MUIGIZAJI na Muongozaji Filamu,
Elizabeth Michael (Lulu) ,22, leo amehukumuiwa
kifungo cha Miaka Miwili gerezani baada ya Mahaka Kuu Tanzania, kumtia hatiani kwa kosa la
kumuua Bila kukusudia. Anaandika Mroki Mroki wa Daily News Digital.
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.
Alisema Aprili 12, 2012 ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Lulu kufikishwa Mahakamani ambapo alifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma za mauaji ya marehemu Kanumba.
Lakini baadae baada ya kusota rumande kwa takribani miezi kumi, Lulu alibadilishiwa mashitaka na kushitakiwa kwa mauaji ya bila kukusudia, shtaka lililomuwezesha kuwa nje kwa dhamana hadi leo.
Tukio hilo lilitokea mnamo Aprili
6, 2012 huko Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam wakati ikielezwa kuwa wasanii
hao wawili wakiwa ni marafiki wakaribu.
LAKINI ELIZABETH AU LULU NINANI?
Diana Elizabeth Michael Kimemeta
kama alivyotambulika na wazazi wake, Michel Kimemeta na mama Lucrecia Kalugira
alizaliwa Aprili 16,1995. Baadae alianza elimu ya Msingi katika shule ya
Remnant baadaadae katika sekondari za Perfect Vision na St Mary’s za jijini Dar
es Salaam na kujiunga na elimu ya juu pale alipojiunga na Chuo cha utumishi wa
Umma kuchukua Diploma ya Meneja Rasilimali watu.
Lulu alianza kuonesha kipaji chake
cha ugizaji akiwa bado mtoto na hapa ni akiwa na umri wa miaka mitano tu, pale
Mwigizaji Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ alipomchukua na kujiunga nae katika Kundi
la Sanaa la Kaole.
Baada ya kujiunga na Kaole Lulu
alianza kushiriki na kuonekana katika michezo mbalimbali ya kuigiza ya kundi
hilo iliyokuwa iukirushwa na ITV na miongoni mwa michezo hiyo ni pamoja na Zizimo, Dira, Baragumu, Gharika, Taswira,
Tufani, Tetemo, Jahazi, Sarafu na Demokrasia.
Mwaka
2005 Lulu alianza kuingia katika filamu ambapo alianza kutoa filamu yake ya
kwanza iliyojulikana kama Misukosuko. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Pia
aliwahi kushiriki katika michezo ya kuigiza ya Redioni kama ule wa Wahapahapa lioshiriki
mwaka 2009, pia alichez mchezo wa Mainda ambao ulilenga kutoa elimu ya umuhimu
wa mawasiliano baina ya mzazi na mtoto katika kulinda vijana wakati wa makuzi
yao.
Lulu
pi ameshiriki na kuonekan katika filamu mbalimbali na majririda maalum zaidi ya
30. Mwezi Agosti mwaka 2013 alizindua filamu yake aliyoipa jina la Foolish
Age, ambayo mbali na kushirtiki kuicheza lakini alikuwa pia kama
mtaryarishaji wa Filamu hiyo.
Filamu
hiyo iliyozinduliwa Mlimani City jijini Dar es Salaam ilichaguliwa kuwa
miongoni mwa filamu zilizooneshwa katikia Tamasha la Kimataifa la Filamu
Zanzibar (ZIFF) ya mwaka 2014.
Filamu
ya Foolish Age ilichaguliwa tena katika Tuzo za watu 2014 ambapo
ilishinda tuzo ya Filamu iliyopendwa huku yeye mwenyewe akishinda tuzo ya
Mwigizaji aliyependwa katika Filamu hiyo.
Mwaka
uliofuata 2016 alitoa filamu mpya ya tatu aliyoipa jina la Ni Noma ambayo ilikuwa ikiuzwa kupitia
mitandao katika App malum ya ProinBox
Ubalozi
Mwaka
2013 alichaguliwa kuwa Balozi wa Tamasha la Filamu Dar es Salaam (DFF) ambapo
pia filamu yake ya Foolish Age ilioneshwa katika tamasha hilo.
Mnamo
mwaka 2014 Lulu aliingia mkataba na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kuwa
Muongozaji wa kipindi Airtel Yatosha
TV Show.
Mwaka
2015, Lulu alisaini mkataba na wa kuwa Balozi wa Paisha Tanzania ambapo alikuwa
Balozi wa App ya Paisha ambayo ilikuwa ikijihusisha na biashara mtandaoni.
Aliendelea
zaidi kung’ara na mwaka 2016, alitangaza na kampuni ya Hengan Baby Products & Sanitary
Co. Ltd. (Tanzania) kuwa Balozi wa bidhaa yake ya taulo za akina mama za Freestyle.
Mwezi
Oktoba Mwaka huu, Azam Media Tanzania kupitia Chaneli yake ya Sinema zetu, ilimtangaza
Lulu kuwa Balozi Maalum wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Sinema Zetu (SZIFF).
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment