WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amezindua mifumo miwili ya kielektroniki
itakayosaidia kuandaa bajeti kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa na
ameonya kwamba mifumo hiyo isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za Serikali .
Mifuyo iliyozinduliwa ni Kupanga Mipango, Kuandaa Bajeti na Kutolea taarifa za hatua za Utekelezaji wa
Bajeti (Planning, Budgeting and Reporting System- PlanRep) pamoja na
mfumo wa Kufanya Malipo na Kutoa Taarifa za fedha ambazo zimetumwa
kwenye Vituo vya Kutoa Huduma (Facility Financial Accounting and
Reporting System-FFARS).
Akizindua mifumo hiyo leo (Jumanne,
Septemba 5, 2017) mjini Dodoma, Waziri Mkuu amesema lengo la mifumo
hiyo mipya ni kuongeza uwajibikaji na ufanisi na kamwe isiwe kikwazo
katika utoaji wa huduma kwa jamii.
“Napenda
kutumia fursa hii kuwafahamisha Viongozi na Watendaji pamoja na
Wananchi wote kwamba, lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza
uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za
Serikali na isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za
Serikali.”
Amesema
ni muhimu mifumo hiyo itumike kwa ufasaha ili kuleta tija inayotarajiwa
na kila muhusika kwa ahakikishe anailinda, anaitunza na kuitumia mifumo
hiyo ili iweze kudumu na kuwa endelevu kwa manufaa ya Taifa.
Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri na Vituo vya kutoa huduma za Elimu na Afya kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mamlaka zinazohusika kwa wakati.
Amesema
ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa zitoe taarifa za mapato na
matumizi kwa Wananchi wanaowahudumia kupitia mikutano, mbao za
matangazo, tovuti, vyombo vya habari na njia nyinginezo.
Waziri
Mkuu amesema kwa sasa Serikali haitarajii kuona kituo chochote cha
kutoa huduma za Elimu na Afya kilichopo chini ya Halmashauri kinakuwa na
matumizi yasiyozingatia taratibu na kanuni za fedha za umma.
“Hatutarajii
kuona viongozi wa mikoa na halmashauri wakibadilisha matumizi ya fedha
bila kuwasiliana na Mamlaka husika. Matumizi ya fedha yafanyike
kutegemea chanzo cha fedha kilichopokelewa kwa wakati na kwa mujibu wa
bajeti iliyotengwa kwa mwaka husika.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi
cheti Nsea Kipilyango ,Kiongozi wa timu ya wataalm ambaye pia ni mwanamke pekee
katika timu ya Wataalma wa mifumo (Programa) waliofanikisha maboresho mapya
katika Mfumo wa kupanga Mipango, Kuandaa
Bajeti (PlanRep) na ule wa Kufanya Malipo na Kutoa Taarifa za fedha ambazo
zimetumwa kwenye Vituo vya Kutoa Huduma (FFARS) aliyoizundua mjini Dodoma jana.(Picha
na Mroki Mroki),
Wataalam na wawezeshaji wa mafunzo na utengenezaji wa Mifumo hiyo walitunukiwa vyeti na Waziri Mkuu. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.
Kaimu
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bi. Inmi Patterson amesema mifumo
hiyo iliyozinduliwa leo itaisaidia Serikali ya Tanzania katika mapambano
dhidi ya vitendo vya rushwa na uboreshaji wa huduma za jamii.
Amesema
Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania katika vita
dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi kwa sababu vinakwamisha utoaji wa
huduma mbalimbali za maendeleo kwa jamii.
“Ufisadi
ni ugonjwa hatari na unaua kama magonjwa mengine yanavyoua. Ufisadi
unazuia maendeleo ya jamii katika nchi husika pamoja na kukwamisha
ukuaji wa uchumi na pia unaua ushindani na ndoto za vijana.”
Amesema
anatambua namna ambavyo Rais Dkt. John Magufuli na wasaidizi wake
wanavyopambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ili kuhakikisha fedha
zote za maendeleo zinazotolewa zinatumika vizuri.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi Bw. George Simbachawene amesema mifumo
hiyo itaziwezesha Halmashauri kupunguza gharama kubwa katika kukamilisha
zoezi zima la uandaaji wa Mipango na Bajeti kwani zilikuwa zikitumia
muda mrefu na gharama kubwa kwenye kuandaa na kuwasilisha Bajeti.
Hesabu
za mwaka 2017/2018 zilizotolewa zinaonyesha kuwa gharama za mchakato wa
maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya mwaka kwa Halmashauri 185 ni
takriban sh. Bilioni 8.32 za kulipia usafiri (Mafuta), posho ya
kujikimu, shajala na gharama za kudurufu Vitabu.
Waziri
Mkuu amesema iwapo kuna mdau anataka kushirikiana na Serikali anapaswa
kutumia na kuboresha mifumo hiyo na siyo kuleta mifumo mingine kwa
sababu uwingi wa mifumo huondoa ufanisi na uwajibikaji.
“Serikali
ina matarajio makubwa na mifumo hii, na nitapenda Ofisi ya Rais -
TAMISEMI na Ofisi yangu zipate taarifa zote za mipango
Msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto alitoa burudani kwa wimbo maalumu kuhusu mifumo hiyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment