Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 31 October 2017

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

 Miongoni mwa mabasi 10 chakavu yanatoka kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 za Serikali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akigua magari yanayotakiwa kukarabatiwa.
 Makonda akikagua basi la Jeshi 
 Basi la Magereza kwa ndani
 Makonda akijaribu kuendesha basi la Magereza
 Basi la Polisi ambalo nalo litafanyiwa ukarabati
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach Ltd kwaajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 za Serikali.

Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach ltd kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

Makonda amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya Makonda.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Sasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal Rajabu Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza, Noel James, ambapo wote kwa pamoja wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam.


WALIOTEULIWA KUGOMBEA UDIWANI KATIKA KATA 43 ZITAKAZOFANYA UCHAGUZI MDOGO TAREHE 26 NOVEMBA, 2017

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Oktoba 26,2017, ilifanya Uteuzi wa Wagombea Udiwani kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo katika Kata 43 zilizopo kwenye Halmashauri 36 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017. 
Jumla ya Wanachama Wagombea 177 wa vyama mbalimbali walichukua Fomu ya Uteuzi Na. 8C na Fomu ya Maadili ya Uchaguzi Na. 10, kati yao 174 sawa na asilimia 92.7 ni wanaume na 13 sawa na asilimia 7.3 ni wanawake. 
Jumla ya Wanachama 155 sawa na asilimia 87.6 ya waliochukua fomu za Uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa Wagombea ambapo 145 sawa na asilimia 93.6 ni Wanaume na Wagombea 10 sawa na asilimia 6.4 ni Wanawake. 
Hadi muda wa mwisho wa Uteuzi ulipofika saa 10.00 jioni jumla ya Wanachama 22 sawa na asilimia 12.4 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda uliotakiwa kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo.
Vyama 13 vimesimamisha Wagombea na idadi ya Kata kwa kila Chama ni kama ifuatavyo: ACT-Wazalendo Wagombea 18 (sawa na asilimia 40), ADA-TADEA Mgombea 1 (sawa na asilimia 2), ADC Wagombea 4 (sawa na asilimia 7), CCM Wagombea 43 (sawa na asilimia 100) CHADEMA Wagombea 42 (sawa na asilimia 98), CHAUMA Mgombea 1 (sawa na asilimia 2), CUF Wagombea 30 (sawa na asilimia 70), DP Wagombea 3 (sawa na asilimia 5), NCCR-MAGEUZI Wagombea 6 (sawa na asilimia 16), NRA Wagombea 2 (sawa na asilimia 5), SAU Wagombea 2 (sawa na asilimia 5), TLP Mgombea 1 (sawa na asilimia 2) na UDP asilimia 2 (sawa na asilimia 5).
Aidha jumla ya Wagombea 30 sawa na asilimia 19.4 ya Wagombea walioteuliwa waliwekewa pingamizi na Wagombea wenzao na Msajili wa Vyama vya Siasa kutokana na sababu mbalimbali. 
 Kwa mujibu wa Ratiba ya Uchaguzi Kampeni za Uchaguzi tayari zimeanza na zitaendelea hadi tarehe 25 Novemba, 2017 ikiwa ni siku moja kabla ya Siku ya Uchaguzi. 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavikumbusha Vyama vya Siasa na Wagombea wao kuwa vinapaswa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 wakati wote wa Kampeni na hata Siku ya Uchaguzi. 
Taarifa zaidi kuhusu walioteuliwa na vyama vyao inapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. www.nec.go.tz na NEC ONLINE TV-TANZANIA. 
Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 31 Oktoba, 2017.


MAPEMAAA SIMBA WAANZA KULIA NA WAAMUZI WA VPL


RAIS MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI MKOANI MWANZA LEO

 Rais Dkt. John Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.
Wananchi wa Butimba na Mkuyuni wakifurahi wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.
Rais Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles
Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags
kilichopo Igogo jijini Mwanza.
Rais Dkt. John Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.
Rais  Dkt. John Magufuli akiangalia utengenezaji wa viti vya plastiki katika kiwanda cha Victoria molders and polybags katika eneo la Igogo jijini Mwanza.
 Rais Dkt. John  Magufuli akiangalia mfuniko uliotengenezwa katika kiwanda hicho cha Victoria molders and polybags Igogo jijini Mwanza.
 Rais Dkt. John  Magufuli akisalimiana na Meya ya jiji la Mwanza James Bwire mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags Igogo jijini Mwanza.
Rais Dkt. John  Magufuli akifungua kiwanda cha madawa cha Prince Pharmaceuticals kilichopo Buhongwa nje kidogo jijini Mwanza. PICHA NA
IKULU


TAARIFA YA MATENGENEZO YA DHARURA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KINYEREZI I

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa Wataalamu wetu wanafanya matengenezo ya dharura  katika Mfumo wa kupokea gesi kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia cha Kinyerezi I.

Hivyo Kituo kitazimwa Saa 6:00 mchana hadi Saa 7:00 Mchana ili kupisha matengenezo.

Baadhi ya maeneo mbalimbali ya nchi katika kipindi hicho yatakosa umeme.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-       
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

31/10/2017


Monday 30 October 2017

NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHI NZIMA

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola akishiriki katika uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es salaam. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Kangi Lugola akizungumza na wanahabari wakati akishiriki katika  uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es Salaam.  
 usafishaji wa mitaro likiendelea katika eneo la Tandale kwa Ali Maua, maeneo hayo yameathirika kwa kiasi kikubwa na mvua za hivi karibuni kutokana na kurundikana kwa taka ngumu.
TAMKO LA MHE.  KANGI ALPHAXARD LUGOLA. (Mb.) NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MUUNGANO NA MAZINGIRA JUU YA OPERESHENI MAALUMU IJULIKANAYO  KWA JINA LA "TUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA -TUSALIMIKE"ALILOLITOA KATIKA  ENEO LA  TANDALE KWA MTOGOLE WILAYA YA KINONDONI
            DAR ES SALAAM, 30/10/2017

Harakati mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuweka Majiji, Halmashauri na Miji, yetu safi,  ikiwa ni pamoja na matamko mbalimbali ya viongozi wakuu hapa nchini. Aidha, Halmashauri za miji na majiji zimekuwa zikiendesha kampeni za usafi kwa kuweka siku maalumu za kufanya usafi wa mazingira na pia kusimamia sheria, kanuni, miongozo na sheria ndogo izinayohusu mazingira.

Nguvu za ziada zinahitajika ili Halmashauri ziweze kuchukua hatua za dhati za kudhibiti taka pamoja na kuhakikisha sheria ndogo na sheria nyingine zinatekelezwa kwa vitendo ili kuhakikisha usafi wa mazingira unasimamiwa ipasanyo na kuhakikisha mazingira yanayotuzunguka yanakuwa masafi.

Pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali bado usafi wa mazingira hauridhishi, taka ngumu katika maeneo mbalimbali kama maeneo ya makazi na maeneo ya biashara hazizolewi kwa wakati, utunzaji wa mifereji ya maji ya mvua na utunzaji wa bustani za burudani haujafikia kiwango kinachostahili, taka bado zinatupwa ovyo kando kando ya barabara na chini ya madaraja na pia taka kutumika kama njia ya kuziba makorongo na kuzuia mmomonyoko wa kingo za mito katika makazi ya watu. Tabia hii imesababisha kuziba kwa mifareji iliyotengenezwa kwa gharama kubwa wakati wa mvua na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekea nyumba nyingi kujaa maji na kuharibu mali za wananchi na hata kusababisha vifo.

Katika kuhakikisha kuwa suala la kampeni ya usafi ni endelevu na yenye mafanikio, leo nataka tuzindue  operation maalumu ya kuzibua mitaro yote nchini, operation hii itakuwa endelevu kwa kila Mkoa, Wilaya , Halmashauri, Kata, Mtaa, Kijiji na Kitongoji. Tutahakikisha kuwa watendaji wote kulingana na sheria ya mazingira na kamati zao wanahakikisha kuwa uchafunzi wa mazingira sasa basi. Hatuwezi kuona nchi inaendelea kuwa katika hali ya uchafu wa aina hii,  wananchi wanakufa kwa kipindupindu na magonjwa mengine wakati watendaji wapo katika ngazi zote kwa mujibu wa sheria.

Operation hii itakuwa ya miezi miwili kuanzia tarehe 1 Novemba hadi tarehe 30 Desemba 2017  na haiondoi maelekezo ya awali ya kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Baada ya tahere 30 Desemba 2017 ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hilii utafanyika nchi nzima kuanzia Januari 2018 Operation hii tutaisimamia sisi ndani ya Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Maafisa mazingira wa Mikoa na Wilaya  pamoja na watendaji wote hadi katika ngazi ya kitongoji na kila mtu atawajibika kwa nafasi yake.


Asanteni kwa kunisikiliza


MAKAMU WA RAIS AZINDUA SERA YA HUDUMA NDOGO YA FEDHA MJINI DODOMA


RAIS MAGUFULI ASITISHA UBOMOAJI NYUMBA ZA WANANCHI MWANZA


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Kigwangalla “Sasa tutakamata majangili kuliko kukamata nyara”

 wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini. Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili. 

“Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini. Ameeleza Dkt.Kigwangalla Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili. 

“Jana tumefanikiwa kumkamata, Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. 

Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla.

Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi. 
Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu aliyekamatwa akijipanga kuingia Hifadhi ya Serengeti 
Baadhi ya risasi zilizokamatwa na jangili huyo 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla akiwa pamoja na Mhifadhi wa Mkuu wa Serengeti William Mwakilema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakiangalia mpaka unahishia pori tengefu la Loliondo-Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti mwishoni mwa wiki wakati wa kukagua maeneo hayo yenye mgogoro na wafugaji.


BREAKING NEWS: NYALANDU AJIUZULU UBUNGE

Na Mroki Mroki
MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu ametangaza kujiuzu nafasi zake zote za uongozi ndani ya CCM.

Akitangaza uamuzi huo jijini Arusha leo, Nyalandu amesema amemuandikia barua Spika wa Bunge wa Job Ndugai kumweleza adhma yake ya kujivua nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.

“Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017,” amesema Nyalandu.


Nyalandu ametoa sababu mbalimbali za kujiuzu kwake nafasi hiyo na kusema kuwa anaondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, akiwa amekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa.


DESTINATION TANZANIA EXCITES AMERICAN INFLUENCERS

 Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke enjoying the scenery at Serengeti National Park recently during their visit organized by Tanzania Tourist Board.

By:  Geofrey Tengeneza
Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke the two famous American influencers have successfully concluded their visit in Tanzania following an invitation extended to them by Tanzania Tourist Board  to visit and feature Destination Tanzania in their  social media networks .

While in the country the two young ladies who are popular fashion models and bloggers with thousands of followers in their social media networks in the USA had a chance to visit Serengeti National Park, a site of great animal migration in the World and the Spice Island of Zanzibar where they took and posted different photos in their accounts of Facebook, Instagram, You tube, tweet  as well as writing in their blogs and tweet.

“We had a wonderful experience in Serengeti and here in Zanzibar and most of our readers and followers have so far shown a great interest on destination Tanzania, once we are back in the USA we are going to write a lot” says Stephenie 

The two influencers were in the country as part of the Tanzania Tourist Board (TTB) strategies to engage celebrities and influencers in the massive campaign to promoting Tanzania as a preferred tourist destination by using social media and influencers so that to increase the number of tourists visiting the country and revenues.