KATIKA
kuhakikisha watanzania wanapata hamasa ya kuishangilia timu ya Taifa ya soka ya
Tanzania U-17, ‘Serengeti Boys’ wanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Nassib Abdul
‘Diamond’ na Ali ‘King’ Kiba watarekodi wimbo maalum wa kuhamasisha kampeni za
kuchangia timu hiyo kuelekea Gabon.
Serengeti
boys ambayo imefuzu fainali za vijana za Afrika zitakazofanyika kwenye mji wa
Librazaville, Gabon inahitaji bilioni moja kwa ajili ya kushiriki fainali hizo
zinazotarajiwa kuanza Mei 14 ambayo ipo kundi moja na Mali, Niger.
Akizungumza na
wandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Kamati ya hamasa ya Serengeti boys ambayo
ipo chini ya serikali, Charles Hilary alisema wameweka mikakati ya kukusanya
fedha kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo.
“Tuliteuliwa
mwezi uliopita na ni muda mfupi sana kabla ya mashindano kuanza lakini
tumekutana na tumeweka mikakati ya kupata kiasi cha bilioni moja na kauli mbiu
ni ‘Kutoka Gabon kwenda India kwenye fainali za dunia’, “ alisema Hillary.
Hillary
alisema msaada wanaohitaji siyo pesa tu hasa msaada wa vyakula, usafiri wa
ndege na vifaa kwa ajili ya kambi kwani itakwenda kuweka kambi Morocco.
Aidha
alisema njia ambazo wameoanisha kupata pesa ni kupitia kila halmashauri
kuchangia kiasi cha milioni moja kila moja na namba ya simu ambayo kila
mtanzania anaweza kuweka pesa na kupiga akachangia.
“Kila
mtanzania anaweza kuchangia kuanzia shilingi 500 na kwa kuzingatia wingi wa
watanzania tutakuwa tumepata pesa za kutosha nap engine kubaki kwa ajili ya
kuipeleka timu hiyo India kwani tunaamini tutafuzu,” alisema Hillary.
Pia Hillary alisema kiwanda cha bia cha Serengeti na Mamlaka
za hifadhi za Taifa (TANAPA) wameonesha nia ya kushirikiana na kamati kutokana
na jina la timu hiyo kufanana moja ya bidhaa/huduma zao.
Naye mjumbe wa kamati hiyo, Beatrice Singano alisema unapiga
namba 223344 na kulipia Selcom na unaweza kulipia kupitia mitandao ya Airtel,
Vodacom na Tigo.
“Ukipiga namba 223344 unakwenda kwenye namba ya mtandao
unaotumia halafu unachagua Selcom na kuweka kiasi cha fedha ambazo unachangia
na pia unaweza kuweka kiasi chochote unachopenda,” alisema Singano
Naye mjumbe
Maulid Kitenge alisema tayari ala za wimbo ambao utaimbwa na Ally Kiba na
Diamond kwa kushirikiana na wasanii kama Mwasiti, Darassa, Vanessa Mdee na
Msagasumu ikwishatengenezwa na wasanii wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti.
“Ali Kiba yuko
Marekani lakini amekwishatumiwa ala ili aingize sauti ila Diamond yupo nchini
na ametumiwa ala na wameahidi kufanya hivyo mara moja na kurejesha kazi hizo,
ili na wasanii wengine waingize sauti zao,”amesema Kitenge.
Wimbo huo utakapokamilika watanzania wanaweza kuununua kama
ringtone kwenye simu zao pia utasambaza kwenye vyombo vyote vya habari kwa
ajili ya kupigwa kuhamasisha watanzania.
Ally Kiba na Diamond wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na
kuwaunganisha watanzania kuichangia Serengeti Boys ambayo ilifuzu fainali za
Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.
Wajumbe wengine ni Selestine Mwesigwa ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Maulid Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu.
Wengine ni Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas; Mkurugenzi wa Global Publishers
Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment