Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 16 May 2017

TECNO YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO

Kampuni ya Simu ya Tecno ikitoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha upendo kilichopo mkoani Mwanza. Tecno ilitoa vyakula vya thamani ya shilindi 2.5.
*******************
Na Alexander Sanga,Mwanza
Uongozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tecno imetoa msaada wa vyakula wenye gharama ya shilingi milioni 2.5 tsh kwa kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi cha Upendo Daima kilichopo kata ya Nyegezi katika wilaya ya Nyamagana.

Akizungumza katika kusherekea siku ya kimataifa ya familia duniani,meneja wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Gerald Tito alisema kampuni yao imeamua kutoa msaada huo kwa kituo hicho kutokana na watoto wengi wamekuwa wakihitaji misaada lakini wanakosa.

‘’Watoto wasiokuwa na wazazi au walezi wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu sana kutokana na kukosa mahitaji ya muhimu kwao kama vile elimu na chakula.Tumekuja hapa kusaidia kituo hiki kwa lengo la kusaidia jamii nzima’’ Tito alisema

Vyakula vilivyotolewa na kampuni hiyo ni mchele kilogramu 100 kwa Unga wa Sembe, kilogramu 100 za Ngano,Maharage na Sukari. Vitu vingine ni Sabuni za kufulia miche 500,Sabuni za kufulia za Foma gold gramu 4000,mabegi ya shule 40 pamoja na madaftari boksi 3.

Tito aliahidi kampuni yao itaendlea kusaidia vituo mbali mbali vya watoto yatima pamoja na watoto wanaoishi katika mazinigira magumu.Meneja huyo alisema kampuni yao itajitaidi kuhakikisha inasomesha baadhi ya watoto kutoka kituoni hapo.

Mkurugenzi wa kituo cha Upendo Daima Laurent Sabini alishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao na aliomba wadau wengine wajitokeze katika kusaidia kituo hicho.

Sabini alisema changamoto kubwa wanayopata ni ukosefu wa ada kwa wanafunzi waliopo katika shule za sekondari kutoka kituoni kwake na changamoto ya kuwalipa mishahara wafanyakazi wa kituoni kwake.Sabini alisema kituo chao kwa mwezi kinatumia shilingi milioni 3.7tsh kwa mwezi kwajili ya chakula tu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment