Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Hamisi
Kigwangalla akizungumza na wanahabari.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Hamisi
Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser
Al Ismaily, Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al
Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman,
Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi
Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben
Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la
Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za
Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la
Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Hamisi
Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben
Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la
Oman, Jijini Dar es salaam jana Oktoba 18, 2017
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla
amesema Tanzania na Nchi ya Oman
zimefanya mazungumzo katika kuimalisha sekta ya Utalii hasa kwenye Utalii wa
kukuza Utamaduni na ule wa Kihistoria uliokuwepo miaka mingi kwa Mataifa hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla amebainisha
hayo jioni ya jana Oktoba 18,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye
maonyesho ya nyimbo na ngoma za Taifa la Oman yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo pia tukio lilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wakiwemo Mawaziri na viongozi wa Taifa hilo la Oman ambao wapo
Nchini kwa ziara ya kusambaza Ujumbe wa Amani na Upendo kupitia meli ya
kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia maonyesho ya ngoma na
nyimbo hizo za Taifa la Oman, Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa, Watanzania
wameweza kujifunza na kufurahia utamaduni wa Oman hasa kupitia nyimbo, ngoma na
mashahiri ambapo amebainisha kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano mwema
hususani wa Kiutaduni na kukuza Utamaduni.
“Watanzania na watu wa Taifa la Oman ni ndugu. Hivyo kupitia
ngoma na nyimbo hizi walizoonesha hapa
zinafanana sana za zile za Visiwa vya Zanzibar na ukanda wetu huu wa Pwani wa
Tanzania.
Pia hata baadhi ya viongozi waliokuja na msafara huu
wanazungumza vizuri lugha ya Kiswahili bila kuchanganya na lugha nyingine huku
wengine kama mulivyowaona wana asili ya Tanzania ikiwemo Visiwa hivyo vya
Zanzibar ambapo walizaliwa huko.” Ameeleza Dkt. Kigwangalla.
Aidha, ameeleza kuwa, kwa sasa wanakusudia kutengeneza
chanzo kipya cha Utalii ambacho kitakuwa ni cha Kihistoria na Kiutamaduni baina
ya Mataifa hayo mawili na kufafanua
kuwa, Histoia ya Tanzania hasa Lugha ya Kiswahili huwezi kukitenganisha Bara la
Arab hususani watu wa Oman.
“Kuna wengine wasomi wa Historia na utamaduni wa Uislamu
wamebainisha kwenye taarifa za kisayansi, kuwa pengine hata dini ya kiisilamu
ilianza kufika ukanda wa Pwani wa Afrika Mashariki kabla ya hata haijafika
baadhi ya Nchi ya Mashariki ya Kati.
Hii ni pamoja na makaburi ya kale kule Bagamoyo, Pemba na
sehemu nyingine za Tanzania ambapo kwa pamoja yanaonesha uwepo wa Waislamu na
mashekhe wa kiisilamu waliofika kuanzia mwaka 1200 mpaka hadi 2000, miaka mingi
iliyopita.” Alibainisha Dkt. Kigwangalla.
Ameongeza kuwa: “Wao wakitangaza vivutio vyao, watavitangaza
na vivutio vyetu vya Tanzania. Lakini pia sisi tutatumia fursa vivutio tulivyonavyo
ambavyo wao hawana kama Mbuga za Wanyama kuwaalika watu wa Omani kuja kutalii
Tanzania, kipindi cha Mwezi Juni, Julai hata Agosti wao ni kipindi cha joto
kali kwani wakati mwingine msimu huo
kule wao wanakuwa na utaratibu wa kutoa rikizo ama mapumziko ya muda wa zaidi
ya siku 30 hadi 40 hivyo tutatumia fursa
ya kipindi hicho na hata wale wanaowapokea Oman waweze kuja Tanzania kutalii”
alieleza.
Pia alimalizia kwamba,
ushirikiano huo, utaongeza soko kubwa la kiutalii.
Msafara huo wa viongozi wa Oman wakiwemo Mawaziri na
wafanyakazi wa Meli hiyo ya Mfalme wa Taifa hilo unajumuisha watu zaidi ya 300
ambapo leo Oktoba 19,2017, umetembelea Wilaya ya Bagamoyo kujinea fursa za
kiuwekezaji na uchumi katika ukanda huo wa Pwani huku Meli hiyo kesho Oktoba 20,2017
ikitarajiwa kuondoka kuelekea Mombasa Nchini Kenya.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment