SHEHE wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum
ameipongeza Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kuzalisha bidhaa zilizo
makini, jambo linaloonesha jinsi ambavyo serikali inafanya kazi nzuri.
Anaandika Lucy Lyatuu.
Kampuni hiyo ni wazalishaji wa magazeti ya Daily News,
HabariLeo, Sunday News, HabariLeo Jumapili na SpotiLeo pamoja na majarida
mbalimbali.
Shehe Salum alisema hayo jana wakati akiwa katika banda
la kampuni hiyo lililoko katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar
es Salaam (DITF) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya
Kilwa.
Alisema magazeti hayo yameboreshwa kwa kiwango kikubwa na
yamekuwa yakitoa taarifa sahihi katika jamii na hata juu ya utendaji mbalimbali
wa serikali.
Aliwasihi waandishi hao kuendelea kuzingatia maadili,
tija na ufanisi katika kazi zao ili kwamba Watanzania waendelee kuwaamini kwani
wengi wao wameamka, wanaelewa na ni wasomaji wakubwa wa magazeti.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment