HABARI iliyotufikia hivi punde
inaarifu kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (pichani). Anaandika Mroki Mroki-dailynewstzonline blog.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa
inaeleza kuwa Ngalamgosi amesimamishwa kazi kuanzia leo Juni 11,2017’
Mwishoni mwa wiki
inayomalizika leo Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari ilitoa
taarifa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
imepokea maombi ya kuongeza muda
wa leseni ya kuzalisha
umeme kutoka kwa kampuni
ya uzalishaji umeme
ya Independent Power Tanzania
Limited (IPTL) (“Mwombaji”).
Hivyo basi,EWURA ina uarifu umma na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni
au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.
Taarifa za ilitolewa chini
ya kifungu cha
19 cha Sheria
ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma
za Nishati na
Maji, Sura ya 414
ya Sheria za
Tanzania na kifungu
cha 8 cha Sheria ya
Umeme, Sura ya
131 ya Sheria
za Tanzania.
Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wanachi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.
Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dk. John
Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa
na jaribio la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzi.
Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO akimtoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikokuwa akifundisha.
Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya ya
bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za
uzalishaji wa umeme.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment