Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 30 June 2017

JENGO LA ABIRIA LA TERMINAL III KUKAMILIKA MWAKANI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika pichaa ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na watendaji mbalimbali mara baaada ya kukagua ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo mchana.

Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International,  Rey Blumrick akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wa hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo mchana.

Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International, Rey Blumrick akifafanua Jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa  Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema, mradi wa ujenzi wa jengo la abiria namba tatu (terminal III) unatarajiwa kukamilika Septemba, mwakani.

Mbarawa ameyasema hayo leo, baada ya kutembelea na kukagua mradi huo ambapo pia ameoneshwa kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake na kwamba hadi sasa baadhi ya vifaa vimeshaanza kufungwa.

“Tumeona iko haja ya kuendelea na mkandarasi huyu ili kuhakikisha anamaliza kazi katika muda ambao tumekubaliana,” amesema.

“Jengo hili likishakamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua watu milioni sita kwa mwaka lakini ukijumlisha Terminal II na III zitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka,”.

Aidha, Profesa Mbarawa amemuhakikishia mkandarasi wa jengo hilo, Bam International kuwa serikali itakuwa ikilipa kwa haraka malipo yote baada ya mkandarasi huyo kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa kazi alizofanya na kuhakiki.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment