Wizara
ya Nishati inawaomba radhi wananchi kufuatia katizo la Umeme lililotokea tarehe
25 na 26 Oktoba, 2017 kuanzia saa 12:30 Jioni.
Katizo
hilo limesababishwa na kukatika kwa waya (Cable)
wa kupeleka Umeme kwenye Geti la kufungulia Maji katika Bwawa la Kidatu
linalozalisha Umeme wa kiasi cha megawati
204.
Hitilafu
hiyo ilisababisha mtambo wa Kidatu pamoja na mitambo mingine ya kuzalisha Umeme
katika sehemu mbalimbali nchini kutoka kwenye Gridi ya Taifa na hivyo
kusababisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye mfumo wa Gridi hiyo kukosa Umeme.
Serikali
imefanya jitihada za kurejesha Umeme kuanzia tarehe 25 Oktoba, 2017, usiku ili
kuhakikisha kuwa Umeme unarudi katika hali yake ya kawaida kwa nchi nzima.
Hadi
kufikia tarehe 26 Oktoba, 2017, baadhi ya mitambo imeanza kufanya kazi na hivyo
maeneo mengi nchini yanapata Umeme.
Aidha,
mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha Umeme wa Megawati 129, utaanza
kuzalisha Umeme ifikapo tarehe 27 Oktoba, 2017, saa 5:00 asubuhi, hivyo kufanya
maeneo yote nchini kupata Umeme.
Hatua
za dharura na za muda mrefu zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha tatizo la
kukatika kwa Umeme halijirudii. Hatua hizo ni pamoja na kukarabatiwa kwa mitambo
yote ya kuzalisha Umeme iliyoharibika ndani ya kipindi cha wiki mbili.
Hatua
nyingine ni kukarabati mfumo wa kituo cha kudhibiti mifumo ya Umeme (Grid Control Centre) ili kuweza kufanya
kazi kwa ufanisi ikiwemo utoaji wa taarifa mbalimbali za hali ya udhibiti wa
mfumo wa Umeme katika Gridi ya Taifa.
Imetolewa na,
NAIBU KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI
26
Oktoba, 2017
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment