Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.Nafasi Ya Matangazo

Friday, 23 June 2017

POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRIJESHI la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya uhalifu klatika siku ya siku kuu ya Eid El Fitri.

Taariofa iliyotolewa na Jeshi hilo kupitia kwa Msemaji wake Advera Bulimba imewataka  wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao.   

"Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao,"ilisema taarifa hiyo.

Naibu kamishna huyo wa Polisi, Advera Bulimba alisema Jeshi la Polisi nchini,  limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba  wananchi wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani  na utulivu.  

Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 

"Vilevile,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini  na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,  Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja  sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi, bodaboda kubeba  mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo," taarifa hiyo ilieleza.

Pia, tunawataka  wananchi wote kuwa wepesi katika  kutoa taarifa kwa kupitia  namba za simu za bure 111 au 112  pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.


RAIS WA PILI WA BOTSWANA SIR MASIRE AFARIKI DUNIARAIS wa pili wa Botswana Sir Kitemure Masire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.

Kufuatia msiba huo, serikali ya Botswana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Sir Ketumile, aliongoza taifa hilo kuanzia 1980 hadi 1998, na amekuwa akisifika  kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka msingi imara wa uthabiti wa kisiasa katika taifa hilo.

Pia alishiriki katika mikakati ya kufanikisha amani katika mataifa kadha Afrika, ikiwa ni pamoja na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Msumbiji.

Botswana ni moja ya nchi tajiri na imara zaidi barani Afrika.

Sir Ketumile alichukua uongozi kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Botswana baada ya uhuru Sir Seretse Khama mwaka 1980.


SPIKA WA BUNGE NDUGAI AKABIDHI VITABU SEKONDARI ZA WILAYA YA KONGWA

 
Spika wa Bunge, Job Ndugai akimkabidhi vitabu Makamu Mkuu wa  Shule ya Sekondari Sejeli , Gerald Kagali ikiwa ni zawadi kwa Shule hiyo, Msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini, tukio lililofanyika leo kijijini Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo,  Mungwe Athman
 Spika wa Binge, Job Ndugai (kushoto) akishuhudia Mwenyeti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Mungwe Athuman akimkabidhi kitabu Mwalimu mkuu wa  Shule ya sekondari Banyibanyi Mwl.Grace Mbise, Ktk tukio lililofanyika leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.     kulia ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa
Spika wa Bunge,Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule Secondary Banyibanyi iliyopo wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma, baada ya kuwapatia vitabu vilivyotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini.
Spika wa Bunge , Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule Secondary Banyibanyi iliyopo wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma, baada ya kuwapatia vitabu vilivyotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini.
Spikawa Bunge, Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari Banyibanyi, baada ya kuwakabidhi vitabu vilivyotolewa kwa msaada wa Mtandao wa kuondoa umasikini, tukio lililofanyika leo wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma.


Thursday, 22 June 2017

RAIS MAGUFULI AMALIZA ZIARA YA SIKU 3 PWANI ATOA MAAGIZO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Juni 22, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 3 Mkoani Pwani kwa kumuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwanyang’anya viwanda watu wote waliouziwa viwanda na Serikali na baadaye kuvitelekeza ili wapatiwe wawekezaji wengine wanaoweza kuviendeleza.

Rais Magufuli amesema kuna viwanda 197 ambavyo viliuzwa kwa watu mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza lakini viwanda hivyo vimekufa na vingine kubadilishiwa matumizi jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za kutekeleza mpango wa ujenzi wa viwanda.

“Waziri wale waliopewa viwanda miaka ile kwa kuuziwa bei ya chee, tukitegemea kwamba vile viwanda vitaendelea kufanya kazi lakini wamevitelekeza na vingine havipo kabisa, usiwe na kigugumizi na wala usiangalie sura, wanyang’anye, wale wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda wapewe, kiwanda sio mwanamwali wa kumtunza ndani, kinatakiwa kifanye kazi kitoe ajira na Serikali ipate mapato” amesema  Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona Fruits Ltd kilichopo katika Kijiji cha Mboga Wilayani Chalinze ambacho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 300 za matunda kwa siku, kuajiri wafanyakazi 800 na kitawanufaisha wakulima 30,000.

Kiwanda hicho kinajengwa na Mtanzania Subhash Patel kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 120.
Kabla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha kutengeneza dawa za viuadudu cha Kibaha ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Cuba kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 22.3 kwa lengo la kuzalisha dawa za kuangamiza viluilui vya mbu na kutokemeza ugonjwa wa malaria.

Akiwa kiwandani hapo Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya kununulia lita takribani 100,000 za viuadudu zilizokwama kiwandani hapo kutokana na Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kutozinunua na ameelekeza kuwa halmashauri zote zitakazopangwa kuchukua viuadudu hivyo ziwe zimechukua kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai.

“Hatuwezi kuwa tunaanzisha viwanda kama hiki cha dawa halafu hatuvitumii, kinazalisha dawa wanatumia watu wa nchi zingine wakati sisi tunaendelea kufa kwa malaria” amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amezindua barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata yenye urefu wa Kilometa 64 na kuipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wote waliofanikisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo inasaidia kutatua tatizo la msongamano wa magari katika barabara ya Chalinze – Dar es Salaam na inapita katika eneo la Bagamoyo ambalo litajengwa bandari mpya na eneo la viwanda.

Ujenzi wa barabara hiyo yenye madaraja makubwa matatu umegharimu Shilingi Bilioni 213 ikiwa ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.

Rais Magufuli pia amezindua kiwanda cha kukausha matunda cha Elven Agri Company Ltd kilichopo katika kijiji cha Mapinga Wilayani Bagamoyo ambacho kina uwezo wa kukausha tani 60,000 za matunda kwa mwaka na kimewekezwa na mwekezaji Mtanzania kwa gharama ya takribani Shilingi Bilioni 26.4

Akiwa kiwandani hapo, Rais Magufuli amesema Serikali yake haitatoa fidia kwa watu ambao wanadai kulipwa fidia kutokana na maeneo yao kuchukuliwa ili kupisha mradi wa ujenzi wa eneo la bandari na viwanda la Bagamoyo na ameagiza watu waliofanya njama za kulipwa fidia wakati hawakustahili fidia hizo warudishe fedha mara moja kabla hatua za kisheria hazijaanza kuchukuliwa dhidi yao.

Wakati huo huo,  Rais Magufuli amesema Serikali yake haitaruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari watakaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Rais Magufuli amesema Serikali ina wajibu wa kulinda misingi ya kitaifa na kusimamia mienendo ya wanafunzi wawapo shuleni na amesisitiza kuwa kuwaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo kutasababisha wanafunzi wengi kujihusisha na vitendo vya mapenzi shuleni.


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64

 Rais Dk John Magufuli leo Juni 22, 2017, amezindua barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata yenye urefu wa Kilometa 64 na kuipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wote waliofanikisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo inasaidia kutatua tatizo la msongamano wa magari katika barabara ya Chalinze – Dar es Salaam na inapita katika eneo la Bagamoyo ambalo litajengwa bandari mpya na eneo la viwanda.

Ujenzi wa barabara hiyo yenye madaraja makubwa matatu umegharimu Shilingi Bilioni 213 ikiwa ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani PwaniRais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani

Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani PwaniMtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani PwaniMtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.