alisema Mstahiki Meya Mwita.

Kwa Upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini, Roeland Van De Geer amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana kwa karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla katika kuleta maendeleo.


MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta . BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.