Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF jijini Arusha juzi ,wakati akifunga mkutano huo ambapo aliwataka wastaafu watarajiwa kujiandaa kustaafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya kuongeza kipato hali itakayosaidia wao kujiendeleza kimaisha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema watumishi wakajianda mapema wakiwemo wa umma na sekta binafsi
Mkurugenzi
wa mfuko wa GEPF Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali
ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo
ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla
Mwenyekiti wa bodi Ya
wadhamini,wa mfuko huo Joyce shaidi akizungumza katika mkutano huo
Kulia ni mkuu wa kitengo cha kusimamia amana za wawekezaji katika benki ya CRDB Bw.Masumai Ahmed
Wadau wa mkutano wakiwa wamesimama kuashiria kumalizika kwa mkutano huo
******************
Mkuu wa mkoa
wa arusha Mrisho Gambo amewataka Watumishi katika sekta za umma kuacha
dhana ya kuogopa kustaafu kazi pindi wanapofikia muda wa kustaafu
badala yake wanatakiwa kujipanga kabla muda haujafika.
Aidha watumishi
wanaogopa kustaafu kwa kuwa wanaanza kujiandaa miaka miwili kabla hali
ambayo inawapa uoga mkubwa wastaafu watarajiwa
Mrisho Gambo
ameyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa mfuko wa mafao ya
kustaafu (GEPF) uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Gambo alisema
kuwa kwa sasa wastaafu wanapata magonjwa ya moyo kwa kuwa hawajajiandaa
na kubuni miradi ambayo inaweza kuwaletea vipato kama mishahara yao
ilivyokuwa
Alisema
maandalizi ni muimu sana kwa wafanyakazi hata kama bado hawajafikia muda
wa kustaafu kwani kustaafu sio ajali bali ni kitu ambacho kipo na
kimeshawekewa utaratibu na mifuko ya hifadhi jamii hapa nchini pamoja na
Serikali.
"Wastaafu wengi
wanakufa pindi wanapoacha kazi hiyo sio sawa ni lazima kila mtu
ajiandae na abuni njia mojawapo ya kujiongezea kipato kwani hata kama
ukijiajiri mwenyewe ni lazima utapata kipato kama kile ulicho kuwa
unalipwa kama sehemu ya ujira wako "aliongeza Gambo.
Wakati huo huo
aliwataka wakuu wa mifuko ya hifadhi hapa nchini kuhakikisha kuwa
wanatoa elimu ya kujiandaa kustaafu kwa wafanyakazi wake kwani uzoefu
unaonesha kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi hawana elimu hiyo
Alisema kama
wafanyakazi watakuwa na elimu hiyo ya kustaafu basi itasaidia kupunguza
ulalamishi kwa wastaafu,magonjwa ya moyo,vifo visivyo na lazima
vinavyotokea.
Naye mkurugenzi
wa mfuko huo Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali
ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo
ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment