Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
WATANZANIA hususan wale
wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa
kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na
kubadilisha vyeti mpya
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata
huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa.
Waziri Mwijage amesema duniani
ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua
ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu
haina mgonjwa wa homa ya manjano.
Aidha amesema maambukizi ya
ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na
inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata
chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako.
Hata hivyo aliwatahadharisha
wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema
wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani
kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina
uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala
Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na
Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo
vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa
rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata
chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa
homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali.
Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani
hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika
tena.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment