Serikali imepanga kukarabati
vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Canada
ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88 sambamba na Bil.12 fedha za
kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo (Mb) amesema lengo la
serikali nikuhakikisha ifikapo Desemba 30, mwaka huu shughuli hiyo iwe imekamilika
ipasavyo kwa kusimamiwa karibu na Wakuu wa mikoa wakisaidiana na
Wakuu wa Wilaya.
Jafo amesema kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Serikali imepokea Dolla za
kimarekani Mil. 66 kutoka Benki ya Dunia
ambapo vituo 103 vitakarabatiwa aidha pia Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepata
Msaada kutoka Ubalozi wa Canada wa dolla za kimarekani Mil 22, ambapo vituo 44
vya afya vitakarabatiwa kwa fedha hizo.
Naibu waziri huyo
alisema, fedha zingine zitakazo tumika
katika zoezi hilo ni zile zilizo vuka katika mwaka wa fedha uliopita.
“Vituo 25 vitafanyiwa
ukarabati kupitia fedha za Benki ya Dunia na mfuko wa afya wa pamoja zilizovuka
mwaka wa 2016/2017, ambapo Bil.12 za kitanzania zitatumika,” alisema Jafo na
kuongeza kwamba kila “kituo kitapatiwa shilingi Mil. 500 za
kitanzania na baada ya ukarabati serikali itakuwa na jukumu lakupeka vifaa
katika maeneo hayo”.
Waziri Jafo amesema, Maeneo ya
kipaumbele wakati wa ukarabati huo ni pamoja na
Upasuaji (Theater), Wodi za mama na Mtoto (Martenity),
Maabara(Laboratory), pamja na Nyumba za watumishi sambamba na maeneo mengine ya
kipaumbele kutokana na fedha zilizopo.
Katika hatua nyingine Jafo
amewagiza Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha Taarifa ya kila mwezi ofisini kwake
juu ya maendeleo ya ukarabati, huku akiwataka Wakurugenzi na watendaji wengine
kusimamia kwa ufasaha zoezi hilo.
Naibu Waziri hakusita kuonya
juu wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo na maelekezo ya serikali
yaliyotolewa
“Nawaomba Wabunge na
Madiwani kushirikiana bega kwa bega na watendaji katika kufanikisha zoezi hili
kwa ufanisi, alisema Jafo na kuongeza kwamba,
“ofisi yangu haita mvumilia Kiongozi au Mtendaji yeyote atakaye onekana kutumia
fedha hizo vibaya au kushindwa kutimiza wajibu wake na kisha kukwamisha
shughuli hii muhimu yenye nia njema kwa maisha ya watanzania.
Akihitimisha maagizo hayo Naibu waziri Suleima Jafo, amezishukuru Wizara zote za kisekta katika kusukuma
gurudumu la maendeleo na kwenda sambamba
na kasi ya Rais Mh. Dkt. John Pombe
Magufuli ya HAPA KAZI TU, ikiwapo,
Wizara ya Afya, Fedha na Mipango pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambao
walikuwa bega kwa bega katika mchakato wote wa kupatikana kwa fedha.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment