Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeme, tayari kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeme kwenye eneo la kiwanda kinachomilikiwa na mfanyabishara maarufu jijini, Bw. Fida Hussein kilichiko Vingunguti leo Mei 4, 2017
Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius
Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao
makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
Mhandisi
wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza
na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“MANENO
ni mawili tu “KA na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo
yalikuwa ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme mkoani Mtwara miezi michche iliyopita.
Kufuatia
maagizo hayo ya Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano na waandihi
wa habari na kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za umeme kuwa walipe
madeni yao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.
Baada
ya tangazo hilo, baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo,
naye aliitisha mkutano na wanahabari na kueleza kuwa JWTZ italipa sdeni lake na
kuagiza wahusika wafanye hivyo mara moja.
Leo
hii Mei 4, 2017, Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali,
aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa taasisi za umma na
binafsi zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa jumla ya shilingi Bilioni
7, ambapo taasisi za serikali pekee zilikuwa na deni la shilingi bilioni 6 na kwa sasa tayari zimelipa
jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi bikioni 4.
“Hizi
taasisi za umma tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na
tunaendelea kuwahimiza wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.”
Alisema Mhandisi Nangali.
Aidha
alisema taasisi binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya hizo
hazijaingia mkataba wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo
akatahadharisha kuwa TANESCO haitasita kuchukua hatua za kusitisha huduma ya
umeme na kwa kuonyesha kuwa Shirika halifanyi mzaha, leo hii kampuni mbili moja
ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Fida Hussein iliyoko Vingunguti wilayani
humo imesitishiwa huduma ya umeme kufuatia deni la shilingi Milioni 29.
Kampuni
nyingine iliyoonja joto ya jiwe ni Iprint
iliyoko eneo la Banda la Ngozi kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo
hadi kufikia leo Mei 4, 2017 ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni 16,95.
Maafisa
wa TANESCO waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa sugu,
walikuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017 kampuni hizo
mbili zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.
Hii ni stakabadhi ya leo Mei 4, 2017 ikionyesha kampuni ya I print ikidaiwa shilinhi milioni 16.95
Maafisa wa TANESCO makao makuu, wakimsikiliza meneja wa kiwanda cha Fida Hussein(kulia)
Wanahabari wakiwa kazini
Mhandisi Athanasius Nangali(kulia), akiongea na waandishi wa habari.
Source: NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Source: NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment