Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.akipata maelezo Jana March 24/2018kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Ruangwa Mkoa wa Lindi(DED) Bwana Andrea Chezue. Jinsi muonekano wa Uwanja wa Michezo wa kisasa Wilaya ya Rungwa utakavyo fanana
*************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka
wakazi wa wilaya ya Ruangwa washirikiane kuhakikisha ndoto ya timu yao ya mpira
wa miguu ya Namungo FC ya kucheza ligi kuu inatimia.
Amesema timu hiyo limeupa mkoawa Lindi
na wilaya hiyo heshima kubwa imepanda imepanda daraja kutoka ligi daraja la
pili kwenda daraja la kwanza katika msimu wa 2018/2019.
Waziri Mkuu ameyasema leo (Jumamosi,
Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa wilaya hiyo kwenye eneo la
Namungo na kuwaomba waendelee kuisaidia timu hiyo ili iweze kupanda na kucheza
ligi kuu.
Amesema daraja la kwanza linaushindani
mkubwa zaidi, hivyo ameutaka uongozi wa timu hiyo kutumia siku 120 zilisalia
kabla ya kuanza kwa ligi kwa kufanya maandalizi ya kuisuka timu hiyo kabla ya
kuanza mashindano.
“Lazima timu yetu ya Namungo FC icheze
daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana
kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”
Pia Waziri Mkuu amekagua eneo la ujenzi
wa uwanja wa mpira wa miguu wilayani Ruangwa unaojengwa katika kitongoji cha
Mtichi kata ya Nachingwea ambacho kinatarajiwa tumiwa na timu ya Namungo FC.
Awali, Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. Hassan
Kungu amesema Namungo FC imefanikiwa kupanda daraja na sasa inashiriki ligi
daraja la kwanza na malengo yao ni kuhakikisha inafanya vizuri ili iweze
kucheza ligi kuu.
“Mbali na mafanikio hayo, timu yetu ya
Namungo FC inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uwanja wenye
viwango vya kuweza kucheza mashindano hao pamoja na chombo cha usafiri.”
Akizungumzia historia ya Namungo FC,
Bw. Kungu amesema timu hiyo ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya
dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya
mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment