Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli akiwa katika Gari
maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa
sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa
Jamhuri
Vikosi
vya Jeshi la Wananchi wa TRanzania JWTZ,pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji
wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli
Baadhi
ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano
wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli. Picha
na Ikulu.
***********
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April
2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Akizungumza mara
baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa
heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara
Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba
atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.
''Muungano ndio
silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda
Muungano kwa nguvu zote. Yeyote
atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema
Rais Magufuli.
Aidha Dkt.
Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani
amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais Magufuli
amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio
makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa
moja lenye nguvu.
Aidha amesema Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja
za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Rais ametaja
mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na
kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu
ya usafiri wa anga, majini,reli na nchi
kavu.
Aidha Muungano
umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na
kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia
nchini.
Kwa mara ya
kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya
Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni
ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi
imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
''Niwahahakikishie
wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na
hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi
mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema
Rais magufuli.
Sherehe za miaka 53
ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa
viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere
na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.
Kauli mbiu ya Sherehe
za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya
muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi
kwa Bidii''
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment