MMOJA wa askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa
Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko)
mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa
Oljoro 833KJ Arusha ,akionesha umahiri na ukakamavu wake kwa kuzuia
pikipiki isiondoke kwa mikono.
Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa
Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko)
mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa
Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao kwa kupitiwa
na pikipiki juu ya migongo yao.
Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa
Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko)
mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa
Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao kwa kukunja
kipande cha nondo yenye ujazo wa milimita 16 kwa mikono.
Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa
Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko)
mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa
Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao.
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema nia ya
kuongeza uandikishaji wa vijana wenye elimu ya juu jeshini unalenga kuwa na
askari wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri mambo haraka.
Kundi hilo la 37 la Mwaka 2016 lilipikwa kwa Wiki 18 katika
Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha
kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ.
Akizungumza baada ya gwaride la mwendo wa pole na haraka
kutoa heshima, maonyesho ya askari waliohitimu na kula kiapo cha utii Meja
Generali Masao aliwataka wahitimu hao kuitumia elimu ya juu kama chachu ndani
ya JWTZ.
“Nia ya JWTZ kuongeza uandikishaji wa askari wenye elimu ya
juu ni kuwezesha uwapo wa askari wenye elimu ya kuwawezesha kutafsiri mambo
haraka,” alisema Meja Generali Masao na kuongeza:
“Elimu mliyonayo ikawe chachu ndani ya jeshi,ikalete matokeo
chanya kazini.Isibakie kuandikisha wasomi wasiokuwa na matunda.Tunataka kuona
elimu ikisaidia kufungua wigo wa uelewa kwa wanajeshi wetu,” alisema.
Aidha aliwataka askari hao kujiepusha na matumizi ya nguvu
migogoro kati yao na raia, ikiwamo marufuku kujihusisha na vikundi vya dawa za
kulevya, bangi, unyanyasaji na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
“Itumieni kwa busara mitandao ya kijamii si kwamba hatutaki
muitumie lakini wanajeshi siku zote tuna akiba ya maneno kwani tunaongozwa na
miiko yetu.
“Tukikubaini dhidi ya vitendo hivi utakuwa umepoteza sifa
jeshini na utafukuzwa. Niwasihi jiendelezeni kielimu fanyeni mambo ya
kimaendeleo ili kuepuka kudhalilika wakati wa kustaafu,” alisema
Meja Generali Masao alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha
askari hao jukumu lililombele yao la kulinda nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje,
ikiwamo kusaidia majanga ya kitaifa na kimataifa watakapohitajika.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya awali ya
Kijeshi, RTS Kihangaiko Kanali Chilo Okombo alisema kuwa askari hao 1,833
wamefanya vizuri katika masomo yao huku askari 6 wakishindwa kuhitimu kutokana
na sababu mbalimbali.
Naye Kamanda Kikosi cha 833 KJ Oljoro Luteni Kanali Sijaona
Myala aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanazingatia mambo ya msingi ambayo ni
utii, uhodari na kuheshimu sheria.
Mbali ya kuhudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi sherehe
hizo zilihudhuriwa pia na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini waliofika
kushuhudia ndugu na jamaa zao wakihitimisha mafunzo ya awali ya kijeshi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment