Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla kuwa Mbunge wa Viti Maalum
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi
(CUF) ,kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Hindu Hamisi Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.
Akizungumzia
uteuzi huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima
Ramadhani amesema kuwa Tume imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla mara baada ya
kupokea taarifa ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kutoka Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kwa
mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Mhe.
Spika aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu kuwepo kwa nafasi wazi ya
mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa
Mbunge wa Viti Malum kupitia chama cha CUF Ndugu Hindu Hamis Mwenda kufariki
dunia.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema
kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya
Uchaguzi ya Serikali za Mitaa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum watatu
(3) kujaza nafasi wazi za madiwani katika Halmashauri tatu za Tanzania Bara.
Madiwani
walioteuliwa ni Ndugu Jane I. Chungwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Rosana S. Mwinyi kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ndugu Pili M.Mfaume kupitia
Chama Cha Wananchi CUF kutoka Halmashauri ya Temeke.
Amesema
uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye
dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13
(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 aliitarifu Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment