Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.


Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 28 May 2017

BARAZA KUU LA CHADEMA KATIKA PICHA

 MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendelea CHADEMA, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo uliofanyika Mkoani Dodoma Mei 27,2017.
 Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Vincent Mashinji akizungumza
 Meza kuu
 Mwenyekiti wa CHADEM, Freeman Mbowe akisoma taarifa za chama. 
Picha zote na Mroki Mroki.
 Wajumbe wa Baraza Kuu wakiwa katika Mkutano huo mjini Dodoma
 Wimbo wa Taifa uliimbwa
 Dua ilifanyika kabla ya kuanza mkutano huo.
 Wajumbe wakiwa mkutanoni
 Wajumbe ambao ni Wabunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Dodoma, Dk Immaculate Sware (kushoto) na Devotha Minja wa Morogoro.

Wajumbe wakifuatilia mkutano huo.


JUMUIYA YA MADOLA YA WAPIGA MSASA WABUNGE KUTOKA NCHI 16

Wajumbe wa Bunge la Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa Mafunzo ya wiki moja yalioandaliwa na Bunge hilo, katika mafunzo hayo Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limewakilishwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Baraza la Wawakilishi Zanzibar limewakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said wakishiriki katika masomo ya wiki pamoja huko Afrika Kusini University of Wits ambapo jumla ya Wabunge kutoka nchi 16 kutoka Jumuiya za Madola wameshiriki masomo hayo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika Nchini Afrika Kusini yalioandaliwa na Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola, akieleza kuhusiana na umuhimu wa kamati za kudumu za mabunge ya Jumuiya Madola kuelekea karne 21. 

Kutoka kushoto ni Mbunge kutoka India Ajay Misra, Naibu Spika Tanzania Dr Tulia Ackson, Seneta kutoka Jamaica Charles Pearnel na Mussa Dlamini Swaziland. Masomo hayo yanafanyika Johanessberg University of Witwatersrand kwa wiki moja na kudhaminiwa na Commonwealth Wealth. 
Wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naibu Spika Dr.Tulia Ackson pamoja Simai Mohammed Said kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa masomomi South Africa University of Witwatersrand wakibadilishana mawazo na Mbunge wa Swaziland Mhe Mussa Dlamini
Naibu wa Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson akisikilizwa kwa umakini na washiriki wenzake. Kutoka kushoto Mhe.Simai Mohammed Said ( Zanzibar ) Pearnel Charles Junior ( Jamaica) Mussa Dlamini ( Swaziland ) na Ajay Misra ( India).
Waheshimiwa Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika mafunzo  Nchini South Africa. wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini. 
Wajumbe kutoka Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ( Commonwealth Countries) wakitembelea Mahakama ya Katiba ( Constitutional Court ) katika mji wa Johannesburg.
Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo hayo kutoka  kushoto  Mbunge wa Jamaica.Mhe.Heroy Clarke ( MP), Charles Pearnel Seneta pia akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Jamaica, Stewart Michael ( MP) na Victor Wright ( MP ). 
Mjumbe kutoka Jumuiya ya Madola pia akiwa Mwakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na Profesa David Everatt ambaye ni Kiongozi wa Skuli ya Utawala katika University of Wits, South Afrika. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson akitoa nasaha zake za shukrani kwa niaba ya Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola walioshiriki mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa University of Witwaterstrand, Johannesburg South Africa.


CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA) CHAFANYA MKUTANO WAKE WA MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM

1
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka akfungua mkutano wa mwaka wa Chama hicho ulioshirikisha wanachama wake ambao ni wanasheria wanawake, Mkutano huo umefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam na kujadili mambo kadhaa yakiwemo mafanikio na changamoto zinazokabili chama chao pamoja na jamii kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
2 3
Kutoka kulia ni Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA), Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka, Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA) na Lulu Ngwanakilala Mtoa mada katika mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyojadiliwa na washiriki wa mkutano huo.
4
Mtoa mada Shamshard Remhamtulla akizungumza katika mmkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
5
Kutoka kulia ni Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA), Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka, Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA).
6
Lulu Ngwanakilala Mtoa mada akizungumza jambo na washiriki wa mkutano wa Chama cha Wanasheria wanawake wa mwaka uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
7
Mtoa Mada Madeline Kimei kulia akijiandaa kutoa mada katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


Saturday, 27 May 2017

VIGEZO KUZINGATIWA KWA WANAFUNZI WANAOKWENDA KUSOMA VYUO NJE YA NCHI

 Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya  akizungumza akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda  katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.
Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakitembelea  mabanda katika  maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India.leo jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya akiwa katika picha ya  watanzania  25 waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo leo jijini Dar es  Salaam.
TUME ya Vyuo  Vikuu Nchini  (TCU) imesema kuwa wanaokwenda  kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa  kuangaliwa vigezo ambavyo vinahitajika.

Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje na ndani anatakiwa kuwa ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.

Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika  tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu,  akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.

Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali.
Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.

Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link  (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India  iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU  kwa ajili ya kuhakikiwa.

 Maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yamesimamiwa na kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kuteuliwa na Balozi wa India.


SIMBA MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA FA TANZANIA BARA

TIMU ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam leo imetazwa rasmi kuwa Mabingwa wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (FA) baada ya kuilaza Mbao FC ya Jiji Mwanza kwa mabao 2-1 katika mtanange wa vuta ni kuvute uliochezwa kwa dika 120 katika dimba la Jamhuri Mjini Dodoma leo. Anaandika Mroki Mroki-Dodoma.

Simba na Mbao zilicheza mbele ya mshabiki lukuki kutoka mji wa Dodoma na mikoa jirani wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ambapo pia mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.


Kufuatia ushindi huo sasa Simba itaiwakilisha nchi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba imekuwa timu ya pili kutwa kombe hilo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) tangu kuanzishwa ambapo watani zao Yanga ndio walikuwa wakwanza kutwaa kombe hilo.

Aliyewainua viti maelfu ya mashabiki wa Simba alikuwa ni mchezaji wa kimataifa wa Simba, mzaliwa wa Ivory Coast, Frederick Blagnon baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza kunako dakika ya 95 na kuamsha matumaini ya wakongwe hao wa Mtaa wa Msimbazi ya kutwaa ubingwa wa FA.

Dakika ya 109 ya mchezo huo mchezaji wa Mbao FC, Robert Ndaki alizima furaha za Simba uwanja wa Jamhuri na viunga vya Mji wa Dodoma ambao tayari walianza kushangilia ubingwa kwa kuifungia timu yake bao safi kufuatia makosa ya walinzi wa Simba na kupiga majalo iliyo mpita mlinda mlango wa Simba.

Dakika ya 119 palitokea piganikupige katika lango la yanga na katika harakati za kuokoa mpira mchezaji wa Mbao aliunawa mpira na mwamuzi wa Ahmed Kikumbo kutoka Dodoma kuamuru mwaju wa penati upige ambapo almanusra mwamuzi aambulie kichapo.

Chiza Kichuya alipiga mkwaju wa penati kunako dakika ya 120 ishirini ambapo bao hilo lilidumu hadi kipenga cha mwisho Simba 2 na mbao 1.

Vikosi vya timu zote mbili vilivyoshuka dimbani hii leo ni
MBAO FC: Benedict Haule, Asante Kwasi, Yussuf Ndikumana, David Mwasa, Salmin Hozza, Boniface Maganga, George Sangija/Dickson Ambundo dk59/Rajesh Kotecha dk104, Jamal Mwambeleko, Pius Buswita, Habib Hajji/Robert Ndaki dk104 na Ibrahim Njohole: KOCHA: Etienne Ndayiragile

SIMBA SC: Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tahabalala’/Abdi Banda dk51, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Said Ndemla/Frederick Blagnon dk80 na Juma Luizio/Ibrahim Hajib dk60. KOCHA: Joseph Omong

WAAMUZI: Ahmed Kikumbo alisaidiwa na Mohamed Mkono na Omary Juma lakini Msimamizi wa Mchezo alikuwa Florentina Zablon. 


Friday, 26 May 2017

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA UNUNUZI WA MBOLEA KWA PAMOJAKaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga.         
**************

Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi utakaosaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Lazaro Kitandu alisema uamuzi huo wa kuanzisha mfumo mpya umekuja baada ya Serikali kugundua kuwa kwa muda mrefu matumizi ya mbolea hapa nchini si ya kuridhisha kutokana na bei ya mbolea kuwa juu.

“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mbolea imeanzisha mfumo huu baada kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam waelekezi wa ndani na nje ya nchi na kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja” Alisema Kitandu.

Kitandu alieleza kuwa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA), Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye matumizi ya chini ya mbolea kwa kutumia kilo 19 za virutubisho hivyo kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo ambapo kiasi hicho hakiendani na malengo ya azimio la Maputo la nchi za SADC linalotaka kufikia angalau kilo 50 kwa hekta moja.

Alisema kuwa kwa msimu wa mwaka 2017/2018 mfumo huo utaanza na aina mbili tu za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na mbolea nyingine zitafuata baadaye kadri itakavyoonekana mfumo huo kuleta manufaa kwa wakulima.

Akifafanua kuhusu faida za mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja, Kitandu alisema utasaidia kuimarisha utaratibu wa usambazaji wa mbolea ambapo wadau wote watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani. 

Kwa mujibu wa Kitandu pia mfumo huo utawezesha wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

“Ununuzi wa mbolea kwa pamoja pia utasaidia kudhibiti bei ya mbolea iwapo kutajitokeza ongezeka lisilokuwa na sababu (soko holela) kwa kuwa bei itatangazwa kwa kuzingatia bei halisi ya mbolea, gharama halisi za usafirishaji wa mbolea, tozo mbalimbali na kiwango stahiki cha faida ya mfanya biashara” alibainisha Kitandu.

Serikali kupitia mfumo huu inatarajia matokeo chanya katika kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima hivyo kuongezeka kwa matumizi ya mbolea na uzalishaji wenye tija ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.