Mhandisi
Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering,Shin Soo akimueleza Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya
ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami
yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi
Johnny Kalupale.
Mafundi wa Kampuni
ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati ya madaraja makubwa
saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa
kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
Meneja wa Wakala
wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale (kulia) akimuonesha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)
hatua mbalimbali za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass),
wakati Waziri huyo alipoikagua, mkoani Arusha.
Moja kati ya
madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa
kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Tingatinga
likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya mchepuo
(Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini
Arusha.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo
kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering,Shin Soo
(katikati)alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha
bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.
*******************
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito kwa wakazi
wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V
ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha
bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
Akikagua mradi
wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa
barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na hivyo
kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.
"Kukamilika
kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano
kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na kurahisisha huduma za
usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri Mbarawa.
Ameongeza kuwa
Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa
wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili vilivyokubalika.
Aidha, Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda uliopangwa.
Aidha, Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda uliopangwa.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven
Ndyamukama, amesema Wizara kwa kushirikiana na TANROADS itaendelea kuhakikisha
barabara na madaraja yote nchini yanajengwa kwa viwango vilivyopo kwenye
usanifu wa kina (Detail design), na thamani ya fedha inapatikana.
Naye, Meneja wa
TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale, amemhakikishia Waziri Prof.
Mbarawa kuendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe mradi kwa wakati
kama walivyokamilisha ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 na kwa ubora
unaostahili.
Mhandisi
Kalupale, ameeleza changamoto zinazoikabili barabara hiyo kuwa ni wingi wa udongo wa tifutifu na mfinyanzi na hivyo kulazimu Usanifu wa kina wa
barabara hiyo kurudiwa upya.
Ujenzi wa
Barabara ya Arusha bypass unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 67
ikiwa ni ushirikiano wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na
Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ujenzi wake utahusisha madaraja makubwa 7,
maboksi kalvari 55 na madaraja ya bomba 55.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment