Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe
amesema uwekezaji unazidi kushamiri nchini Tanzania na TIC inahakikisha
wawekezaji wanaendesha shughuli zao vizuri na kwa faida.
Mwambe amesema hivi TIC imeondoa dosari zote zilizokuwa zinawakwaza
wawekezaji na kwamba mwekezaji mpya anakamilisha mchakato wote wa kupata
vibali na nyaraka nyingine za kumwezesha kuwekeza ndani siku tatu na
kila huduma inapatikana ndani ya Ofisi ya TIC (One Stop Center).
Mwambe ameongeza kuwa kauli za kuwa hali ya uwekezaji Tanzania ni mbaya
ni za uzushi na zenye nia ya kuchafua sifa ya Tanzania ambayo kwa ni
moja ya nchi 10 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi duniani kwa wastani
wa asilimia 7.2, na ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Afrika Mashariki.
Amesema
ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepata uwekezaji wa Dola za
Marekani Bilioni 1.35 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 3 za
Kitanzania, ikifuatiwa na Uganda iliyopata uwekezaji wa Dola za Marekani
Milioni 537 ambao ni chini ya nusu ya Tanzania.
Mwambe ameongeza kuwa pamoja kuwepo kwa hali nzuri ya uwekezaji TIC
inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwavutia wawekezaji na
kuwaeleza fursa mbalimbali muhimu ikiwemo uwepo wa soko la uhakika la
ndani ya nchi na nje ya nchi, vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa na TIC
pamoja na ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment