Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari St Getruda iliyopo Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma
wakiulaki mwenge wa uhuru jana,uliofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa
ujumbe wa mwenge kwa mwaka 2017 ambapo kiongozi wa mwenge kitaifa
Amouru Hamad Amour amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanaongeza bidii
katika masomo yao ili waweze kufanikisha ndoto walizonazo kimaisha. Picha zote na Muhidin Amri.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kushoto,akipokea mwenge wa
uhuru jana kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka
katika kijiji cha Mahanje halmashauri ya wilaya ya Madaba mara baada ya
mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Njombe
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2017, Amour Hamad
Amour,akimsikiliza mwenyekiti wa Mahanje Saccos Wilayani Songea, Arika
Mgina mara baada ya kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika
Saccos hiyo na kupongeza uongozi kwa kazi nzuri inayofanya ya kuwainua
wananchi kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Shafi Mpenda, akifuatiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour akiinua
ndoo ya maji jana mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji safi na
salama katika kijiji cha Lilondo halmashauri ya wilaya ya Madaba,wakati
wa siku ya kwanza ya mbio za mwenge wa uhuru mkoani Ruvuma,kulia ni
mkazi wa kijiji hicho Ostella Mwenda.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour (kulia) na Mkimbiza mwenge kitaifa Frederick Ndahani wakiomba dua ya kuwaombea
waasisi wa mwenge wa uhuru Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa
Zanzibar hayati Abeid Karume katika kijiji cha Lutukira katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,mara baada ya kukagua kikundi cha vijana
waendesha boda boda wanaojishuhulisha na kilimo cha mahindi kijijini
hapo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment