Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Chemba mkoani
Dodoma wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati mkubwa wa
wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa Barbara
kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kalema
wilayani Chemba wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati
mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa
Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika
maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani
Dodoma.
Amesema
Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama
ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya
maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye
makazi yao.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 20, 2017) alipozungumza
kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Chemba na Kondoa
waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema, Bicha na Bereko akiwa
njianu kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi.
Alisema
kwa sasa Serikali imeendelea na uchumbaji wa visima virefu, vifupi
pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo
mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao.
Pia Waziri Mkuu alisema
wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya
shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo
vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote
watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa
makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa
zinasababisha ukame.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisemahakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa huduma hiyo katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
Ameagiza
wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu ya pili ndipo
waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh. trilioni moja
kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado
havijaunganishiwa nishati hiyo.
“Rais
wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga
fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote
vikiwemo na vya wilaya za Chemba na Kondoa. Gharama za kuunganishiwa
umeme huo ni sh. 27,000 tu.”
Pia
Waziri Mkuu alisema mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo
wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama
hizo zimeshabebwa na Serikali.
Waziri
Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye
vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo
mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira
na kukuza uchumi.
Awali
mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Mjini Bw. Edwin
Sanda na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ambaye ni
Mbunge wa Kondoa Vijijini waliomba Serikali iwasaidie katika kutatua
kero ya maji na umeme.
Walisema
katika maeneo mbalimbali ya majimbo yao wanakabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa huduma ya umeme pamoja na maji safi na salama hivyo
kusababisha wananchi kushindwa kushiriki vema kwenye shughuli za
kimaendeleo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment