Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 19 September 2017

WAZIRI MKUU AUTAKA MKOA WA PWANI KUBORESHA MAENEO YA UWEKEZAJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea kiwanda cha Sabuni cha KEDS wilayani  Kibaha September 19, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo  na Kushoto  kwake ni Mkurugenzi Mtenaji wa kiwanda hicho, Jack Fen. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Pwani waboreshe miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 19, 2017) wakati akizungumza na kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Keds kilichopo Kibaha na kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford kilichopo Chalinze.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mkoani Pwani na amewaagiza viongozi wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanakuwa na miundombinu muhimu kama maji, umeme na barabara.

“Nimefarijika kuona miradi hii mikubwa ya ujenzi wa viwanda ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika, nawashukuru kwa kuunga mkono mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.”

Amesema mbali na viwanda hivyo kutoa ajira nyingi kwa Watanzania, pia vitakapoanza uzalishaji vitawawezesha wananchi kupata bidhaa mbalimbali kama vigae kwa bei nafuu kwa kuwa vitakuwa vinazalishwa nchini.

Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaofanyakazi kwenye viwanda hivyo wawe mabalozi wazuri wa Taifa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwathibitishia wawekezaji kwamba wao wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na hakuna haja ya kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda hivyo Bw. Jack Feng amesema ujenzi wa huo umekamilika kwa asilimia 90 na sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na ufungaji wa mitambo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji Oktoba mwaka huu.

Amesema vigae watavyovizalisha wanatarajia kuviuza kwa gharama nafuu kwa sababu asilimia 95 ya malighafi inapatikana ndani ya nchi. Pia ameahidi kutoa ajira nyingi kwa wananchi waishio kwenye maeneo yanayozunguka viwanda hivyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo amemuomba Waziri Mkuu awasaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.

Mhandisi Ndikilo amesema mahitaji waliyonayo ya nishati ya umeme ni megawati 92, ambapo kwa sasa wanasambaziwa megawati 40, hivyo ameomba suala hilo lipatiwe ufumbuzi wa haraka ili lisije kuathiri uzalishaji.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment