Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano
wao na Hospitali ya B.L.K ya nchini India
ambapo kwa pamoja wameweza
kuwafanyia upasuaji wa kufungua na bila
kufungua kifua wagonjwa 64. Kulia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na
Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka
Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa
pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji wa
kufungua na bila kufungua kifua wagonjwa 64. Kushoto ni Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge.
***************
MADAKTARI kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa
ushirikiana na wenzao wa Hospitali ya B.L.K ya nchini India wamewafanyia wagonjwa
64 upasuaji wa moyo ambao ni wa kufungua
na bila kufungua kifua.
Kati ya hao wagonjwa nane
walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na 52 walifanyiwa upasuaji wa bila
kufungua kifua (catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cathlab.
Pia madaktari hao wamepata
mafunzo ya kufanya upasuaji wa milango miwili ya moyo ambapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewi
kwenye taasisi hiyo .
Mafunzo hayo ya siku tano
yaliyo ongozwa na wataalamu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India itasaidia
serikali kuokoa zaidi ya milioni 30 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu ya
mgonjwa wa moyo wenye uhitaji wa upasuaji wa milango miwili ambapo asilimia 25 ya wagonjwa wana uhitaji
huo.
Akizungumza na Waandishi wa
habari jana Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Peter kisenge alisema kupitia kambi ya siku
tano ya madaktari nane wanaotibu maradhi
ya moyo ,Wataalamu wa usingizi ,Wataalamu wa kutoa damu kwenye mapafu ,kutoka
Hosipitali ya BLK ya nchini India imesaidia kutoa mafunzo ya uwekaji na
upasuaji wa milango miwili kwenye moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo ambapo
huduma hiyo itakuwa ya kwanza kutolewa hapa nchini.
Mbali na huduma hiyo Dk
Kisenge alisema tayari madaktari watatu wa taasisi hiyo wanaweza kutoa huduma
ya uwekaji wa milango miwili ya damu kwenye moyo huku Daktari mmoja akipata mafunzo ya miaka
miwili nchini india.
Kuanza kwa huduma hiyo alisema
watasaidia watoto wadogo ambao milango yao imeziba ambapo awali walikuwa
hawafanyiwi upasuaji kutokana kutokuwepo kwa ujuzi wa upasuaji wa milango hiyo.
Alisema kwa wagonjwa 64
waliofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo wangesafirishwa nchini india serikali
ingepoteza zaidi ya bilioni 6 .
Kwa upande wake Daktari Bingwa
Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India Dk
Ajal Kajul alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa madaktari hapa nchini
ambapo baadhi ya madaktari walioambatana nao watabaki katika taasisi hiyo
kwaajili ya kuendelea kutoa mafunzo zaidi.
Dk. Kaul alisema wataendelea kuonyesha ushirikiano
wa kutoa ujuzi kwa madaktari wa hapa nchini ambapo octoba mwaka huu watatoa
mafunzo ya upandikizaji wa figo,na wagonjwa wenye matatizo ya mgongo katika
Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment