Mtafiti
Mwandamizi Mshiriki kutoka Mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta (PS3), Dk.Fenohasina Rakotondrazaka, akitoa mada
kwa Maofisa Habari na Tehama kutoka Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa ya
Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wanaoshiriki mafunzo elekezi ya
uwekaji wa taarifa katika tovuti yaliyoandaliwa na PS3 na kufanyika jijini
Mwanza.
Na Mroki Mrok, TSN Digital Mwanza
KATIKA kuhakikisha Serikali inaboresha
usimamizi wan a ushirikishwaji wa wananchi katika Nyanja ya habari na
mawasiliano kwa umma, Maofisa habari na Tehama kutoka Sekreatarieti za mikoa
mitano na mamlaka za Serikali za mitaa 37 kutoka katika kanda ya Ziwa wapo
jijini Mwanza kwaajili ya mafunzo maalum ya uendeshaji tovuti zao.
Takribani juma moja maofisa
hao watapatiwa mbinu mbalimbali za kuendesha tovuti zao ambazo mapema wiki
ijayo zinataraji kuzinduliwa baada ya mafunzo kwa maofisa hao kukamilika.
Mradi huo unaendeshwa ikiwa ni
utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni mradi wa miaka mitano ambao unatekelezwa na
unafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya
Tanzania bara.
PS3 inaimarisha mifumo ya
sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji
wa taarifa, na tafiti tendaji.
Ushirkiano huu wa PS3 katika
ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na
matumizi ya huduma za umma, hususani kwa jamii ambazo hazijanufaika vya
kutosha.
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao
(eGA), Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Shirika la Kimarekani
la Misaada ya Kimaendeleo (USAID) waliunda mfumo ambao utafanya kazi ya
kuhuisha mfumo kwa kushirikisha taarifa ambazo zitajenga ufanisi, uwazi na
uaminifu wa umma.
Maofisa
Habari na Tehama kutoka Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza,
Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakishiriki katika mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika
tovuti yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
na kufanyika jijini Mwanza.
Maofisa
Habari na Tehama kutoka Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza,
Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakishiriki katika mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika
tovuti yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
na kufanyika jijini Mwanza.
Mofisa Habari na Tehama wakiwasilisha tovuti zao.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment