MAJIRA ya Saa 5:25 usiku Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, aliyekuwa akipatiwa matibabu kufuatia shambulio la risasi la kudhuru mwili katika Hospitali ya Rufaa Dodoma (General) alichukuliwa katika gari la wagonjwa hadi Uwanja wa Ndege wa Dodoma tayari kwa safari ya kwenda kwenye matibabu Mjini Nairobi Kenya.
Lissu akisindikizwa na Mwenyekiti wake wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge Peter Msigwa wa Iringa Mjini walisafiri kwa ndege ya Kukodi ya Kampuni ya Flight Link usiku wa saa sita usiku.
Madktari, wauguzi, Ndugu na Jamaa wa Tundu Lissu wakimpakia katika gari la wagonjwa STL 1308 aina ya Iveco mali ya Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupelekwa hadi Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
Wabunge Mbalimbali na Viongozi wengine wa Serikali akiwepo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba walimsindikiza.
Gari la wagonjwa lililompeleka uwanja wa Ndege
Ilikuwa ni simanzi kwa Wabunge
Mke wa Tundu Lissu akiwa na ndugu wengine.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ambao walisafiri na Mbunge Tundu Lissu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment