Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (mwenye kombati) akisaidia kupanga kuni kwaajili ya kutekeza bangi iliyokamatwa katika msako maalu wa dawa za kulevya Wilayani humo.
Mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa kwa kulima bangi akitiwa mbaroni.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma
,
JUMLA ya hekari nne za
mashamba ya bangi zimeteketezwa kwa
moto Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma pamojoa na watuhumiwa watatu waliokuwa
wakijihusisha na ulimaji wa zao hilo
haramu kutiwa mbaroni .
Uteketezaji huo
umefanyika katika msako maalum ulioanza mapema wiki hii ukihusisha Kamati ya
ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kakonko.
Akiongoza zoezi la
uteketetezaji wa bangi hekari tatu zilizo kutwa zimelimwa katika hifadhi ya
akiba ya wanyama pori ya Kigosi Moyowosi
Wilayani humo jana, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea
Ndagala alisema kamati ya ulinzi na usalama ilipata taarifa kutoka kwa Wananchi
wanaochukia uhalifu kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo kunawatu wanalima bhagi
ndipo walipo amua kuanza msako huo.
Kanali Ndagala alisema
zoezi hilo la kuwasaka walima bangi na kuteketeza bangi iliyo kutwa katika
mashamba ya walima bangi, limeanza jumatatu ya wiki hii na mpaka sasa
wamefanikiwa kuchoma hekari nne za mashamba ya bangi na kukamata watuhumiwa
watatu waliokuwa wakijihusisha na ulimaji wa zao hilo ambapo shamba moja
walitembea mwendo wa masaa manne kwa piki piki hadi kufikia eneo hilo wanalo
lima .
Alisema katika hifadhi
ya akiba ya Wanyama pori walifanikiwa kukamata shamba lenye hekari tatu na
mtuhumiwa, Ntibalima Masuhuko Mkazi wa Kazuramihunda aliekutwa katika shamba
hilo na Kijiji cha Mbizi kitongoji cha
Nyangereke waliteketeza shamba la bangi hekari moja na kukamata watuhumiwa
wawili waliokuwa wakilima shamba hilo.
Hata hivyo Kanali
Ndagala alisema zoezi hilo ni endelevu wataendelea kuwasaka wote wanao lima
bangi kokote pale walipo hata majumbani kwao ilikuhakikisha wanaokoa Vijana
walio asilika na dawa za kulevya ambao wengi wao wanadhiriki hata katika
vitendo vya wizi na ujambazi kutokana na msukumo wa dawa hizo.
"Nitoe onyo kwa
Wafanya biashara wa dawa za kulevya waache tabia hiyo serikali yetu inamacho
kila kona na watoto wengi wameharibikiwa kwasababu ya tamaa za watu wachache
kupata utajiri wa haraka kwa yeyote
tutakae mbaini tutamchukulia sheria ilikuwa fundisho kwa wengine , nimeona kwa
sasa tumejitahidi kuzuia uuzaji wa bangi kwassa haipatikani sana mitaani tuta
hakikisha haipo kabisa", alisema Mkuu huyo.5
Kwa upande wake
Mtuhumiwa mmoja aliekutwa katika Shamba la bangi hekari tatu huko hifadhini
,Ntibalima Masuhuko alidai kuwa alikabidhiwa shamba hilo awe kama mlinzi na
kudai mimea hiyo ya bangi kwamba ni Magugu tuu yaliyo kiwa shambani na hana
uelewa wowote kuhusiana na mmea wa bangi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment