Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana.
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akihoji uchafu uliokuwa ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana
Baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mkoa wa Mara, hali hiyo ni kinyume na utaratibu wa vyumba vya upasuaji
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo chumba hicho cha upasuaji huku akipata maelezo.
Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara.
******************
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk.
Hamisi Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji
vya hospitali ya rufaa ya Musoma na zahanati ya Murangi na vyumba hivyo
kubadilishwa stoo na eneo la taka.
Naibu Waziri ambaye Mkoani Mara kwa
ziara ya kikazi ya siku nne alifanya ziara ya kushtukiza katika
hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini uchafu uliopo katika chumba cha
upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa mashuka na mipira yake kuwekwa
chini na huku kukiwa na vifaa vya kuwekea mashuka hayo.
"Hivi ndivyo
mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani ya nyie
kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu jamani, sisi
sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa Mkoa au
mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo hopspitali
ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa?"Alihoji
Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa.
Aidha aliagiza Katibu
Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda kuajiri Mganga mfawidhi wa hospitali
(Medical officer Incharge) mpya atakayesimamia hospitali hiyo.
Sanjali
ya hayo alishangazwa pia kuona chumba hicho mabomba na masinki yakiwa
mabovu na ukosefu wa taa katika chumba cha kutokosea vifaa,
(stearlization Room) vifaa vya kubebea madawa ambavyo vinanesa nesa na
vifaa vya kuchemshia vifaa vya upasuaji vikiwa chakavu na sehemu ya
kuwekea vifaa hivyo ikiwa pia chakavu.
Akiwa katika chumba cha upasuaji
cha Murangi alipokelewa na harufu za damu iliyooza na harufu ya
popo,huku vifaa vya kutupia taka zikiwa ni ndoo za mafuta ya kupikia na
kuagiza pia usafi ufanyike na kuondolewa kwa kinyesi cha popo na kuziba
maeneo wanayopita kwani sehemu hiyo inatakiwa kuwa na usafi wa hali ya
juu.
Aidha aliagiza kuwepo kwa mtaalamu wa mashine mpya iliyopo katika
chumba hicho,na mashine ya usingizi,(Anaesthesia Machine), kwani hakuna
mtaalamu na kuwekwa mfumo wa computer ili kukusanya mapato halisi. Akiwa
katika wodi ya wazazi aliwasalimu wazazi waliojifungua siku hiyo na
kuwaombea afya njema.
Nao Wazazi, Nyachiro Phares wa kata ya chumwi
aliyejifungua siku hiyo mtoto wa kike na Sikujua Goda wa Kata ya Musanja
aliyejifungua mtoto wa kiume waliipongeza Serikali kwa jitihada zake za
kuhakikisha Mwanamke anajifungua salama kuliko hapo awali ambapo
walikuwa wanajifungua nyumbani hali ambayo ilikuwa inahatarisha afya na
usalama wao.
Akizungumza mara baada ya Naibu Waziri kutembelea wodi ya
wazazi,chumba cha upasuaji na Maabara, Mjumbe Mkutano Mkuu UWT Taifa
kutoka Wilaya ya Musoma, Eva-Sweet Musiba alimpongeza Naibu waziri huyo
kwa ziara yake Mkoani Mara ambayo italeta chachu ya kufanya kazi kwa
uadilifu na si kwa mazoea ambayo yalikuwa yamekidhiri. Aidha amewataka
akina Mama kuipenda Serikali ya awamu ya Tano kwani inajali akina mama,
wazee na watoto.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment