Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 26 October 2017

UFAFANUZI KUHUSU KUKATIKA KWA UMEME KUANZIA TAREHE 25 - 26 OKTOBA, 2017



Wizara ya Nishati inawaomba radhi wananchi kufuatia katizo la Umeme lililotokea tarehe 25 na 26 Oktoba, 2017 kuanzia saa 12:30 Jioni.

Katizo hilo limesababishwa na kukatika kwa waya (Cable) wa kupeleka Umeme kwenye Geti la kufungulia Maji katika Bwawa la Kidatu linalozalisha Umeme wa kiasi cha megawati  204.

Hitilafu hiyo ilisababisha mtambo wa Kidatu pamoja na mitambo mingine ya kuzalisha Umeme katika sehemu mbalimbali nchini kutoka kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye mfumo wa Gridi hiyo kukosa Umeme.

Serikali imefanya jitihada za kurejesha Umeme kuanzia tarehe 25 Oktoba, 2017, usiku ili kuhakikisha kuwa Umeme unarudi katika hali yake ya kawaida kwa nchi nzima. 

Hadi kufikia tarehe 26 Oktoba, 2017, baadhi ya mitambo imeanza kufanya kazi na hivyo maeneo mengi nchini yanapata Umeme.

Aidha, mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha Umeme wa Megawati 129, utaanza kuzalisha Umeme ifikapo tarehe 27 Oktoba, 2017, saa 5:00 asubuhi, hivyo kufanya maeneo yote nchini kupata Umeme. 

Hatua za dharura na za muda mrefu zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha tatizo la kukatika kwa Umeme halijirudii. Hatua hizo ni pamoja na kukarabatiwa kwa mitambo yote ya kuzalisha Umeme iliyoharibika ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Hatua nyingine ni kukarabati mfumo wa kituo cha kudhibiti mifumo ya Umeme (Grid Control Centre) ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo utoaji wa taarifa mbalimbali za hali ya udhibiti wa mfumo wa Umeme katika Gridi ya Taifa.

Imetolewa na,
NAIBU KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI
26 Oktoba, 2017


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment