Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 28 May 2018

SIMANZI YA TAWALA BUNGENI, KIFO CHA MBUNGE KASUKU BILAGO

 VILIO, Majonzi na Simanzi vimetawala katika viunga vya Bunge jijini Dodoma hii leo kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mwalimu Kasuku Bilago. Anaandika Mroki Mroki – Daily News Digital, Dodoma

Mwalimu Bilago alifikwa na umauti wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumamosi Mei 26, mwaka huu  jijini Dar es Salaam.
 Muda mfupi baada ya Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kufungua kikao cha Bunge kwa kusoma dua, alitoa Bungeni hapo Taarifa ya Spika kuhusiana na msiba huo mzito uliolifika Bunge, naabade kutangaza kuahirisha Bunge hadi Mei 29 saa tatu asubuhi, ili kupisha Maombolezo huku mipango ya kuuleta mwili katika viwanja vya Bunge kwa heshima za mwisho ikifanyika.
 Daily News Digital ilishuhudia wabunge wakitoka Bungeni huku wakiwa na nyuso za huzuni na wengi wao wakibubujikwa na machozi na vilio vya kwikwi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amemtaja marehemu kuwa ni miongoni mwa wabunge Bora ambao walikuwa wakijenga hoja  na kutoa michango yenye maslahi mapana kwa Jimbo lake na nchi kwa ujumla.

Nae Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule alizungumzia msiba huo na kusema ni pengo kubwa Mwalimu Bilago ameliacha si kwa Kambi ya Upinzani bali kwa Bunge zima kutokana na mchango wake aliokuwa akiutoa.
 “Mwalimu Bilago alikuwa Mwalimu kweli kweli, hakuna siku ambayo alisimama kuchangia asipate sapoti ya Bunge zima nah ii ni kutokana na ucheshi wake lakini pia hoja zake za msingi alizokuwa akizitoa Bungeni,”alisema Haule.

Mwili wa Marehemu Bilago unataraji kuletwa Bungeni Mei 29 kwa heshima za mwisho na baade kusafirishwa hadi Kijiji cha Kasuga Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma ambako utahifadhiwa Mei 30 mwaka huu. 
 Wabunge mbalimbali wakifarijiana kufuatia Msiba huo mzito wa Mwezao.
 Mawaziri wakiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha Mbunge Kasuku Bilago wa Jimbo la Buyungu, Wilayani Kakonko mkoa wa Kigoma.
Wabunge wakisaini kitabu cha maombolezo


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment