Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 31 August 2017

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omar Mahita Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa  (TISS), Cornel Lundu Apson mara baada ya mazungumzo yake na viongozi wastaafu na wa sasa wa vyombo  vya Ulinzi na Usalama  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Omar Mahita(IGP Mstaafu), Said Mwema(IGP Mstaafu) pamoja na Ernest Mangu(IGP Mstaafu) Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wasasa na wastaafu wa Magereza Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.
                                                      *****************
RAIS Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wastaafu na viongozi wa sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.


Viongozi hao ni Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Wakuu wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Wakuu wa Idara ya Uhamiaji, Wakuu wa Jeshi la Magereza na Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Baada ya mazungumzo hayo viongozi wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaita na kufanya nao mazungumzo, ambayo yamewawezesha kubadilishana mawazo na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao na viongozi wa sasa wa vyombo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais Magufuli na tunampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, sio jambo la kuficha amefanya kazi nzuri, na kila mmoja wetu amezungumza hilo na tunamtakia kila la heri ili aweze kuendeleza pale alipofika, kwa kweli tumefurahi sana,” amesema  Cornel Apson, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Mstaafu. 

“Tumeona ni jambo jipya na halijawahi kutokea kwa Rais kutuita viongozi wastaafu, nchi yetu chini ya Mhe. Magufuli inakwenda vizuri, Watanzania tuiunge mkono Serikali hii kwa sababu inatuelekeza mahali kuzuri,” amesema Jenerali Mstaafu Robert Mboma, Mkuu wa JWTZ Mstaafu. 

Viongozi hao wamempongeza, Rais Magufuli kwa uendeshaji mzuri wa Serikali, hususani katika kusimamia uchumi, kupiga vita rushwa, kujenga nidhamu kwa watumishi wa umma na wamemuahidi kuendeleza zaidi ushirikiano na viongozi waliopo sasa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu , erson Msigwa amesema Rais Magufuli amekutana na viongozi hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano imara zaidi kwa viongozi wastaafu na viongozi wa sasa katika kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama wa nchi.

“Rais Magufuli amefurahishwa sana na mwitikio wa viongozi hawa wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama na amewahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza itaendeleza ushirikiano nao ili kunufaika na uzoefu wao,” amesema Msigwa