Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta . BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.
********************
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya
Kaskazini.
ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za
Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya
Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi
jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya
Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo
,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika
Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio
ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari zilizopo katika
vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni
ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo
ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa
huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda
kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi
pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu
ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo
agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa
Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan
walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao
yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount
Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva
walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi Matandiboi wakapiga
simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza
kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi
,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara
Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake
kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe na si kama lilivyofanya
jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha
huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi kwa wasaidizi wake juu ya
agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya
biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa
kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa Mahindi yake ambayo
amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya
Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi
ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao
yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima
aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro
imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha
Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba
na kusafirisha Mahindi kwenda nje ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema
jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa
Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba
yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari
tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)
Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia
tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe
yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema
Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na
usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu
kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na
mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda
kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za
Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa
mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya
nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa
nchi kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la
sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka
agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa Mei 30,2017,uliozuia
utokaji wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza
kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha
Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA) kukosa takwimu muhimu wa bidhaa
zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha
sukari na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa
takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya
askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa
katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza
kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye
kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment