Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Bidhaa za Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Mbazi Msuya akipokea nakala ya gazeti la Daily News kutoka kwa Ofisa wa TSN, Suzane Kessy alipotembelea banda la Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanataraji kufikia kilele Julai 13 mwaka huu. Brigedia Msuya aliiambia TSN Online kuwa maonesho mengine makubwa ya Bidhaa za zinazozalishwa na Viwanda vya ndani kufanyika Desemba mwaka huu yakiwa na lengo la kuonesho Uwezo wa Tanzania katika Uchumi wa Viwanda.
Miongoni mwa Bidhaa ambazo huzalishwa nchini Tanzania kwa viwanda vya Ndani ni pamoja n bidhaa za ngozi kama hizi.
TAZAMA VIDEO HII.
TAZAMA VIDEO HII.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment